Naomba msaada, mtoto wangu anajinyea

Daaa umejibu kwa ukali mpaka nimeumia. Sina uhakika kama una mtoto tayari*. Binafsi nina mtoto wa umri uliozaidi ya huo, na bado naendelea kumfunza mwanangu hizo habari za kupupu. Ninachojua ni kuwa watoto wanatofautiana sana linapokuja suala la kujifunza kitu kipya. Wapo wanajifunza mapema na wanaochelewa. Kikubwa kwa mzazi ni uvumilivu.
 
Miaka 12 tu? Heri huyo. Kuna watu mpaka wanahitimu kidato cha sita bado.......
 
Wangu alikuwa hivyo hivyo, nikaanza kumchapa viboko, leo hii akisikia tu haja anakwenda mwenyewe chooni.
 
Mzoeeshe kukaa kwenye poti na kila ukijua ni mida yake ya kujisaidia mmwambie akae kwenye pot atazoea tu,pia mpime minyoo
We ndo umemaliza kila kitu mtoto lazima ajifunzie kwenye pot si unamwelekeza aende chooni mana anapata uoga..miaka ya nyuma kinamama walikua wanainyosha miguu yao na kuitanua kidogo kisha wanamkalisha mtoto anajisaidia na anajenga picha kuwa yupo chooni badae anazoea ila siku hizi utandawazi ndo kuna mambo ya kutumia poti vilevile kama mzazi/mlezi kuna zile lugha kali za kuwambia mtoto pindi akibanwa na haja si nzuri huwa zinawaathiri anaweza jifanya kaghairi kujisaidia kumbe ashaharibu..
 
Mie wangu nikimuweka kwenye poti analia utadhani poti lina mdudu nshachoka, anapupu kasimama utadhani ng'ombe
Yaan wa kwangu ni hvyo hivyo, ikimwambia ukisikia kupupu unatakiwa kwenda wapi? Anakujibu poti, ila kalilete sasa, balaah hataki kabisa kukaa, yaan wa kwako na wa kwangu wanafanana kabisa
 
Yaan wa kwangu ni hvyo hivyo, ikimwambia ukisikia kupupu unatakiwa kwenda wapi? Anakujibu poti, ila kalilete sasa, balaah hataki kabisa kukaa, yaan wa kwako na wa kwangu wanafanana kabisa
Mie nimeamua kumuacha, aendelee hivo hivo kama ng'ombe ha ha ha, anaenda pembeni anashika kitu anapupu akimaliza anarudi poti hataki kabisa
 
Hapo mkuu tafuta watalaam wa afya watakusaidia sanaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…