Naomba msaada wa kiasi chochote cha fedha niweze kujikimu kwa muda nitafutao ajira

natamani kupata mtaji wa kujiajiri lakini imekuwa shida sana kwa hivi sasa,ndio maana naomba pale ninapokwama,japo nami sio kuwa niwakukaa tu,huwa najitahidi
 
Pole sana ungeomba hata kusaidiwa hela ya kabiashara hata kutembeza matunda au biashara yoyote ndogo Mungu akusaidie hitaji lako utasaidiwa leo ya kula kesho ukiamka unatakiwa hela nyingine ya kujikimu
Kweli dada ila nihali tu imenitokea,sipendezwi na hii hali ila ni kheri kudhalilika kwa muda kuliko kufa njaa,inaumiza sana
 
Rais alisema kufika mwezi wa 6 2017 bado upo mjini bac ww mwanaume. Umengangania mjini mpaka sasa unajifanya kidume. Wenzio tupo vjijini huku tunalima bamia na mvua imetubust kwelikweli. Mi nimekuonea huruma ila naona kma hujajionea huruma mwenyewe.
Kaka nipo mbeya dar niliondoka toka mwezi wa Tisa
 
Kuaminiana kweli ni kazi ila kama una ndugu yako hapa mbeya naweza meet nae kuthibitisha kweli Nina changamoto kama binadamu wengine wanaopitia magumu
Nimejikuta nakurumia ghafla binti, bahati mbaya sana Mbeya sina ndugu hakika
 
Hapa kuna watu wengi sana watapigwa na kulizwa...


Cc: @mahodaw
Sawa ndugu,yote ni maoni lakini Mimi sioni haja ya kusemwa vibaya Wakati maelezo yangu Hapo wazi kwa kila utakalopenda kulijua au hata kuonana nami
 
natamani kupata mtaji wa kujiajiri lakini imekuwa shida sana kwa hivi sasa,ndio maana naomba pale ninapokwama,japo nami sio kuwa niwakukaa tu,huwa najitahidi
Vizuri, lakini ukiwa unaomba pesa moja kwa moja tena pesa ya kula...hapo kuna wengine watakufananisha na wale watu wa dodoma
 
umri?
taaluma?
unasubiri utakapoajiriwa, ajira gani hiyo??
Unajishughulisha na nini kwa sasa kujipatia kipato?
vipi unaweza kumudi gharama za bando kuingia jf au kuna mtu anakudhamini?
 
Ndugu omba mtaji au kazi ya kufanya sio kuomba hela ya kula
Nadhani Hapo ndio nilikosea kwa kutoamini naweza saidiwa mtaji ila kwa kuamini naweza saidiwa kidogo mtu alicho nacho kwa kusogeza maisha
 
umri?
taaluma?
unasubiri utakapoajiriwa, ajira gani hiyo??
Unajishughulisha na nini kwa sasa kujipatia kipato?
vipi unaweza kumudi gharama za bando kuingia jf au kuna mtu anakudhamini?
26
Beauty services
Now ninasimamia boutique(japo ni closed kwa muda)

Naweza kuunga kifurushi cha mia tano,na mb,sababu huwa Si download zaidi ya kuchat hivyo kina mudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…