Naomba msaada wa kifedha nilipie pango. Mwenye nyumba kaja kutoa vitu

Naomba msaada wa kifedha nilipie pango. Mwenye nyumba kaja kutoa vitu

Mwenye nyumba kaja kutoa vitu vyako,anakudai 250k na mfukoni una 150k,fanya kitu kimoja Chukua vitu vyako kaviweke kwa rafiki yako,hiyo 150k usimpe mwenye nyumba jifanye umekosa hata mia.
Nenda katafute chumba kingine cha 30k lipia miezi minne 120k, 30k bakiza ya dharula maisha yanaendeleaa.
 
Huo ndiyo uhalisia mimi wazazi wangu walikuwa na nafasi wakawa wanaishi maisha ya mboga saba nimesoma kwa vibarua hadi chuo kikuu hata mahari ya kuoa nilitoa mwenyewe kwa sasa nawaangalia tu siyo jukumu langu kuwalea wadogo zangu na wao,misaada yangu naelekeza kwa maskini na wanangu,wamesema maneno mabaya dhidi yangu lakini Mungu ananisimamia kwani sina deni nao!!

Apambane
Maneno mabaya dhidi yako? Walikuwa mboga saba ila ulijisomesha kwa vibarua ina maana walikutelekeza au wewe ulikuwa mtukutu na hukuwa na adabu?

Ni ngumu sana kwa mzazi mwenye nafasi kufanya hayo kwa mwanaye!

Kuna kitu umetuficha hapo, ushauri wangu ni kuwa jaribu kuweka kila kitu wazi, haiingii akilini kabisa.
 
Nawashauri mlipe kodi direct kwa mwenye nyumba.

Dogo anashindwa jukwaa la kamari toka mwaka 2019...
Screenshot_20220501-203530.png
Screenshot_20220501-203412.png
Screenshot_20220501-203328.png
 
Screenshot_20220501-204015.png

dogo anabeti sana, dau la chini ni elfu tano😅😅😅

***** mi mcheza kamari siwez mpa hela yangu hivi hivi
Screenshot_20220501-203943.png

mikeka itakuua acha hizi mambo kaa usome😓😓😓
Screenshot_20220501-203849.png

unateketeza elfu 20 hivi hivi wakati unasoma na unadaiwa gharama mbalimbali za maisha
 
Mkipata uwa mnaona waliokosa ni wazembe.
"KUKAUKIWA KUPO"
Hutakiwi kumuonea huruma mzazi wako. Maana hili ni jukumu lake kukusomesha na kukulea mpaka pale utakapo jitegemea!
Wewe muongezee tu mawazo ili akili imkae sawa.

Ifikie wakati tuishi maisha kama ya Wazungu. Haya masuala ya kufyatua tu, halafu watoto wanakuja kuteseka na kusumbua watu wengine hayana tija hata kidogo.

Samahani sana mtoto/mdogo wangu [emoji120] kama nitakukwaza kwa haya maneno yangu.
 
Dodoma nzima hakuna vyumba bei chini ya hapo? Ushauri wangu,Ishi kwa hali uliyonayo Tafuta kwingine hama,kwa sababu we bado unatafuta kubaliana na kila hali ili mradi usome tu.
....tafuta sehemu uhame. Mahalia ambako una kilo Moja unusu lakini mwenye nyumba anaotaka kutolea vyombo Kwa kukosa Kilo, Sio Mahalia pa kuishi.....!
 
Huyu jamaa yupo Chuo ila ndiyo hajitambui that much!

Anataka hela za wanaJF akachanie mikeka.

Uduwanzi mtupu!

-Kaveli-
Screenshot_20220501-205338.png
betting ni addiction mbaya sana.
haina tofauti na madawa ya kulevya.
Screenshot_20220501-205338.png


dogo ubadilike, matumizi yako ya pesa unayaelekeza kubaya sana.

gamble responsibly. Mimi mwenyewe nabeti sana tu lakini sina ujinga wa.kubeti mpaka nikashindwa kulipa kodi wala kuiathiri familia
 
Just like that unaweka namba na unategemea utumiwe pesa!unafikiri sisi ni wajomba zako?kuwa serious jamaa!!
Hiyo pesa unaweza ukapewa na mtu hata balabalani,lakini lazima uonyeshe uaminifu,hapa kwenye mtandao sio njia nzuri,Bora ungejirekodi watu wakuone kama unashida kweli,au kagonge hodi kwenye geti la mtu hapo uzunguni dodoma,
Uzunguni tena!? Hahaaaa... wenyewe tupo hapa capital tunamalizia siku.
 
Kwa hapa issue ilipofikia namshauri kijana achukue laki na nusu aliyonayo akabeti, hadi asubuhi ana mamilioni.
 
View attachment 2207823betting ni addiction mbaya sana.
haina tofauti na madawa ya kulevya.
View attachment 2207823

dogo ubadilike, matumizi yako ya pesa unayaelekeza kubaya sana.

gamble responsibly. Mimi mwenyewe nabeti sana tu lakini sina ujinga wa.kubeti mpaka nikashindwa kulipa kodi wala kuiathiri familia
Baada ya kuona hizi screenshots zinazomuhusu, nimegundua kijana kashakuwa addicted na kubet, itamchukua muda kupunguza au kuacha kabisa.

Na kwa sababu hii inaonekana watu wake wa karibu wameshaijua tabia yake na wamechoka kumsaidia pindi anapokwama.

Huenda anakwama kweli ila kubet kunamfanya aonekane anamalizia pesa huko.
 
Back
Top Bottom