macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Da umefanya siku yangu iishe vizuri sana. Mungu ni mkubwa. Japo sikujui lakini huwa nikisia binadamu mwenzangu anakumbwa na tatizo kama ulilokuwa umeambiwa unalo huwa najisikia vibaya mno. Ila kweli Bongo nyoso. N nini kilikuwa kimetokea mwanzoni? Sitaki kumlaumu sana huyo dr kwani hata vipimo vya maabara Bongo wakati mwingine huwa fyongo.Mrejesho. Nilipost humu kuomba ushauri kuhusu hali yangu ya afya baada ya kuambiwa ini langu lina shida. OK ilibidi nirudi Amana na kuomba rufaa ya kwenda Muhimbili kuona na Dr bingwa wa ini. Baada ya kufika Muhimbili nilifanyiwa vipimo vyote muhimu vya awali vya utambuzi wa tatizo kwenye ini, kongosho, nyongo na figo. Pia nilifanya Utrasound ya tumbo na Endoscopy. Vipimo vyote havikuonesha dalili ya uharibifu ktk ini na viungo vingine vya ndani, hivyo Dr akiishia hapo kuwa ini halina shida hivyo hakuna haja ya kuagiza vipimo zaidi. Kuhusu maumivu ya tumbo upande wa juu kulia chini ya mbavu Dr alisema huenda ni sababu ya vidonda vya tumbo ambavyo viligundulika kwenye kipimo cha Endoscopy. Hivyo zoezi la uchunguzi kuhusu ini na viungo vingine vya ndani liliishia hapo na ugonjwa pekee uliotambuliwa ni ulcers ambapo nilipewa dozi ya wiki 6. Ahsanteni kwa ushauri wenu na pole mlizonipa.