Naomba msaada kwa wenye uzoefu mikopo ya Azania bank kwa wanachama wa NSSF

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Wakuu nawasalimu. Naomba kama Kuna mtu ana uelewa na Hili anisaidie. Azania bank wanatoa mikopo kwa wanachama wa NSSF. Kama mtu aliachishwa kazi kipindi cha janga la Corona kwa sababu kampuni iliamua kupunguza wafanyakazi na hakutoa mafao yake NSSF na ameamua kutokuajiriwa tena anaweza kupata mkopo?
 
Nimejaribu kupiga Simu customer service ya Azania bank nikapata tu automated reply. Nadhani Jumapili hawana watu ofisini
 
Wakuu nawasalimu. Naomba kama Kuna mtu ana uelewa na Hili anisaidie. Azania bank wanatoa mikopo kwa wanachama wa NSSF. Kama mtu aliachishwa kazi kipindi cha janga la Corona kwa sababu kampuni iliamua kupunguza wafanyakazi na hakutoa mafao yake NSSF na ameamua kutokuajiriwa tena anaweza kupata mkopo?
Kwanza tuanze na hicho unachokijua.
Je ni kweli kuwa NSSF wanatoa mikopo maalum kwa wanachama wa NSSF?
Je dhamana inakuwa ni huo uanachama au vipi?
Vigezo vingine zaidi ya uanachama ni vipi?
 
Mikopo inatolewa Azania bank kwa wanachama wa NSSF
 
Wakuu nimewasiliana na Azania bank Leo wameniambia hawajafikia mkataba na NSSF wa kukopesha wanachama. Nimeshangaa sana maana hii habari ni ya siku nyingi tu. Ngoja niwatafute NSSF nijiridhishe na Hili jibu
 
Mambo ya bongo haya . Mtu ana akiba ya mamilioni lakini hakopesheki
 
Nimewatafuta NSSF wala hakuna la maana waliloniambia. Naambiwa lazima uwe active member then upitie kwenye SACCOS. Ukiwauliza Azania bank wanakuambia bado hawajafikia mkataba na NSSF wa kutoa mikopo. A total confusion🤔😬
 
Nimewatafuta NSSF wala hakuna la maana waliloniambia. Naambiwa lazima uwe active member then upitie kwenye SACCOS. Ukiwauliza Azania bank wanakuambia bado hawajafikia mkataba na NSSF wa kutoa mikopo. A total confusion[emoji848][emoji51]

unawezakuta customer care kote ulikopiga hawana idea na unachowauliza[emoji2][emoji2][emoji2]

bongo kila kitu kinawezekana.
 
Nimepiga customer care Dar hawakuwa na jibu wakaniunganisha na branch ya Arusha. Niliyeongea nae akasema yuko idara ya mikopo but majibu ndio hayo😬
 
Customer service zingine wala hazina idea na product wanayouza
 
HIYO MIKOPO INATOLEWA NA AZANIA BENKI MKUU,ILA UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KWENDA KWENYE OFISI ZA SIDO AU VETA HAO NDIO WATAKUKAGUA NA KUKUANDIKIA RECOMENDARION LETTER YA KUPELEKA AZANIA BENK
 
Nimepiga customer care Dar hawakuwa na jibu wakaniunganisha na branch ya Arusha. Niliyeongea nae akasema yuko idara ya mikopo but majibu ndio hayo😬
NENDA SIDO AU VETA NDIO WANA KUPA ZILE TAARIFA ZA AWALI
 
Back
Top Bottom