Creams zinasaidia ila kama hujui kuitunza ngozi yako chunusi zinarudi pale pale
Jaribu kutumia *botouer ant acne (kama ngozi yako ni ya mafuta sana)
Botouer whitening (kama una ngozi kavu)
Pendelea kuosha uso na maji ya uvuguvugu na sabuni za herbal
Usipake mafuta mazito usoni, ukitembea kwenye jua kali sana hakikisha unakitambaa cha kujifutia uso na immediately unavyofika home osha uso
Yani uso uwe unacheza sana na maji, pia pendelea kunywa maji mengi sana, punguza vyakula vya mafuta mengi
Njia za asili
Changanya ndizi mbivu, limao na manjano paka usoni kaa nayo dkk20 osha uso na maji ya uvuguvugu
Asali, limao, manjano, liwao
Nyanya, sugulia usoni
Uteute wa alovera paka usoni, dkk 20-30 osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu
Nb:
Usikamue chunusi (maybe zile za njano maana zinaleta muonekano wa kinyaa kwako na kwa watu unaokutana nao) usikamue ukitumia hayo maelekezo niliyotoa zitakauka na kuisha kabisa zenyewe
It depends na ngozi inareact vipi kuna inayowahi na zinazochelewa, usichoke kama majibu ni ya taratibu mno
Unapokamua chunusi ndio zinaleta black spots/dots usoni na kuongeza idadi ya chunusi (yale majimaji, maana ngozi ya uso ni laini sana na very sensitive)