Naomba Mwenye Picha ya Mbowe na Viongozi wa CHADEMA Wakishiriki Msibani kwa Mama Mzazi wa Halima Mdee

Mbowe anahusika vipi hapo kwenye msiba au chadema for that matter?
Kwani Msigwa na Jobo wakienda hawatoshi?
 
Mtoto akikosea huadhibiwa. Kwa huu utoto wa CHADEMA tutawadhibu kwenye sanduku la kura.
 
Siyo vizuri kutumia msiba wa watu kufanyia siasa ndugu. Huko unapotaka tuelekee sipo .
 
Ila Lucas sijui sometimes akili yako unaiweka wapi sijui.

Sasa unajua kabisa kina Halima na huyo Mbowe hawaelewani tena pakubwa tu unataka waende msibani kufanya nini
 
Ila Lucas sijui sometimes akili yako unaiweka wapi sijui.

Sasa unajua kabisa kina Halima na huyo Mbowe hawaelewani tena pakubwa tu unataka waende msibani kufanya nini
Mbona Mbowe alikuwa na akina Mheshimiwa Mdee kanisani kkkt alipokuwa anataka wamchangie mchango kanisani? Au umeshasahau mara hii?
 
HIYO HAPO


Kutoka Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa wa Mbinguni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam - Kibangu, lililopo Ubungo Kibangu sehemu ambapo ibada ya kuaga mwili wa Bi Theresia Mdee ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Viti maalum Halima James Mdee aliyefariki hivi karibuni inaendelea, tunakusogezea habari picha zikimuonesha Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe akiwa Kanisani hapo

Kwenye habari picha hii Mbowe anaonekana akiwa ameketi pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko, aliyekuwa mgombea Ubunge wa CHADEMA jimbo la Ubungo 2020 ambaye pia ni Mstahiki Meya wa zamani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob na waombolezaji wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…