Naomba muongozo wa kupata vibali vya kusafirisha nyama

Naomba muongozo wa kupata vibali vya kusafirisha nyama

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Habari,

Nataka niwe nasafirisha nyama kutoka Tanzania bara kupeleka Tanzania visiwani. Mwenye uzoefu wa hii biashara naomba anifahamishe kuhusu namna ya kupata vibali na nyaraka zote zinazohitajika katika biashara hii. Na namna nzuri ya usafirishaji na kufanya packing.

Asante.
 
Vibali nenda Ofisi za Veterinary pale Tazara ndio vilikuwa vinatolewa, ukiwa nacho mwaka mzima utatumia. Gharama za boti wanachaji kwa uzito au Cubic Metre, Bandari utalipia port charges kwa kila cubic metre 1 kwa shilingi 11,500/=. Nyama inatakiwa usafirishe kwa boti ya kwanza asubuhi
 
Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?
 
Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?
Hicho ni kwa ajili ya Zanzibar nje ya nchi kuna vibali vingine.

Kwanini usisafirishe Mbuzi, ukachinjie kule kule
 
Ni mbuzi mkuu.
Vipi kwani nguruwe kuna kipengele gani mkuu?
Ninavyojua kwa uelewa wangu mdogo ile ni nchi ya kiislamu (tukubali tukatae) na nilikua na ndugu yangu alikua naapeleka sana kitimoto kwenye mahoteli ila alikuja kiacha na kila nikimuuliza ananiambia ndugu yangu we acha tu acha hizo stori acha kabisaaaaa. Kila nilipomuuliza aliishia kusema hivyo. Japo wapo wavaa kanzu nao wanafanya hiyo biashara na ndo waziba mirija
 
Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?
Nje ya nchi inabidi unayempelekea akupe vigezo vya aina ya nyama iweje,ufunge vipi ili ikidhi kuingia nchini kwao.

Kibali cha mifugo,chakula na gharama za kusafirishia na Clearing and fowarding agent
 
Nimeshauriwa kuchinja ni bora zaidi
Ok, unaweza ukafunga kwenye mifuko ya nailon kisha ukaweka kwenye viroba kwa kilo 100.

Kama unaharaka na mzigo unatakiwa ukienda pale Azam Marine, kuna wadau wanavyo vibali kwenye mfuko wa shati. Unaomba ukitumie kwa trip kisha umpe malipo yake wanakodisha wapo standby
 
Back
Top Bottom