THINK OUT OF THE BOX
New Member
- Apr 30, 2015
- 4
- 0
Naomba kuuliza kuhusu uhalali wa askari hawa kufukuzwa kazi kama ilikuwa sawa kwa maelezo haya;ilikuwa ni siku ya jumamosi askari polisi wawili walipata taarifa kwamba kunamtu mmoja alikuwa na meno ya tembo askari wale walikwenda wao wawili wakamuita muhusika wakamwambia sisi ni askari tunataarifa hizi tunataka kufanya ukaguzi nyumbani kwako mwenyenyumba akakubali lkn hawa kuwa na kiongozi yoyote wa serikali yaani hata mtendaji lkn baada ya ukaguzi wao wakafanikiwa kupata jino moja la tembo wakaondoka na mtuhumiwa mpaka kituoni wakiwa njiani ndugu wa mtuhumiwa walimpigia simu ocd wakamjulisha na walipofika kituoni ocd aliekekeza kesi isifunguliwe mpaka afike alikuwa nje ya kituoni alipofika aliamuru mtuhumiwa apewe dhamana na lilejino la tembo lilifunguliwa taarifa kama mali ya kuokota na waliookota walitajwa wale askari lkn iliandikwa kwamba wameokota karibu na nyumba ya mtuhumiwa.Baada ya siku kadhaa wale askari walishitakiwa kijeshi kwa kosa la kufanya upekuzi bila kuwa na search order na kubambikia jino la tembo.Kumbuka RB yao iliandika kuwa jino hilo ni mali ya kuokota na waliookota ni wale askari.Askari hao walishitakiwa na mashitaka hayo yalisikilizwa na yule ocd na walimkataa kwa kukosa imani nae lkn bado aliendesha mashitaka yao na mwishowe walifukuzwa na hata nakala ya mwenendo wa mashitaka walinyimwa lkn walikata rufaa ambayo mpaka leo hawajajibiwa na IGP.Je kwa mtazamo wa kisheria nini walitakiwa kufanya au je hukumu ilikuwa sahihi?Naomba ufafanuzi au mtazamo wenu wadau.