Za leo ndugu zangu,
Naitwa Thandiwe, ni mkazi wa Dar lakini kwa sasa nipo mkoani. Kiukweli hali ya maisha imekuwa ngumu hatukatai ndugu zangu hasa sisi tuliopo mikoani kwa sasa ila kiukweli, kuna wengine tunashindwa jihusisha na mambo yasiyo na maadili ili kujipatia kipato, kwani ninaamini kheri kuomba msaada unapokwama kuliko kujificha na kufa na njaa.
Ombi langu kwenu wenzangu, msaada wa kiasi chochote cha pesa ili kusukuma siku wakati nikiendelea kufuatilia ajira. Kwa yeyote atakaeguswa nipo tayari kuweka mawasiliano yangu PM ili kujieleza zaidi.
Mungu awabariki wote watafutaji.