Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?Vibali nenda Ofisi za Veterinary pale Tazara ndio vilikuwa vinatolewa, ukiwa nacho mwaka mzima utatumia. Gharama za boti wanachaji kwa uzito au Cubic Metre, Bandari utalipia port charges kwa kila cubic metre 1 kwa shilingi 11,500/=. Nyama inatakiwa usafirishe kwa boti ya kwanza asubuhi
Hicho ni kwa ajili ya Zanzibar nje ya nchi kuna vibali vingine.Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?
Ninavyojua kwa uelewa wangu mdogo ile ni nchi ya kiislamu (tukubali tukatae) na nilikua na ndugu yangu alikua naapeleka sana kitimoto kwenye mahoteli ila alikuja kiacha na kila nikimuuliza ananiambia ndugu yangu we acha tu acha hizo stori acha kabisaaaaa. Kila nilipomuuliza aliishia kusema hivyo. Japo wapo wavaa kanzu nao wanafanya hiyo biashara na ndo waziba mirijaNi mbuzi mkuu.
Vipi kwani nguruwe kuna kipengele gani mkuu?
Nje ya nchi inabidi unayempelekea akupe vigezo vya aina ya nyama iweje,ufunge vipi ili ikidhi kuingia nchini kwao.Asante sana mkuu, ubarikiwe. Kwahiyo nikikata hiki kibali, kitatumika kusafirishia mzigo popote pale iwe ndani au nje ya Tanzania?
Ok, unaweza ukafunga kwenye mifuko ya nailon kisha ukaweka kwenye viroba kwa kilo 100.Nimeshauriwa kuchinja ni bora zaidi