Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Unatokwa na povu kana kwamba mtoa mada ndiye kiumbe pekee mwenye shida hapa nchini! Si umsaidie?Unajuwa kuna mjinga na mpumbavu, ni heri ya mjinga ukimuelimisha anaelewa, ila mpumbavu ni kipaji huwezi kumbadilisha.
Walioweka bodi ya mikopo kwenye vyuo vya elimu ya juu si wajinga, watoto wanapofika stage hiyo familia nyingi za kibongo wazazi wanakuwa wameshaishiwa nguvu za kiuchumi ila kuna wachache sana wanakuwa na uwezo wa kusomesha watoto zao hata Ulaya kwa cash.
Sasa malengo ya bodi ilikuwa ni kusaidia wazazi wasife kabla ya muda wao kwa mizigo ya familia, mzazi anateseka tangu mimba mpaka mtoto anafikisha miaka 21.
Imagine labda una watoto watatu tu kwa miaka 21 uwe unawahudumia wewe ukijumlisha na umri uliokuwa nao wakati wanazaliwa tayari unaanza clinic za kisukari kama umesalimika na stroke, hapo hujamuweka mama yao ambaye ndio mtambo wa kuzalisha stroke na magonjwa yasiyoambukiza.
Kwakweli mimi siamini kama kuna motoni tena, tumeshaunguwa hapa hapa duniani, labda motoni wametengewa wazungu.
Maneno mengi ya kejeli ya nini sasa! Ujuaji mwingi, kumbe bongotole tu.