Naomba msaada wa kuondoa madoa na chunusi usoni

Naomba msaada wa kuondoa madoa na chunusi usoni

Mkuu una umri gani? hivyo vitu vinaendana na umri...ukishafika 30 Hakuna chunusi zitakusumbuwa,,,sasa utahangaika sana,,cha kukushauri TAFUTA SABUNI NZRI YA MEDICATED..na lotion ambayo sio strong,,, na usitumie cream yeyote,,,hyo cream ndy inakuletea chunusi...hakikisha usiku unaosha USO wako na SABUNI then usipake lotion yeyote...iwe unapaka lotion asubuhi tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengine tulijibiwa mpaka tuzae.
 
Wengine tulijibiwa mpaka tuzae
Kuna umri kuanzia balehe hadi 25 chunusi zinasumbuwa sn,,Mimi nilisumbuka sn na chunusi,,nilikuwa hadi naona aibu kukutana na watu,,nilikuwa kwny umri wa secondary,,, kufika 30 ziliacha zrnywe,,kwhyo usisumbuke sn mkuu,,fuata niliyokushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una umri gani? hivyo vitu vinaendana na umri...ukishafika 30 Hakuna chunusi zitakusumbuwa,,,sasa utahangaika sana,,cha kukushauri TAFUTA SABUNI NZRI YA MEDICATED..na lotion ambayo sio strong,,, na usitumie cream yeyote,,,hyo cream ndy inakuletea chunusi...hakikisha usiku unaosha USO wako na SABUNI then usipake lotion yeyote...iwe unapaka lotion asubuhi tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio 30 tu ni mpaka zaidi ya hiyo 30

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Melodia,

Usitumie cream yoyote

Kunywa maji mengi,pata muda wa kupumzika/kulala,epuka vyakula vya mafuta mengi na osha uso/oga kabla hujalala kila siku (usilale ukiwa umepaka chochote usoni)

Mie huwa napata chunusi pia nikikasirika kasirika ama kuwa na stress so nafikiri nayo inaweza kuwa sababu
ohh nzuri sana umedhihirisha kuwa chunusi ni tatizo la ndani so linapaswa kutibiwa ndani zaidi ya nje, maana ukihangaika nalo nje utaona limeisha ila kukikaaa baada ya muda kidogo pasipo kutumia hizo dawa za nje au cream inamaanisha tatizo litajitokeza tena maanamzizi haujang'olewa.

Maranyingi ni tatizo la homoni, dawa ni kushughulikia homoni hizo ili zisifanye uharibiffu ndani ambapo matokeo huonekana nje.

But umeelezea vyema sana baada ya kugundua kwako inatokeaje
 
Kama bado unasumbuliwa nenda duka la vipodozi nunua Extra claire kavu.

Utakuja kunishukuru
 
Chukua unga wa dengu na limao.jioni kabla ya kulala koroga na paka. Uache zaidi ya masaa manne. Then nawa na maji tuu. Asubuhi usitumie mafuta aina yoyote.Ndani ya wiki moja utaona matokeo mazuri
 
Na mimi nilipata chunusi sana. Ngozi yangu sio nyeupe labda nishauri tu jaribu kutumia sabuni ya ASANTEE (Tamarind & Honey). Unaosha uso (usiache povu-unanawia tu) pia unaweza ukaogea mwili mzima. Tumia mara mbili kwa siku ukiamua kuogea mwili mzima. Binafsi nimeanza kuitumia kwa wiki sasa napata maendeleo mazuri chunusi zinakauka. Ila hakikisha unapaka mafuta usoni mepesi (mfano blackseed oil yaani habat sawda haya yapo maduka ya wapemba kkoo au maduka ya urembo au ya vitu vya asili) maana ngozi itakaushwa na hio sabuni..haitakiwi ibakie kavu vinginevyo itamenyeka. Kama ngozi yako ni ya mafuta usitumie olive oil au coconut oil.

unaweza tengeneza scrub ya asili nyumbani (ya asali, au ya liwa au ya kahawa) halafu mara moja kwa wiki unafanya scrub usoni mpaka shingoni (au hata mwili mzima) usoni unapitisha tu mkono kwa kuzunguka viduara taratibu kama unaogesha mtoto (usisugue kabisa)..unaweza ukasuuza halafu ukaosha hata mara mbili.
Pia jitahidi kunywa maji mengi, kufanya mazoezi na kula mboga mboga na matunda kwa wingi. Ngozi nzuri ni matokeo ya afya nzuri.

