Naomba msaada wa kiasi chochote cha fedha niweze kujikimu kwa muda nitafutao ajira

ndugu zangu wana JF mtu anapoomba msaada kama huna kitu cha kumpa au kumsauli ni vyema ukakaa kimya kabisa kuliko kumkejeri na kumtusi matusi ya rejareja.
hakuna aliyeingia mkataba na Mungu awe na maisha mazuri mpaka anakufa ugumu wa maisha hutokea kwa yeyote ikiwa wewe Mungu kakuwezesha kuwa na maisha mazuri shukuru lakin siyo kuona wasionacho hawana akili wewe unaakili sana.
kwa wale ambao wamepitia ugumu wa maisha na sasa Mungu amewasaidia wanamaisha mazuri nadhani wanajua, hakuna anayeomba awe na maisha magumu.

Huna msaada kaa kimya.
 
Kweli nataka moyo Dada,ila nadhani kuna kazi zingine zinazoendana na hizo ambazo hazikufanyi thamani yako ishuke,kama kutengenezea nyumbani chakula au vitafunwa na kudeliver maofisini
Yap fanya hivyo
 
Ahsante kaka Paul, nimegundua kila mtu huchukulia matatizo ya mwingine kwa namna yake lakini,busara tu au ushauri unaweza kunijenga
 
 
Kwanini usiombe kupatiwa Ajira kama kuna mtu ana uhitaji kutona na kazi unayo itaka..hali ya sahizi hata niki kupa milion 2 bado nakuwa sijakusaidia..

Zaidi ni wewe kujaza madeni mwosho wa siku maisha yako yatazidi kuwa magumu
 
Maswali yananijenga pia,sijfikiria kujihusisha n mahusiano kwa hivi karibu ni,kwani natamani kujiinua kwanza walau niwe na shughuli yangu itakayokidhi nahitaji japo najua umri unaenda
sawa, kama una bank account si mbaya ukatuandikia hapa.
 
Ahsante kaka Paul, nimegundua kila mtu huchukulia matatizo ya mwingine kwa namna yake lakini,busara tu au ushauri unaweza kunijenga
Kuna mkaka mmoja nilimpenda sana yeye yupo Tabora alianza na mtaji wa sh 8000 anaamka asubuhi anaenda machinjioni ananunua kichwa cha ng'ombe kimoja anawapa watu wanamchalangia kwa sh 500 then anazipanga zile nyama kwenye mafungu ya bei ya 2000 na mafungu ya bei ya 1000 anaingia mtaani nyumba kwa nyumba anasema kichwa kimoja cha sh 8000 kinampa faida ya sh 6000 kwa siku wakati mwingine mpaka saa saba mzigo unakuwa umeisha saiz ananunua vichwa viwili kwahiyo faida yake kwa siku ni 11,000.
kwa haraka haraka unaweza ona ni kazi ya mtu asiye na hadthi hebu piga hesabu kwa mwezi anashilingi ngapi, kama ni kodi ya chumba, umeme na maji tayari anailipa.
 
Ahsante kaka Paul,hakika yeye ni Mwingi wa rehema..
Kwahiyo dada kama ni biashara si lazima utafute mtaji wa malaki kadhaa hata mtaji mdogo anza nao taratibu simamia vizuri mradi wako taratibu utakuza mtaji halafu utaenda kwenye mtaji mkubwa.
kuanza na mtaji mdogo pia inakusaidia kuwa na uchungu wa mali yako na kuitunza vizuri.
 
Naamini katika kuinuka toka chini kaka hivyo sibagui wapi pa kuanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…