Naomba msaada wa kifedha nilipie pango. Mwenye nyumba kaja kutoa vitu

Mwenye nyumba kaja kutoa vitu vyako,anakudai 250k na mfukoni una 150k,fanya kitu kimoja Chukua vitu vyako kaviweke kwa rafiki yako,hiyo 150k usimpe mwenye nyumba jifanye umekosa hata mia.
Nenda katafute chumba kingine cha 30k lipia miezi minne 120k, 30k bakiza ya dharula maisha yanaendeleaa.
 
Maneno mabaya dhidi yako? Walikuwa mboga saba ila ulijisomesha kwa vibarua ina maana walikutelekeza au wewe ulikuwa mtukutu na hukuwa na adabu?

Ni ngumu sana kwa mzazi mwenye nafasi kufanya hayo kwa mwanaye!

Kuna kitu umetuficha hapo, ushauri wangu ni kuwa jaribu kuweka kila kitu wazi, haiingii akilini kabisa.
 
Nawashauri mlipe kodi direct kwa mwenye nyumba.

Dogo anashindwa jukwaa la kamari toka mwaka 2019...
 

dogo anabeti sana, dau la chini ni elfu tano😅😅😅

***** mi mcheza kamari siwez mpa hela yangu hivi hivi

mikeka itakuua acha hizi mambo kaa usome😓😓😓

unateketeza elfu 20 hivi hivi wakati unasoma na unadaiwa gharama mbalimbali za maisha
 
Mkipata uwa mnaona waliokosa ni wazembe.
"KUKAUKIWA KUPO"
 
Dodoma nzima hakuna vyumba bei chini ya hapo? Ushauri wangu,Ishi kwa hali uliyonayo Tafuta kwingine hama,kwa sababu we bado unatafuta kubaliana na kila hali ili mradi usome tu.
....tafuta sehemu uhame. Mahalia ambako una kilo Moja unusu lakini mwenye nyumba anaotaka kutolea vyombo Kwa kukosa Kilo, Sio Mahalia pa kuishi.....!
 
Huyu jamaa yupo Chuo ila ndiyo hajitambui that much!

Anataka hela za wanaJF akachanie mikeka.

Uduwanzi mtupu!

-Kaveli-
betting ni addiction mbaya sana.
haina tofauti na madawa ya kulevya.


dogo ubadilike, matumizi yako ya pesa unayaelekeza kubaya sana.

gamble responsibly. Mimi mwenyewe nabeti sana tu lakini sina ujinga wa.kubeti mpaka nikashindwa kulipa kodi wala kuiathiri familia
 
Uzunguni tena!? Hahaaaa... wenyewe tupo hapa capital tunamalizia siku.
 
Kwa hapa issue ilipofikia namshauri kijana achukue laki na nusu aliyonayo akabeti, hadi asubuhi ana mamilioni.
 
Baada ya kuona hizi screenshots zinazomuhusu, nimegundua kijana kashakuwa addicted na kubet, itamchukua muda kupunguza au kuacha kabisa.

Na kwa sababu hii inaonekana watu wake wa karibu wameshaijua tabia yake na wamechoka kumsaidia pindi anapokwama.

Huenda anakwama kweli ila kubet kunamfanya aonekane anamalizia pesa huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…