Kama upo na stress jitahidi sana kupunguza mawazo kwani huongeza tatizo.

Pia ni vizuri uonane na daktari, pengine una allergy na kitu (chakula au kiungo fulani) ambacho hupelekea wewe kupata chunusi.

Hayo ni maoni yangu. Nitoe angalizo kiwa mimi sio mtalaam wa ngozi. Naongelea uzoefu tu na experience yangu na chunusi.

Naamini utapata suluhisho.
 
Habari wakuu,
Ninaomba msaada kwa mwenye uelewa wa cream nzuri(isiyochubua please)kuondoa tatizo la chunusi usoni kwangu.

Nimeshatumia vitu vingi Lakini baada ya muda tatizo hurudi.Ninaomba mwenye Tiba ya uhakika anisaidie.

Nimesikia La vista cream inasaidia na haichubui Kuna mwenye testimony na hili?

Asanteni!

Sent using Jamii Forums mobile app

JINSI YA KUONDOA CHUNUSI USONI KWA KWA HARAKA ZAIDI.

Na:Mr tibalishe

Chunusi ni vipele vinavyojitokeza katika ngozi hususan sehemu za usoni, kifuani na mgongoni kutokana na mafuta kushindwa kutoka kwenda nje ya mwili (juu ya ngozi ya nje). Huweza kutokea kwa mtu yeyote aliyepevuka kimwili, japokuwa wanawake hutokewa zaidi na vipele hivi.

SABABU ZA CHUNUSI
Sababu kubwa ya chunusi ni kukaa kwa mafuta chini ya ngozi ya nje na kusababisha uvimbe. Hii inatokana na mafuta hayo kuzalishwa kwa wingi zaidi au kushindwa kupita kwenye matundu ya kutolea mafuta kwa sababu matundu hayo yameziba.
Pia bakteria wa chunusi huweza kushambulia ngozi na kusababisha chunusi au kuzifanya chunusi kuwa nyingi zaidi na kubwa kubwa
Vitu vinavyosababisha au kuongeza ukubwa wa chunusi ni pamoja na
1. Kiasi kikubwa cha mafuta kwenye ngozi
2. Kuziba kwa matundu ya kutolea mafuta kwenye ngozi
3. Homoni za uzazi mwilini (Androgens)
4. Msongo (Stress)
5. Maambukizi ya bakteria wanaosababisha chunusi
6. Kemikali (vipodozi) kali au zisizoendana na ngozi ya mtu
7. Aleji (Mzio) kwa baadhi ya vipodozi na kemikali zingine
8. Baadhi ya vyakula (vinavyotokana na maziwa, chipsi na chokoleti)

NINI CHA KUFANYA?
Ukitokwa na chunusi cha kwanza hakikisha unakuwa mwangalifu ili usiziongeze zaidi. Tafuta sababu insayozisababisha na kisha iepuke au iondoe hiyo kwanza
Cha pili epuka kupasua chunusi. Kupasua chunusi husababisha makovu chunusi zitakapopona
Tatu tafuta matibabu na uanze matibabu mapema. Ni rahisi zaidi kutibu chunusi ukiziwahi kuliko ukiwa umechelewa

MATIBABU YA CHUNUSI
Matibabu ya chunusi hutegemea na ngozi ya mtu na chanzo kinachosababisha hizo chunusi. Matibabu hayo mara nyingi hulenga kuua bakteria wanaosababisha chunusi hizo, kupunguza mafuta na kuzibua matundu ya kutolea mafuta ili mafuta yaweze kupita na kwenda nje ya ngozi.

