Naomba mwongozo wa kununua Subwoofer

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032
Nina uhitaji wa Subwoofer kwa matumizi binafsi (nyumbani). Kama mnavyojua siku hivi kuna kampuni nyingi au aina kedekede za kichina zinazotengeneza hizo bidhaa.

Hivyo naomba mwongozo kwa wataalamu na wazoefu. Je, ninunue/nichukue ya kampuni gani,- ambayo ni imara na ina muziki wa ukweli unaokaribiana na Sony.
 
Kwa bajeti ya
Subwoofer za kichina Nunua SEAPIANO TU

Seapiano Nzuri Ni
  • SEA PIANO (Sp1002)
  • Hii Ni ya spika 2 fupi.
Inauzwa Kati ya 170,000- 190,000 inategemea na muuzaji.

-SEA PIANO (sp 910)
Hii Ni ya spika 2 ndefu.
Inauzwa Kati ya 300,000- 350,000 kutegemea na muuzaji.

- SEA PIANO (5-1 channel)
Hii Ina spika 4 ndefu,1 fupi.
Inauzwa Kati ya 450,000- 500,000 kutegemea na muuzaji


Ila Kama uwezo upo,
Nunua SOUND BAR za Lg au Sony

Changamoto:
1. samsung SOUND BAR usinunue.
KWANINI?
Zinawahi kuchoka haraka zikipigwa mda mrefu na kwa sauti kubwa.
Zile Power zake zinachemsha haraka na mda SI mrefu zinakua na mafua.

2. LG sound bar ni nzuri sana upate Zile zisizo na deki.
Zenye deki zinasumbua,
zinabagua baadhi ya music au video formats na ziko limited HUWEZ kuzitumia bila kuziunga Kwenye deki.
Inamaana deki ikizingua, spika zinabaki Kama makasha.

Bei zake zinarange kutegemea na muuzaji husika.
Watts 650- 450,000-550,000
Wats 750- 650,000 - 800,000
Watts 1000- 850,000- 950,000
Watts 1200- 1,000,000- 1,200,000

3. Sony ziko vizur sana,
Changamoto yake Ni mfuko wako TU, Bei imechangamka kutokana na watts(uwezo)

Bei zake zinarange kutegemea na muuzaji husika.
Watts 650- 500,000-650,000
Wats 750- 750,000 - 900,000
Watts 1000- 1,000,000- 1,200,000
Watts 1200- 1,200,000- 1,500,000
 
epuka tu vitu used!
 
Pine tech lakini lazima upate original
 
Asante
 
Hela yako tu mkuu ila hizo ndio kali
  1. Klipsch R-120SW.
  2. Polk HTS Home Theater Subwoofer.
  3. MartinLogan Dynamo Subwoofer.
  4. BIC America F12.
  5. Definitive Technology ProSub 1000.
  6. Audioengine S8. ...
  7. Bic Acoustech PL-200 II.
  8. SVS SB-1000.
 
Mwamba uko vizuri sina shaka na wewe hebu nipe update sahizi napata sabufa gani nzuri kwa 200,000?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…