Naomba mwenye amewahi kutumia TV za Alitop anisaidie kujua strength na weakness zake

Wadau kuna na hizi TV za Itel naona sana mtangazo yake , vipi quality yake ziko vizuri au midosho ?
 
Kama kweli ni muuzaji mzoefu nipe bei ya hisense 55 kwa sasa na Goodvision 55
Au hata hisense 43 smart na Goodvision 43 smart. Kidogo nmepunguza heshima yangu kwako.
 
Kwa Sasa,
Tv quality kwa uimara na picha nzuri na ya mtu asiye na uchumi mkubwa

Ni GOODVISION

Changamoto Yao:
Size ya vioo kwa baadhi ya size wanapunja mno

Mfano:
[emoji117]inchi 42 ya goodvision,
Kiuhalisia ukiipima Ni nchi 40

[emoji117]Inch 43 ya goodvision,
Kiuhalisia ukiipima Ni nchi 42

[emoji117]Nch 32 Hii imetimia

[emoji117]Nchi 25 ya goodvision
Kiuhalisia ukiipima Ni nchi 24

[emoji117]Nchi 24 ya goodvision
Kiuhalisia Ni nchi 22

Hizi nyingine ndogo ndogo zote wameiba nchi 2 kila tv
 
55 hisense kwa sasa ina range 1,550,000 had 1,600,000 inategemea
Wakat soyi ambae ndio Goodvision kwa sasa had 1,150,000 unapata au chini ya hapo. So ni vizur ukamwambia mshikaji ukweli

Kingine kusema tv za hisense znapatikana kwa wingi ni uongo

32 smart, 43 smart, 50, 55, 58, 65 hizi kupata ni mtihani sanaaa japo znapatikana kwa uchache ila bei kubwa. So mwambie ukweli kama ana hela aongeze ila sio kumdanganya aongeze 30 had 50
 
Kama kweli ni muuzaji mzoefu nipe bei ya hisense 55 kwa sasa na Goodvision 55
Au hata hisense 43 smart na Goodvision 43 smart. Kidogo nmepunguza heshima yangu kwako.
Bei hizo Apo mkuu
 
Mtoa mada kaongelea alitop 32"
Ambayo Bei ya sokoni mpya Ni 270,000
Hizo nyingne unazotaja, uwezo wake haujafika hapo

wakati goodvision mpya Ni 295,000
Ambapo soyi mpya bei Yake Ni 280,000

Hata Kama wauzaji wanatofautiana vipi
Utofauti wa Bei hauwezi kuzidi elfu 20, 30 maximum 50.

Vinginevyo awe kapigwa
 
Mkuu vipi kuhusu Aborder, wao ubora wao ukoje, na nimeona wametoa 32" smart TV, ikoje hii pia, nahitaji kuchukua hii

Asante
 
55 hisense kwa sasa ina range 1,550,000 had 1,600,000 inategemea
Wakat soyi ambae ndio Goodvision kwa sasa had 1,150,000 unapata au chini ya hapo. So ni vizur ukamwambia mshikaji ukweli

Udhaifu wa soyi na goodvision mpk Bei kua chini Ni kwamba size zilizoandikwa kwenye box hazitimii.

Ikumbukwe hizi zote zinauzwa na mkorea mmoja anaesupply hizo tv Tanzania nzima

Ambaye uyo uyo ndie anaesupply pia tv za HQ.

Mfano,
iyo nchi 55 ya soyi na goodvision,
Ukiipima kiuhalisia Ni nchi 49 na haifiki 55

Kwaiyo huwezi Sema umeuziwa Bei rahisi wakat umeuziwa Bei sawasawa kabisa na size yake kwa kampuni zinazotimiza size.

Mkorea wa goodvision na soyi Ni mhuni kwenye kucheza na box zake.

Kama kweli wee Ni muuzaji,
Nna imani kua huu uhuni wa kupunja size ushakutana nao makampuni mengi.
 
Mkuu vipi kuhusu Aborder, wao ubora wao ukoje, na nimeona wametoa 32" smart TV, ikoje hii pia, nahitaji kuchukua hii

Asante
Mazuri yao:
Kwenye uBora wa picha wako vizur,
Kwenye uimara nako hawasumbui Sana, isipokua Taa za kwenye vioo vyao (backlight) zinaungua HARAKA Kama hutumii tv guard.

Changamoto 01:
Sema Sasa tv zao haziingiliani spea yoyote na kampuni nyingine yoyote ile. Hadi vioo huwa vinazidi sentimental kadhaa mbele.

Kwaiyo tv Yao ikipata shida
Inakulazimu uwapelekee wakatengeneze wao wenyewe pale kwenye service centre zao za msimbazi na pale gerezani.

Uzur Ni kwamba wanatengeneza bure, Ila Bei ya spea na kuagiza utalipa wewe. Ambapo spea zao ziko expensive.

Changamoto 02:
Tv zao zinatoka kwa version na zote haziingiliani spea.
Mf: Kama ulinunua aborder 32" ya mwaka 2019 jua haiingiliani spea yoyote na aborder ya mwaka 2021 au 2022

Maana ake,
Kama tv yako Ni kizamani, itabidi usubiri Sana spea ije uko wanakoagiza Kama special order.
 
Kwenye boss umenena. Nilinunua ya kusukumia muda ila ni mwaka wa tatu inaelekea ipo fresh kabisaa
 
Kumbe WA gonjwa wengi humu.......wee umesikia wapi kuna TV inaitwa alitop kama sio China's sheet.......nunua uone inavyogeuka Chini juu juuchini ndio utakuwa umejifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…