Naomba msaada nakosea wapi kwenye kuconnect hii form na database

Aisee mimi nashida sama kwenye mysql yani niliinstall mysql ila hairun kabisaa inasema No server detected wakuu msaada...tofaut na Mysql naweza tumia nini kama mbadala
 
Post picha ya browser nzima pamoja na url address bar kuanzia site ya kwanza ya registration, nadhani unakosea kutumia server yako, nikiangalia picha ya mwisho yenye screen nyeusi ya PHP naona url inasoma file la PHP kutoka kwenye file system yaani C:/..... unapotumia webserver browser yako inabidi iende kwenye address ya hiyo server na sio kufungua file directly kupitia file system so kwa local server url itakua mfumo wa localhost:8080/My-Projects au similar.

Kama unatumia server kiusahihi kamwe hauwezi kuona php code maana ni security risk kubwa kama hapo credentials zako zote zinasomeka.
 
Ingia hapa:

 
Mkuu naomba unieleweshe zaidi maana hapa sijaelewa.
Folder la project liko kwenye htdocs.
Hapa kuna screnshots
hii ni code ya kupost:
<form action="sign-in.php" method="post">
Hapa url screenshot ya page form

hapa screenshot nayopata nikisubmit hii form
 
Jinsi unavyofungua file zako sio sahihi, unafungua kupitia file system badala ya kupitia server, nadhani utakuwa una double click au unabdrag drop, hii sio sahihi, kwa vile php ni backend/server side inabidi iwe processed na server kisha server itume majibu kwenye browser kupitia http wewe unafungua mafile directly kupitia file system so haujaihusisha server kabisa ni kama hauna xampp, kumbuka browser haielewi php browser inaelewa html,css, na js tu so ndo maana php code yako inaonekana tu kwenyen screen kwa sababu browser inafungua kama text file. Njia hii ya kufungua mafile ya html kwenye file system inafanya kazi kwa kiasi fulani kwa site simple za frontend tu (html/css/js).

So fanya ifuatavyo, run XAMPP hakikisha Apache na MySql zinarun, bonyeza btn ya Admin pembeni ya Apache itafungua browser katika site kama localhost/dashboard (localhost ni computer yako kwa vile server ya apache ipo kwenye computer yako) hii dashboard ipo ndani ya htdocs folder so apache inaenda ndani ya htdocs inasoma yaliyomo ndani ya dashboard folder kama kuna php inapitia php processing kisha inarudisha html kwenye browser.

So kwa vile site yako iko ndani ya htdocs/My-Projects andika localhost/My-Projects katika browser address bar yako, apache itaenda ndani ya hiyo folder na kutafuta file kama index.html au index.php na itaiprocess na kurudisha page kama inavyotakiwa.

Pia ningekushauri usitumie -, space, na kuchanganya herufi kubwa na ndogo kwenye folder na file zako so folder myprojects ni bora zaidi.
 
Mkuu yani nashukuru sana sana. Kosa langu lilikuwa hivyo nilikuwa na access file directly kw kulibofya. Nashukuru sasa hivi ina signup kabisa na kuandika kwenye database kabisa.
Asante sana mkuu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…