1. Kuua Bakteria wanaosababisha Chunusi
Bakteria hawa huuliwa kwa kutumia dawa za kuua bakteria zijulikanazo kama Antibiotics. Utaalam na umakini unahitajika katika matumizi ya dawa hizi Pia ni lazima zitumike kwa maelekezo ya daktari

2. Kupunguza mafuta juu ya ngozi na kuondoa mafuta yaliyoziba matundu ya mafuta
Hii ni njia kubwa sana na rahisi ya kukabiliana na chunusi. Kwa kuwa mafuta ni sababu kuu kwa watu wengi basi njia hii husaidia watu wengi sana.
Hili huweza kufanywa kwa kutumia
- Sabuni za PROTEX (Iliyoandikwa DEEP CLEAN) na PEARS (Iliyoandikwa OIL CLEAR)
- Poda ya POND’S (Iliyoandikwa OIL CONTROL)
- Sabuni za maji za kusafishia uso na kuondoa uchafu na mafuta ya ziada (Face Wash au Facial Cleansers)

3. Kuondoa uchafu wote na seli zilizokufa na kuziba matundu ya kutokea mafuta kwenye ngozi
Njia hii hufanya kazi vizuri sana pia. Uchafu huo na seli zilizokufa zikiondolewa mafuta hupita vizuri na kwenda nje ya ngozi bila kusababisha chunusi. Matokeo yake mtu hupona chunusi na pia kuzizuia zisijitokeze.
Hili hufanywa kwa kutumia dawa zinazoondoa utando wa uchafu na seli zilizokufa zilizopo juu kabisa ya ngozi.
Mifano yah ii ni Persol Gel

MUHIMU:
- Ili kudhibiti vizuri chunusi na kuziondoa kabisa unahitajika kujua kwa usahihi kabisa chanzo cha chunusi hizo na vinavyoziongeza
- Mara nyingi chunusi hutibiwa kwa kutumia zaidi ya dawa moja au kipodozi kimoja. Jua vizuri mchanganyiko wa dawa na vipodozi vya kutumia
- Tumia dawa na vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Tofauti na hapo chunusi zitaongezeka zaidi
- Kutibu chunusi vizuri na kwa usalama kunahitaji muda. Kuwa mvumilivu na tumia vitu vyote kama ulivyoelekezwa
- Usipasue chunusi. Utabaki na makovu ambayo nayo pia yatakusumbua

Kwa maelezo zaidi, ushauri na matibabu ya Chunusi, Makovu, Madoa, Mafuta mengi usoni.
SHARE MARA NYINGI UWEZAVYO MUNGU ATAKUBARIKI

NIMECOPY NA KUPASTE KUTOKA KWENYE THREAD INGINE.
 
Na mimi nilipata chunusi sana. Ngozi yangu sio nyeupe labda nishauri tu jaribu kutumia sabuni ya ASANTEE (Tamarind & Honey). Unaosha uso (usiache povu-unanawia tu) pia unaweza ukaogea mwili mzima. Tumia mara mbili kwa siku ukiamua kuogea mwili mzima. Binafsi nimeanza kuitumia kwa wiki sasa napata maendeleo mazuri chunusi zinakauka. Ila hakikisha unapaka mafuta usoni mepesi (mfano blackseed oil yaani habat sawda haya yapo maduka ya wapemba kkoo au maduka ya urembo au ya vitu vya asili) maana ngozi itakaushwa na hio sabuni..haitakiwi ibakie kavu vinginevyo itamenyeka. Kama ngozi yako ni ya mafuta usitumie olive oil au coconut oil.

unaweza tengeneza scrub ya asili nyumbani (ya asali, au ya liwa au ya kahawa) halafu mara moja kwa wiki unafanya scrub usoni mpaka shingoni (au hata mwili mzima) usoni unapitisha tu mkono kwa kuzunguka viduara taratibu kama unaogesha mtoto (usisugue kabisa)..unaweza ukasuuza halafu ukaosha hata mara mbili.
Pia jitahidi kunywa maji mengi, kufanya mazoezi na kula mboga mboga na matunda kwa wingi. Ngozi nzuri ni matokeo ya afya nzuri.

Kama upo na stress jitahidi sana kupunguza mawazo kwani huongeza tatizo.

Pia ni vizuri uonane na daktari, pengine una allergy na kitu (chakula au kiungo fulani) ambacho hupelekea wewe kupata chunusi.

Hayo ni maoni yangu. Nitoe angalizo kiwa mimi sio mtalaam wa ngozi. Naongelea uzoefu tu na experience yangu na chunusi.

Naamini utapata suluhisho.
Mkuu samhan iv kW mfano mm n mweusi nikiogea hio asantee sabun haiwez nichubua nikawa mweupe we unaionaje ukitumia?
 
Habari wakuu,
Ninaomba msaada kwa mwenye uelewa wa cream nzuri(isiyochubua please)kuondoa tatizo la chunusi usoni kwangu.

