Mkuu naomba msaada wako maana nimeagiza Caldina na ina engine ya D4 nimeona huu uzi nimeshtuka kidogo nipe uzoefu wako wa nini nifanye maana nimeshaagiza tayari naomba kujua hasa kwenye ishu ya mafuta naona wadau wanasema mafuta yetu ni tatizo kwa D4 na lolote lile ambalo ni usefull ili niifanye motorcar yangu isiwe kimeo.
Nashidwa kuelewa kwanini watanzania tumezidi kwa uwongo na kuchangia hata tuichokijua, utasemaje D4 Engine ni ugonjwa wa moyo? Come on guys. Mi nina Vista Ardeo D4 Engine huu mwaka wa saba sasa na haina shida, yaan nimeisha safiri nayo nchi nzima bila shida na hata sasa hivi ukinambia twende wapi, ni mafuta tu then safari.
Cha msingi hapa kwa haya magari ya kisasa ni service na maintainance tu, vitu vyote vinataka nidhani ni sawa na kusema ipad au tablet sio komputer nzuri sababu ni delicate....come on !!!!
Tuache uwongo.
Mwenye tatizo na Engine ya D4 aniulize nimsaidie.
maana mara nyingi ni sensor tu ndo zinazengua na unakuta ni uchafu tu ilaukisafisha au kuipa safari ndefu kidogo ule uchafu unaungua then haiwezi kusumbua. Tatizo kubwa la kuwa nayo makini ni service tu. na aina ya engine oil na air filter lazima viwe geniune.
pia usiende kwa mafundi wasio na komputa, maana mfumo wake ni wa kisasa so lazima waipime kwa komputa ndo utajua tatizo nini.
Mara nyingi inakuwa na mis au kuzima zima ambao ni tatizo dogo sana kama nilivyoeleza hapo juu.
Yes kwa swala la mafuta, usiweke ya mtaani kwenye madumu, weka vitu ambavyo unauhakika navyo na usiwe unabadiri badiri.
Mi nina genereta ya diesel na nissan patrol ya diesel td 42 engine, juzi nimejisahau nikaweka petrol kwenye jenereta baada ya muda ikaleta mis za ajabu na iakazima mpaka nime drain mafuta yote na kusafisha then kuweka diesel ndo ikawaka, so hayo mafuta yenye mchanganyiko wa diesel na petrol nikaongeza diesel na kuyatumia kwenye nissan maana sikutaka kujaribu kwenye D4 Engine hahahaha nadhan ndo ungekuwa mwisho wake hahaha