Naomba Msaada wa kisheria kuhusu hili la ndoa ya mkeka

Naomba Msaada wa kisheria kuhusu hili la ndoa ya mkeka

Kijana bado anakula kwa baba hivo mzigo utakuwa wa mzee na binti anajulikana ni kicheche mtaani. Hofu ni kifungo naomba msaada wa kisheria kutoka mwanasheria
Binti ameona hali ya kwao kijana kuna nafuu ya maisha na haikuwa plan ya siku moja. Zile genye za teen age zina mgharimu
 
Tumeona twende nayo mbele kuoa hapana kwa kweli binti ni kicheche. Aliwekwa ndani tumemtoa walioshtaki wameomba kesi itoke kituo kidogo ieleekee kituo kikubwa cha polisi. Jumatatu nafikiri kutakua na kikao dawati la jinsia pande mbili hakuna muafaka basi itakwenda mahakamani.

Mashtaka yao yanasomeka: kosa la kumzorotesha mwanafunzi masomo kwa kumpa mimba. Wanadai imempelekea kufeli na kuramba zero.
Hamko serious,huyo dogo atakula mvua 30,kubalini aoe,atachomokea juu kwa juu.
 
Hamko serious,huyo dogo atakula mvua 30,kubalini aoe,atachomokea juu kwa juu.
Sorry mimba sio yake, naomba unipe mwongozo wa kisheria binti akisema tu kama huyu ndo alonipa mimba mahakamani inatosha hiyo kuwa ushahidi tosha au kutahitajika ushahidi mwengine?
 
Wamekupa suluhisho jepesi wadau kwamba jifanye mjinga maisha yaendelee kwa kukubali ndoa kisha dogo hata anasafiri anamtelekeza hapo anaenda kusaka maisha, siku zikisonga anajifungua mtoto anatoka sio copy (kama kweli hajampa hiyo mimba) anamlima talaka mchezo umeisha dogo anaoa yule amtakaye.
Ila ww inaonekana unaleta kaubabe ka kutaka kesi, wakikaa vizuri hao unaowadharau dogo anakula mvua 30 kiulani tu na nyie mliokuwa mnataka kesi mnaanza kulaumiana na kurudi kuomba upande mwingine msamaha muyamalize na inakuwa too late.


Umekaa unasema tu huyo binti kicheche kicheche,


Shauri yako,
Kuna dogo alizingua ka issue za kiujana kiutani utani hivi tukachukulia masihara na dharau kama zako hivi,

Gues what?

Alikula mvua 30 na baada ya hapo zikatakiwa hela mingi sana kila mtu akaona ni mzigo basi watu full kuzimiana simu.

Anaendelea na mvua yke
fuata ushauri wa jamaa hapo juu
baada ya yote mahakamani
ikiongozwa na wakili wa serikali ROBERT KIDANDO

eenhe binti tueleze ilikuaje
si unajua maswali ya robart kidando na abdallah chavula akitaja tu aliyenipa miba ni yule pale KUSHNEY

yaan hapo labda aje peter kibatala na colum yake akiwa na bwana malya nashon nkungu kwenye cross examination
ndio kiboko ya kina kidando na chavula

mkuu hiyo kesi kuwa mpole na usikubali ifike kituo kikubwa itawatoka ela nyingi sana na mimba mtalea

kubalini kutoa huduma msubiri mtoto azaliwe bado miezi 5 tu si mingi
 
Sorry mimba sio yake, naomba unipe mwongozo wa kisheria binti akisema tu kama huyu ndo alonipa mimba mahakamani inatosha hiyo kuwa ushahidi tosha au kutahitajika ushahidi mwengine?
ndio na akisema huyu simjui si yeye na kesi inaisha hapo

sister angu alimkana mzee mahakamani
akamtetea bwana ake akasema huyu mimi simjui
akaulizwa mimba alikupa nani akajibu nilibakwa ila niliogopa kusema 7bu niliona aibu

kesi ikaisha hapohapo
sasa hivi wana watoto watatu washaoana na maisha yanaenda

usishindane na mwanamke akiamua
 
Kausha tu wakija Tena kwako fukuzia mbali wambie mpaka ajifungue full stop.
 
Ushauri: Kama unaona usumbufu kupambana na hiyo kesi kubali ndoa then baada ya wiki tu unampa talaka tatu mchezo umeisha ila jiandae kurogwa
Daaaah mwamba umetisha.......

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kesi za mimba mabinti wanasikilizwa sana mahakama.

Binti akipoint tu kama aliyonipa mimba ni yule pale. Ujue unakula mvua miaka 30 kama utani

Hata ujitetee vipi mahakama itakuuliza swali simple tu je hujawai kutembea nae hata mara 1. Sasa ole wake jibu lako liseme nilitembea nae zamani sana ama nilivaa kinga siku hiyo
 
Habari wakuu, kuna binti anadai kijana wetu amempa mimba. Hivyo wamekuja wazazi wa binti kudai ndoa ya mkeka, kinyume na hapo wanatishia kumfunga kijana wetu kwani binti kamaliza form four mwaka jana. Mimba ina miezi 4/5 hivo iliingia wakati akiwa mwanafunzi ingawa kwa sasa amemaliza.

