Naomba mwongozo wa maneno ya kiswahili sanifu

Naomba mwongozo wa maneno ya kiswahili sanifu

Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2006
Posts
4,568
Reaction score
2,918
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali na watu mbalimbali wakiongea, Mfano ni leo bungeni kuna kamjamaa kalikuwa naona kanawasilisha mambo ya utumishi. Sasa hicho kiswahili kilinishinda nimeamua kubadilisha channel!!

THELATHINI------SELASINI
TATHMINI---------TASMINI
KURIDHIKA--------KURIZIKA
MARIDHAWA-----MARIZAWA
TAFADHALI---- TAFAZALI

Na mengine mengi ya jinsi hiyo. Sasa naomba waswahili wa kiswahili sanifu ambacho ninategemea kitumike bungeni lakini hata watu wakubwa serikalini wanachakachua!!! Hii ni mifano hai ni namna gani watu wamechoka na we do not care!!!!! hata kutamka!!!! Unless BAKITA walishaidhinisha kuwa hayo maneno yanaweza kutumika mbadala. NAOMBA MUONGOZO!!!!
 
mbona tayari umeshatoa mwongozo mwenyewe, sie tutoe mwongozo gani mwingine tena?
 
Nina maana ni sahihi kutumia maneno hayo?
 
siyo sahihi na tayari umeishaweka inavyotakiwa kwa usahihi!!
 
Ni commom mistakes katika lugha,mara nyingi wahusika wanajua usahihi lakini kutakana na maeneo waliyokulia wanajikuta ulimi umejenga mazoea ya kutotamka maneno kiufasaha,ni kama wale wenye kuweka R sehemu ya L na L sehemu ya R.
 
Kiswahili ni lugha ya watu?
Watu wepi hao?
Ni wazi huyo mzungumzaji uliyemsikia si mtu wa pwani, si mtu wa mwambao na kiswahili si lugha mama kwake.
Hata hivyo, kuna haja ya kuwapiga msasa wabunge ili watumie lugha ya kiswahili kwa ufasaha.
 
Sasa we ndugu naona umekuwa punguani..... nini hicho? ondoa upupu wako mbona usha jijibu?
 
Hilo ni tatizo la watu kutokuwa wamahiri wa lugha ya Kiswahili....Tatizo hilo laweza kutokana na athari za lugha mama,kutumia lugha zaidi ya moja, matatizo ya kimaumbile n.k. Tatizo hilo laweza kumpata mtu yeyote bila kujali mazingira anayotokea....
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali na watu mbalimbali wakiongea, Mfano ni leo bungeni kuna kamjamaa kalikuwa naona kanawasilisha mambo ya utumishi. Sasa hicho kiswahili kilinishinda nimeamua kubadilisha channel!!

THELATHINI------SELASINI
TATHMINI---------TASMINI
KURIDHIKA--------KURIZIKA
MARIDHAWA-----MARIZAWA
TAFADHALI---- TAFAZALI

Na mengine mengi ya jinsi hiyo. Sasa naomba waswahili wa kiswahili sanifu ambacho ninategemea kitumike bungeni lakini hata watu wakubwa serikalini wanachakachua!!! Hii ni mifano hai ni namna gani watu wamechoka na we do not care!!!!! hata kutamka!!!! Unless BAKITA walishaidhinisha kuwa hayo maneno yanaweza kutumika mbadala. NAOMBA MUONGOZO!!!!

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa haya ni makosa, tena yanayoweza kuepukika. Lakini, kwa kuwa unaomba mwongozo wa kiwahili sanifu, basi hatuna budi kuanza na wewe. Sitazungumzia hali ya kuchanganya lugha 2 (kiingereza na kiswahili) kama ulivyofanya (ambayo pia sio usanifu), ila nitazungumzia kiswahili chako.

Neno "kutegemea" yaani "depend/rely on" (kwa kiingereza) umelitumia vibaya. Nina uhakika ulitaka kusema "ULITARAJIA" yani "expect" kwa kiingereza.
Neno "kuchakachua" yaani (adulterate" kwa kiingereza) limekuwa likitumika vibaya siku za karibuni. Sina uhakika kama umelitumia kisanifu hapa (japo maana ya kimuktadha ingeweza kukubaliaka).
Na hako "kamjamaa kalikokuwa kanawasilisha"-hapo nako umeharibu lugha. Ungeweza kusema "kajamaa" kumbeza kuyo muwasilisha mada. Kwa maana ya kuwa ni kivumishi cha sifa-kama lengo lako lilikuwa kuifisha sifa yake. Lakini sio "Kamjamaa" Mtu "mjamaa"-yaani "socialist" ni mtu anayeamini katika falsafa ya ujamaa-mathalani ile ya Baba wa Taifa.

Kwa hiyo, tunapoona kibanzi machoni mwa wenzetu, tusisahau kuwa kuna boriti kwenye macho yetu. Pia unapojipanga kukosoa lugha jitahidi basi kukosoa kwa kutumia lugha sanifu. Maji taka hayatakatishi kaniki.

Tuendelee kujifunza.
 
Back
Top Bottom