Naomba msaada wa kisheria

Naomba msaada wa kisheria

Joined
Apr 30, 2015
Posts
4
Reaction score
0
Naomba kuuliza kuhusu uhalali wa askari hawa kufukuzwa kazi kama ilikuwa sawa kwa maelezo haya;ilikuwa ni siku ya jumamosi askari polisi wawili walipata taarifa kwamba kunamtu mmoja alikuwa na meno ya tembo askari wale walikwenda wao wawili wakamuita muhusika wakamwambia sisi ni askari tunataarifa hizi tunataka kufanya ukaguzi nyumbani kwako mwenyenyumba akakubali lkn hawa kuwa na kiongozi yoyote wa serikali yaani hata mtendaji lkn baada ya ukaguzi wao wakafanikiwa kupata jino moja la tembo wakaondoka na mtuhumiwa mpaka kituoni wakiwa njiani ndugu wa mtuhumiwa walimpigia simu ocd wakamjulisha na walipofika kituoni ocd aliekekeza kesi isifunguliwe mpaka afike alikuwa nje ya kituoni alipofika aliamuru mtuhumiwa apewe dhamana na lilejino la tembo lilifunguliwa taarifa kama mali ya kuokota na waliookota walitajwa wale askari lkn iliandikwa kwamba wameokota karibu na nyumba ya mtuhumiwa.Baada ya siku kadhaa wale askari walishitakiwa kijeshi kwa kosa la kufanya upekuzi bila kuwa na search order na kubambikia jino la tembo.Kumbuka RB yao iliandika kuwa jino hilo ni mali ya kuokota na waliookota ni wale askari.Askari hao walishitakiwa na mashitaka hayo yalisikilizwa na yule ocd na walimkataa kwa kukosa imani nae lkn bado aliendesha mashitaka yao na mwishowe walifukuzwa na hata nakala ya mwenendo wa mashitaka walinyimwa lkn walikata rufaa ambayo mpaka leo hawajajibiwa na IGP.Je kwa mtazamo wa kisheria nini walitakiwa kufanya au je hukumu ilikuwa sahihi?Naomba ufafanuzi au mtazamo wenu wadau.
 
Asakari wana makosa tayari wameenda kinyume na sheria utaendaje kufanya search bila warrant? Sheria hawajui au ni kulewa uaskari gu, wangekuwa na warrant ina maana lazima wangeenda na mkuu wao pia haya yote yasingetokea! Inavyoonekana hiyo biashara mtandao wake ni mkubwa na ocd yupo ndani yake
 
Kukutajia pcd wa wapi bado sio msaada kwangu na uliesema wanamakosa kwa kupekua bila warrant nikuulize kuna aina ngapi za search kama sikosei zipo mbili with warrant and without warrant and without warrant it is an emmergency search it can be conducted even without warrant.Kwahiyo naomba ushauri wenye tija usio wa chuki eti kwavile ni polisi.
 
Pole sana mliingilia deal ya OCD!!! Najua mlisukumwa na njaa zenu ili mpate kitu kidogo toka kwa mtuhumiwa. Pole sana bado kuna mapori kibao, karibu tulime.
 
Pamoja na kuwa maaskari wanamakosa lakini wamekanyaga nyaya za mkuu wao bila kujua ikawagharimu.
 
Wewe polisi gani unashindwa kujua sheria nq mwenendo wa makosa ya jinai

Nenda kasome CPA wewe hata moshi hayo mambo yanafundishwa kwanzo huna maadili mambo ya kazini kuyaleta hapa kwa raia

Bahati nzuri umefukuzwa kazi nyinyi ndio wale wanaochafua jeshi letu usirudi tena hapa jamvini kuja kuleta habari za polisi hapa sawa?
 
Kimsingi nilikuwa naangalia baadhi ya watu uwezo wao wa kufikiri lkn nikaona nitoe kisa cha ainahiyo ambacho hakina ukweli lkn ni mambo ambayo yapo bali nimegundua baadhi ya waliochangia uwezo wa kisheria ni mdogo udhani nilipo uliza mm ni polisi au nimepatwa na mkasa huo lkn unaweza ukakutana na issue kama hiyo ukatakiwa uitatue kama reasoning zenu ni hizo bado sana.
 
Kimsingi nilikuwa naangalia baadhi ya watu uwezo wao wa kufikiri lkn nikaona nitoe kisa cha ainahiyo ambacho hakina ukweli lkn ni mambo ambayo yapo bali nimegundua baadhi ya waliochangia uwezo wa kisheria ni mdogo udhani nilipo uliza mm ni polisi au nimepatwa na mkasa huo lkn unaweza ukakutana na issue kama hiyo ukatakiwa uitatue kama reasoning zenu ni hizo bado sana.

Kweli ee!
 
Usidanganye kuwa ulikuwa unajaribu uwezo wa watu kufikiri wakati wewe mwenyewe umeonyesha uwezo mdogo wa kufikiri,toka lini polisi akafanye search without police inspector? Hapo ungefikiri vizuri ungetudanganya kuwa walienda kumkamata mtuhumiwa akakutwa na exhibit,halafu kitu au exhibit iliyoletwa na askari iweje ifunguliwe kama mali ya kuokota hasa pembe/jino la ndovu? Ungekuwa unajua kufikiria usingendanganya hivyo manake unaweza sana askari anaweza kufungua taarifa ya mali ya kuokota madawa ya kulevya halafu asiwekwe ndani kuwa ni mhusika? Wewe ndo jifunze namna ya uwasilishaji mada kwa hadhiraW usiyoijua,humu tuna wanasheria,polisi,walimu madaktari na kadha wa kadha.
 
Mkuu ulietoa post nikutie moyo kwani yasemwayo n maneno ya wakosaji wasojua maana ya mitandao ya kijamii. Hakika uelewa wa watu kwnye lugha yao kiswahili ni hafifu xn, mwenzetu ameomba msaada wa kisheria nyie mnaleta hisia zenu juu ya polisi lkn tambueni amani mlonayo sasa ni kwa ulinzi wao km jeshi na kiapo chao ni kuwalinda nyie raia. Km kuna misconduct among polisi basi sio wote ni wachache, kwa hivyo ndugu unaejifanya kutoa amri ya kutokuweka post za kipolisi humu una mamlaka gan? hujui kwa nn tunatakiwa kuweka majina bandia humu?
Mtoa post ndugu THINK OUT OF THE BOX nikushukuru kwa scenario ulotupa jamvini na ni ukweli usiopingika kwmba kuna kosa kwa either of the parties. Nipende kuuliza hao askari walikuwa na cheo gani? then ni wakati gani walifanya hyo search? na pia ni sheria gani ya kijeshi imetumika katika kuwafungulia mashtaka hao polisi? ningependa kufahamu hayo machache pamoja na wasomi wanaojielewa ili tulichanganue suala hili.

Mlinzi wa Taifa
 
Asante ndg Soli ya kiatu kwa kuliona hilo ufafanuzi ni kwamba muda ulikuwa asubuhi majira ya saa moja,vyeo vyao ni makonstable na sheria walizotumia ni PGO NA PFSR(POLICE FORCE SERVICE REGULATION OF 1995).
 
ahah kama ni askar aacha tuwe wote huku mtaa na wenyewe waone joto la kauli ya apigwe tu na utapigwa tu.
 
Back
Top Bottom