Naomba mwenye kufahamu utaratibu wa kurudia masomo ya kidato cha nne

Status
Not open for further replies.

BMW P9

Member
Joined
Feb 19, 2022
Posts
66
Reaction score
87
Habarini za kazi wapendwa poleni na majukumu ya kila siku

Naomba mwenye kufahamu utaratibu wa kurudia masomo ya kidato cha nne aniambie je? iwapo mtu anataka kurudia masomo yote aliyofanya mwanzao inawezekana na atapewa cheti kingine na division mpya tofauti na ya awali au utaratibu ukoje

Naomba kwa anae faahamu anijulishe.
 
Kwanza Dirisha La Usajili Lishafungwa Kwa Mwaka Huu (2022) ,Huwa Wanafungua Kuanzia Tarehe 01/01 Hadi 31/03 ,

Pili Wanaruhusu Kurudia Idadi Yeyote Ya Masomo Unayohitaji ,

Tatu ,Ukirudia Unapata Alama Mpya Na Cheti Kipya (Hawaunganishi Matokeo Ya Zamani Na Mapya )

Utaratibu Wa Kuomba Nafasi Unaanzia Kituo Unachohitaji Kujisajilia Wanakupa Muongozo,

Kama Una Swali Niulize.
 
Uzi huu auone pia Eric Shigongo, mzee wa kusoma Bachelor's degree bila kupitia elimu ya sekondari
 
Kwanza inategemea masomo ya aina gani science au art?

Usajiri umeshafungwa ungewahi mwakani mwezi wa pili .
Unatakiwa uende kituo (shule,) utskayofanyia mtihani unalipa 50000, ili wakupe namba ya mtihani .

Then utaenda posta kuchukua fomu ya necta na kujaza ili uombe kufanya mtihani ni 15000.
Kisha subiri kati kati ya mwezi huo watakuja kuhakiki pale kituo utachofanyia mtihani ikiwemo namba yako mpya na ya zamani, then masomo mangapi umechukua.

Kama ni art basi ukichukua masomo chini ya saba utaendelea na cheti kile kile.

Ukichukua saba ndio unapata cheti kipya cha mwanzo kinavunjwa.

Pia ni ngumu kupata hata division 3 iwapo utachukua masomo chini ya 7 kwa na,9, kwa science..
 
Nilifanya masomo nane ya arts pamoja na kemia kwaio ili nipate cheti kipya inatakiwa nifanye yote nane
 
Hapana saba pia yanatosha sababu kiwango kinachotakiwa cha masomo ya art ni 7 tu mkuu hapo utapata cheti kipya.
 
Na kama mtu akisajili masomo yote lakini akashindwa kufanya somo moja wapo atapata cheti au itakuaje
Ushauri, sajili masomo ambayo utaweza kuyafanya, ila kama kuna somo utashindwa kulifanya wataweka nyota tu cheti unapata. Cheti kinatoka ukipata KUANZIA D mbili au C moja.
 
Na je kuna limitation ya muda toka umemaliza elimu ya sekondari maana kwa sasa mimi nina mwaka wa 9 na bado nina ndoto ya kurudia mtihani wa kidato cha nne mwakani!
 
Hakuna Limitation, Kipindi unajisajili wao wataomba tu namba yako ya kidato cha nne ya miaka hiyo na watakupatia namba mpya
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hapana saba pia yanatosha sababu kiwango kinachotakiwa cha masomo ya art ni 7 tu mkuu hapo utapata cheti kipya.
Nashukuru sana kwa mwongozo vipi na cheti kitaandikwa mwaka nilio rudia mtihani au kitakua kipya lakini mwaka ule ule
 
Nami nahitaji kufanya mtihani wa somo moja pekee la Biology ambalo si kulifanya hapo kabla.Cheti changu kina masomo 10 ambayo ni English,Civics,Kiswahili,Geography,Basic Mathematics,Chemistry,Engineering Science,Surveying,Architectural Draughting na Building Construction. Je,naweza kuongeza somo la 11?.Muongozo wadau.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom