Naomba msaada kwa haya yanayonikabili

Naomba msaada kwa haya yanayonikabili

mjasiria2mbo

Member
Joined
Apr 23, 2014
Posts
43
Reaction score
18
Jambo la kwanza nina mtoto wa miez 3,huyu mtoto anacheua utadhan anatapika sijui tatizo ni nini!

Tatizo la pili...... Bado sijaanza period ila kama wiki mbili zilzopita nilikutana na mume wangu sasa je,kuna uwezekano wa kuwa nimepata mimba??

Na je,kukutana na mume wangu kunaweza leta tatizo lolote kwa mtoto?

Asanteni!
 
Jambo la kwanza nina mtoto wa miez 3,huyu mtoto anacheua utadhan anatapika sijui tatizo ni nini??? Tatizo la pili...... Bado sijaanza period ila kama wiki mbili zilzopita nilikutana na mume wangu sasa je,kuna uwezekano wa kuwa nimepata mimba?? Na je,kukutana na mume wangu kunaweza leta tatizo lolote kwa mtoto???? Asanteni!


kama ulikuwa hujaanza kupata hedhi siyo rahisi kupata mimba maana hakuna yai linalopevuka,mara nyingi hutokea kwa baadhi ya wanawake hasa miezi ya mwanzo kutokana na kunyonyesha mtoto vizuri, vichocheo vinavyohusika na kukomaa kwa yai huzalishwa kidogo kama mtoto ananyonya vema,lakini kadri mama anavyopunguza kumnyonyesha mtoto hivyo vichocheo vyanavyohusika na kupevusha yai huongezeka na linapopevuka lisipopata mbegu ya mwanaume linaharibika,hapa kizazi kinajisafisha hapo ndo hiyo inaitwa hedhi.

lakini kuna wanawake wachache waliojaliwa wao wakiwa wananyonyesha huwa hawapati hedhi hata kama ni miaka mitatu,ndiyo maana unyonyeshaji inawekwa kama njia ya asili ya uzazi wa mpango.Hivyo hawa ni ruksa kula tunda siku zote.

Hakuna madhara ya kukutana na mmeo kwa mtoto zaidi ya kupata Mimba ikiwa kama unapata siku zako ukikutana na mmeo siku za hatari.

suala la kucheua sana nafikiri usimzidishie sana kumnyonyesha ni vema ukawa unamnyonyenya kidogokidogo ila mara nyingi,kuliko kumnyonyesha maziwa mengi kwa wakati mmoja.
 
Asante Mkuu Ng'wana ong'wa kulwa!! Ngoja mpunguzie kunyonya japo ni mbishi hatari!!! Asante sana
 
mjasiria2mbo, Kama hauko tayari kuwa na mtoto mwingine ni vizuri sana kutumia condom au njia zozote za uzazi wa mipango, aliyosema ng`wana ong`wa kulwa ni sawa ila sio 100% safe.
 
Last edited by a moderator:
Jambo la kwanza nina mtoto wa miez 3,huyu mtoto anacheua utadhan anatapika sijui tatizo ni nini??? Tatizo la pili...... Bado sijaanza period ila kama wiki mbili zilzopita nilikutana na mume wangu sasa je,kuna uwezekano wa kuwa nimepata mimba?? Na je,kukutana na mume wangu kunaweza leta tatizo lolote kwa mtoto???? Asanteni!

Ndo maana ukijifungua unashauriwa kuanza uzazi wa mpango Mara tu 40 inapoisha wanawake wengi wamejikuta na mimba kwa risk uliofanya wewe .hivo zingatia hilo after two weeks kapime upt uwe na uhakika ama utajikuta unamwachisha mtoto kunyonya akiwa na miezi sita afu we uendelee kulea ujauzito
 
Asante Mkuu Ng'wana ong'wa kulwa!! Ngoja mpunguzie kunyonya japo ni mbishi hatari!!! Asante sana

yaaa mnyonyeshe kidogokidogo baada ya muda unampa haki yake tena usimpe full dozi kwa wakati mmoja wengine mpaka hutapika wakipigwa dozi sawasawa.
 
Back
Top Bottom