Naomba msaada mwenye kujua jinsi kilimo cha korosho, soko lake lipoje pia?

1Africa54

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
464
Reaction score
549
Wakuu naombeni anae jua kilimo Cha korosho kinaendeshwaje, bei ya korosho, jinsi ya kuongeza thamani nk
kilimo-cha-korosho-scaled-e1661587531401.jpg
 
Unachekesha sana hivi mkorosho ulijua ni mahindi ukipanda leo utavuna kesho
 
Kwa uzoefu mdogo nilionao kwa kuona, kwanza korosho ni zao kama maembe ukipanda leo utavuna baada ya kuanzia miaka mitatu na itategemea na aina ya mbegu uliyopanda, namna ulivyohudumia yaani madawa maji na uwiano kati ya mche mmoja na mwngne.

Katika ulimaji wa korosho watu wamegawanyika katika aina mbili ambapo kuna wenye mashamba na wasio na mashamba.
Wenye mashamba, wanalima kama kawaida yaani wanahudumia miti yao ya korosho kwa kusafisha na kupulizia dawa pale muda wa kufanya hivyo unapofika na hatimaye anavuna na kupeleka ghalani ambapo anapima kilo kisha anadubiri muda wa mnada ukifika ili kujua bei ya mzigo wake utakavyouzwa.

Kuna kundi la wasio na mashamba ambapo hawa hununua kidogo kidogo kutoka mashambani katika kipindi cha mavuno hadi wanapata mzigo wa kutosha kisha wanapeleka ghalani tayari kwa kisubiri mnada ili mzigo uuzwa..

Ni matumaini yangu unepata kitu kidogo sasa!!
 
Nimejifunza jambo kubwa hapa
 
Korosho ni zao la biashara na chakula.
Linasitawi zaidi maeneo ya joto na yenye mvua za kutosha.

Maeneo maarufa kwa kilimo cha korosho ni mkoa wa Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga.

Kilimo cha korosho unaotesha miche ya korosho kwenye viriba kisha kuviatika shambani mithili ya yule anayepanda miti ya mbao.

Pia waweza panda mbegu za mikorosho moja kwa moja kama mtu apandavyo mahindi japo njia hii haitumiki sana.

Eka moja inakuwa na wasitani wa mikorosho (miti ya korosho) 25 -35 kwa mikorosho ya asili na 40-70 kwa miti ya kisasa.

Miti ya asili inachukua nafasi kubwa na mti wake huwa mkubwa sana tofauti na miti ya kisasa ambayo haiwi mikubwa sana na haidumu sana kabla ya kufa tofauti na miti ya asili ambayo huweza kufikisha zaidi ya miaka 100 ikitunzwa na kuhudumiwa vizuri.

Uvunaji wa korosho huchukua miaka mitatu kwa uchache ila mavuno huwa mengi kuanzia mwaka wa saba na kuendelea kutegemea aina ya mbegu, matunzo, hali ya hewa au ubebeshwaji wa mikorosho.

Unaweza jifunza kwa vitendo kwa kutembelea Mkoa wa Mtwara ambao unaongoza kwa kilimo cha korosho hususani pale chuo cha kilimo Tali Naliendele ambacho kiko kama 12km kutoka Mtwara mjini au baadhi ya maeneo yanayozalisha sana yapatikanayo wilaya za Tandahimba vijiji vyote, Newala vijijini, Masasi (hususani Tarafa ya Mchauru) na Lindi wilaya ya Nachingwea.

Ni hayo tu kwa uchache
 
Nimekuelewa vizuri sana ndugu vipi kwenye biashara ya kununua na kuuza kipindi Cha mnada ipo vizuri kwenye upande wa faida?
 
Vipi kwa wilaya ya liwale pia mkorosho mmoja kwa wastani unatoa kilo ngapi?
 
Inategemea ukubwa wa mkorosho, umri, matunzo na hali ya hewa.

Kwa mkorosho mkubwa wa miaka 10+ kama hizo factors nilizozitaja hapo juu ziko vizuri, unapata kuanzia 20kg hadi zaidi ya 100kg endapo una miaka 25+

Ila kama factors za hapo juu haziko sawa, kwa mkorosho mmoja wa 10+ years hata kilo moja unaweza usivune.
 
A

Aseeeee Bora ufuta
 
Mm nataka kujua napataje mbegu hz zipo madukani
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ni hivi ikifika mwezi wa 9 nunua korosho ghafi halafu uandae kitalu upande kwenye mifuko ya kuoteshea mbegu....halafu uwe unamwagia maji mpaka iote halafu mwezi wa 1 unahamishia shambani...halafu unasubiri miezi kama 5 ndipo unatafuta kuliko na mikorosho bora unaenda kukata matawi kwa ajili ya kubebesha
 
Back
Top Bottom