Kijana anakataa sio yake kwani ana muda mrefu hajawasiliana naye na binti mtaani ana mabwana wengi.

Sasa sisi tumesema mpaka ajifungue tupime DNA tutahudumi. Wao wanaendelea kutishia kumfunga.

Je, kisheria wana kipengele cha kumfunga hapo?

Asante
Hapo pana makosa mawili na yanajitegemea. Sijajua umri wa huyo binti, kama ni under 18, basi ni ubakaji, kama kazidi kosa linakuwa kufanya mapenzi na mwanafunzi.Kosa la pili ni kumpa ujauzito mwanafunzi. Muda unaoangaliwa siyo sasa ila ule muda kosa linapodaiwa kufanyika.
 
Hapo pana makosa mawili na yanajitegemea. Sijajua umri wa huyo binti, kama ni under 18, basi ni ubakaji, kama kazidi kosa linakuwa kufanya mapenzi na mwanafunzi.Kosa la pili ni kumpa ujauzito mwanafunzi. Muda unaoangaliwa siyo sasa ila ule muda kosa linapodaiwa kufanyika.
Asante je ni ushahidi gani utakaotumika kumtia hatiani?
 
Watu waongo!

Eti Binti akiku-point tu kuwa huyu ndie alinipa mimba, hapo hapo unahukumiwa miaka 30?

Ya wapi hiyo nyie?

Je kama anambambikizia mtu?

Lazima ushahidi uwepo bana.

Hassani
FRESHMAN
permanides
Mzimu wa Kolelo
Kasome SOSPA 1998,makosa mengi sana yanayohusisha unyanyasaji wa kingono,ikiwa pamoja na ubakaji huwa hayahitaji shahidi wa tatu.Maelezo na vielelezo sahihi tu ya mbakwaji yanatosha kukunyoosha.
 
Watu waongo!

Eti Binti akiku-point tu kuwa huyu ndie alinipa mimba, hapo hapo unahukumiwa miaka 30?

Ya wapi hiyo nyie?

Je kama anambambikizia mtu?

Lazima ushahidi uwepo bana.

Hassani
FRESHMAN
permanides
Mzimu wa Kolelo
Alafu kinachokufunga sio kumpa mimba bali ni kusex nae akiwa under 18,so mara zote mwanamke hukutaja umempa mimba kama ulishawahi sex nae.
 
Ikiwa binti hajafikisha miaka 18 unayo kesi ya kujibu , mbaya zaid dogo amekubali kama alikuwa na mahusiano nae huo utakuwa ushahidi tosha lkn pia bint akisema tulikuwa tunakutania wapi na akenda kuonyesha na pia mazingila yakaendana na maelezo yake , kuhusu binti kuwa kicheche sio mada kwa sababu atambiwa akawalete hao wengine ambao anasema ana uhusiano na binti mwambieni awe makini jela nje nje hapo
 
Ikiwa binti hajafikisha miaka 18 unayo kesi ya kujibu , mbaya zaid dogo amekubali kama alikuwa na mahusiano nae huo utakuwa ushahidi tosha lkn pia bint akisema tulikuwa tunakutania wapi na akenda kuonyesha na pia mazingila yakaendana na maelezo yake , kuhusu binti kuwa kicheche sio mada kwa sababu atambiwa akawalete hao wengine ambao anasema ana uhusiano na binti mwambieni awe makini jela nje nje hapo
Aisee umegonga mule mule, binti ameshafikisha 18. Dogo hajakubali kama alikua na uhusiano naye. İla hiyo pointi ya kuonesha walipokua wanakutania katika upelelezi ilikuepo na binti akaenda kuonesha japo hakua anajiamini sasa hatujui kama ndio mazingira yanaendana na maelezo yake. Dah kinachouma ujue msela aliyekua ana date nae mpaka dakika za mwisho anapata ujauzito anajulikana mtaani ila binti ndio hajamtaja anataka ndoa na dogo huyu.
 
Hivi aliyeshtaki akiamua kufuta kesi kuna kizuizi chochote eti kwasababu faili limeshafunguliwa?
 
Wameamuaje... Wametoa kesi mahakamani? Mmkubali kutoa mahari?
Baada ya kupelekeshana sana na nenda rudi za polisi, ilipofika hatua ya kwenda mahakamani tulikaa tena kikao cha wazee wa pande mbili na hekima kubwa kupita maamuzi yakawa kwa hatua iliyofikia ya mpaka familia hizi kupelekana polisi kusimama ndoa itakua ni ngumu na haiwezekani tena hivo maamuzi ni kuihudumia mimba mpaka na mtoto ila sio ndoa.

Hivo wamekubali kufuta kesi tuhudumie tumeenda kufuta kesi ila wajomba wanaweka password ndio nikauliza kwani kufuta kesi kuna vikwazo vyovyote.
 
Back
Top Bottom