Naomba msaada wa kitabibu juu ya huu ugojwa

Ndugu yangu

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
676
Reaction score
359
Wana Jf habari za jumapili?

Kwanza kabisa naanza kwa kutoa pongezi kwa Jamiiforum Doctors kwa kazi nzuri za ushauri na msaada wa kitalaam mnaoutoa kwenye hili jukwaa.

Mimi nina sumbuliwa na ugonjwa ambao nashindwa kuuelewa unasababishwa na nini, nina mafua yaliyoganda ndani ya koo la hewa nikipenga huwa hayatoki hadi nizibe tundu moja la pua huku nikivuta pumzi kwa ndani, nikishavuta yanashuka juu ya taya na kuyatema.

Nina mda mrefu sasa, nilishawahi kutumia dawa za hosipitali aina ya centirizine dihydrochoride hali ikawa nzuri, lakini nilipo maliza dozi baada ya mda wa miezi kama miwili hali ilirudi tena.

Kwa anayejua tiba ya ugonjwa huu naomba msaada. Natanguliza shukrani zangu kwenu nyote. Akhsanteni
Mungu awabariki
 
Dawa ya Mafuwa yaliyoganda. Chukuwa Mafuta ya Zaituni (Olive Oil Virgin) Fresh Tia Kidogo Katika Puwa Pakapaka Ndani Ya Puwa Yako Kabla Ya Kulala. fanya hivyo kila siku kisha uje hapa unipe Feedback.Mkuu@Ndugu yangu
attachment.php
 
Attachments

  • olive-oil__oPt.jpg
    olive-oil__oPt.jpg
    32 KB · Views: 668
Dawa ya Mafuwa yaliyoganda. Chukuwa Mafuta ya Zaituni (Olive Oil Virgin) Fresh Tia Kidogo Katika Puwa Pakapaka Ndani Ya Puwa Yako Kabla Ya Kulala. fanya hivyo kila siku kisha uje hapa unipe Feedback.Mkuu@Ndugu yangu
attachment.php

Asante kaka Mzizimkavu, nitafanyia kazi
 
Dawa ya Mafuwa yaliyoganda. Chukuwa Mafuta ya Zaituni (Olive Oil Virgin) Fresh Tia Kidogo Katika Puwa Pakapaka Ndani Ya Puwa Yako Kabla Ya Kulala. fanya hivyo kila siku kisha uje hapa unipe Feedback.Mkuu@Ndugu yangu
attachment.php

Kaka Mzizimkavu, nimetembea hapa mtaani kutafuta hii dawa sijabahatika kuiona, niliyoiona ni Fragata olive oil, vip hii haiko tofauti sana na hiyo hapo juu
 
Mkuu haina tofauti ila inatakiwa upate Fragata Olive Oil Extra Virgin au upate Fragata Olive Oil Virgin.
 
Kaka Mzizimkavu hiyo dawa nmeipata na nimeendelea kutumia, ila kuna mabadiliko nayaona yameanza kujitokeza, mfano kichwa kuuma, matezi kuuma na makoozi mengi sana kwenye koo la hewa, wakati mwingine hadi shingo inauma, vip niendelee kutumia hii dawa au waweza nishauri nyingine? Natanguliza shukrani zangu za dhati na Mungu akubariki, Akhsante
 
Endelea na hiyo dawa kwa muda wa siku 14. Unaweza kutumia Asali pamoja na kitunguu saumu kimoja ukachanganya na Asali kijiko kimoja kikubwa ukawa unakula kila siku asubuhi na jioni. Kitunguu saumu kimoja kizima kikate mara 2 utumie asubuhi kuchanganya na kijiko kimoja cha Asali na jioni fanya hivyo kila siku. Dawa zingine hiz hapa chini .

UNASUMBULIWA NA MAFUA? KULA VIFUATAVYO

Mafua
ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa, kutoka msimu wa joto kuingia baridi au kutoka msimu wa kiangazi kuingiza masika. Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua, ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.

Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.

SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.

VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.

CHAI
Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the American College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.

Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku. Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa mtoto wa shule siyo mbaya. Kwa mtu mzima, asizidishe vikombe vitatu kwa siku. Ikumbukwe kuwa chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu. Kunywa kiasi kwa afya yako.

MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.

ASALI
Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua. Asali inasaida kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.

Watoto wanaoruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri kati ya miaka 2 hadi 5. Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6-11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.

MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilichonacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunduza siku za kusumbuliwa na ugonjwa kukohoa.

CHOKOLETI NYEUSI
Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa ‘chocolate’ nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalika huwa kinga kwa maambukizi mengine.

PWEZA
Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.

VIAZI VITAMU
Kirutubisho aina ya ‘Beta-carotene’ huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).

Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine, unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwili unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza kila mara.
 
Endelea na hiyo dawa kwa muda wa siku 14. Unaweza kutumia Asali pamoja na kitunguu saumu kimoja ukachanganya na Asali kijiko kimoja kikubwa ukawa unakula kila siku asubuhi na jioni. Kitunguu saumu kimoja kizima kikate mara 2 utumie asubuhi kuchanganya na kijiko kimoja cha Asali na jioni fanya hivyo kila siku. Dawa zingine hiz hapa chini .

UNASUMBULIWA NA MAFUA? KULA VIFUATAVYO

Mafua
ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa, kutoka msimu wa joto kuingia baridi au kutoka msimu wa kiangazi kuingiza masika. Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua, ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.

Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.

SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.

VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin' ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.

CHAI
Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the American College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.

Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku. Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa mtoto wa shule siyo mbaya. Kwa mtu mzima, asizidishe vikombe vitatu kwa siku. Ikumbukwe kuwa chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu. Kunywa kiasi kwa afya yako.

MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.

ASALI
Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua. Asali inasaida kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.

Watoto wanaoruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri kati ya miaka 2 hadi 5. Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6-11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.

MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilichonacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunduza siku za kusumbuliwa na ugonjwa kukohoa.

CHOKOLETI NYEUSI
Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa ‘chocolate' nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalika huwa kinga kwa maambukizi mengine.

PWEZA
Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.

VIAZI VITAMU
Kirutubisho aina ya ‘Beta-carotene' huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).

Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine, unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwili unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza kila mara.
Haya kaka asante, tutaendelea kuwasiliana
 
Back
Top Bottom