Nimeshatumia vitu vingi Lakini baada ya muda tatizo hurudi.Ninaomba mwenye Tiba ya uhakika anisaidie.

Nimesikia La vista cream inasaidia na haichubui Kuna mwenye testimony na hili?

Asanteni!

Sent using Jamii Forums mobile app
Jitahidi kuoga vzuri tu Macream yatakuchubua na kukuongezea hyo michunusi

Naomba kuwasilisha
 
Mkuu samhan iv kW mfano mm n mweusi nikiogea hio asantee sabun haiwez nichubua nikawa mweupe we unaionaje ukitumia?

Sijaona kama imenichubua au kunifanya kuwa mweupe. Kuna ambazo nimesikia ni kali kama ile ya papai unatakata. Nilishauriwa kwa ngozi yangu nitumie ya ukwaju. Ile sabuni inaondoa chunusi kabisa na binafsi imenipa matokeo mazuri. Ila sasa baada ya chunusi kuisha unastop kutumia. Nilishauriwa hivyo. Nilitumia pakti moja tu zikaisha.

Saa hivi nipo kwenye kuangalia jinsi ya kuondokana na makovu (natumia clear essence medicated fade cream-inapatikana maduka ya SH Amon na Zurii House of Beauty) naona safari inaenda vizuri. Kwa mkoani sifahamu inapopatikana ila kwa DSM zipo hapo.

Kwenye upande wa sabuni, situmii tena Asantee natumia PEARS ya rangi ya njano naogea mwili mzima. Nimependa matokeo yake kwa ngozi yangu. Hii nanunuaga maduka yale ya wapemba.

Nikukumbushe kutafuta na kutumia Moisturizer nyepesi sana usoni isiyo na mafuta (oil free moisturizer) ili ngozi isibaki kavu vinginevyo ngozi itabaki kavu na utamenyeka. Asantee inakausha ngozi katika kutoa chunusi. Huo ndo mrejesho wangu mpaka hivi sasa.

Kila la kheri.!
 
Shukrani Mkuu ngoja nifanye mpango nikachukue n mm nianze kutumia nijaribu naamin n hio sabun nitaipata sababu nipo tanga wapemba km wote
 
Tafuta sabuni flani iv inaitwa AHSANTE ya ukwaju.. Baada ya mwez mmoja na nusu njoo hapa utoe ushuhuda.. Tumia kwa kunawia Au kuogea.... Achana na vi tube vitakuchubua
 
Tafuta sabuni flani iv inaitwa AHSANTE ya ukwaju.. Baada ya mwez mmoja na nusu njoo hapa utoe ushuhuda.. Tumia kwa kunawia Au kuogea.... Achana na vi tube vitakuchubua
Pamoj ndug soyuncu
 
Creams zinasaidia ila kama hujui kuitunza ngozi yako chunusi zinarudi pale pale

Jaribu kutumia *botouer ant acne (kama ngozi yako ni ya mafuta sana)
Botouer whitening (kama una ngozi kavu)

Pendelea kuosha uso na maji ya uvuguvugu na sabuni za herbal

Usipake mafuta mazito usoni, ukitembea kwenye jua kali sana hakikisha unakitambaa cha kujifutia uso na immediately unavyofika home osha uso

Yani uso uwe unacheza sana na maji, pia pendelea kunywa maji mengi sana, punguza vyakula vya mafuta mengi

Njia za asili

Changanya ndizi mbivu, limao na manjano paka usoni kaa nayo dkk20 osha uso na maji ya uvuguvugu

Asali, limao, manjano, liwao

Nyanya, sugulia usoni

Uteute wa alovera paka usoni, dkk 20-30 osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu

Nb:
Usikamue chunusi (maybe zile za njano maana zinaleta muonekano wa kinyaa kwako na kwa watu unaokutana nao) usikamue ukitumia hayo maelekezo niliyotoa zitakauka na kuisha kabisa zenyewe

It depends na ngozi inareact vipi kuna inayowahi na zinazochelewa, usichoke kama majibu ni ya taratibu mno

Unapokamua chunusi ndio zinaleta black spots/dots usoni na kuongeza idadi ya chunusi (yale majimaji, maana ngozi ya uso ni laini sana na very sensitive)
sawa sawa!
 
Back
Top Bottom