Naomba msaada: Nahitaji frame Kariakoo, mtaa wa kuuza pochi za kike

Naomba msaada: Nahitaji frame Kariakoo, mtaa wa kuuza pochi za kike

Entim

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
4,025
Reaction score
2,261
Wakuu, nawasalimu kwa jina la JMT.
Nimeingia Dar, takribani miezi 3 iliopita nikitokea Mtwara baada ya kufunga biashara yangu Mtwara MC
Uchumi umeshuka kwa kasi na ninaelekea kupoteza mtaji, hadi natamani kujinyonga.
Nimejaribu biashara mtandaoni nimeishia kuchata na watu, eg mtu anauliza bei wakati bei ipo, mtu anakuja inbox anataka kuona mzigo, yupo Bukoba, km 3,000.

Ninaomba msaada ni wapi naweza kupata fremu Kariakoo, preferably mtaa wa Mchikichi na Swahili.
Biashara yangu kubwa, au nilioiozea ni kuuza women hand bags ( WHBs), yaani mikopa ya akina mama. Wholesale and retail sales.
Nawasilisha
 
Umejipanga kwa hilo mkuu? Pesa ipo ya kutosha? Kama pesa ipo tokea eneo la tukio ila hakikisha una mwenyeji mbobevu wa k/koo usijeukalizwa.
 
Umejipanga kwa hilo mkuu? Pesa ipo ya kutosha? Kama pesa ipo tokea eneo la tukio ila hakikisha una mwenyeji mbobevu wa k/koo usijeukalizwa.
Asante angalau nimempata mwenyeji ila ingependeza kutriangulate anachoniambia ili nisijepoteza mtaji wangu bure. eg. Ameshauri niende Mtaa wa Mchikichi na Swahili ila nilipotembelea jana, nilikuta kuna duka moja tu la kuuza Pochi, I was not impressed!
 
Kwa ushauri wangu anza na stoo ukiwa unasoma mazingira, chukua mzigo wa jumla mkali lipia store na uanze kuuzia ukiwa stoo. Tafuta soko kwa wanaopanga mezani nnaamini ukiwa na mali nzuri utauza tu kikubwa bei iwe cheap.

NB: hapo kwenye kutafuta soko hakikisha unae mtu anaeifaham kariakoo vizuri kwenye upande wa pochi. Kila la heri mkuu.
 
Back
Top Bottom