Naomba neno moja tu la Kingereza ambalo halina tafsiri rasmi ya Kiswahili

Naomba neno moja tu la Kingereza ambalo halina tafsiri rasmi ya Kiswahili

Msaada wa kiswahili cha maneno yafuatayo...😂
Adenocarcinoma
Erythroblastosis fetalis
Gait
Retinoblastoma
Cubital fossa
Popliteal fossa
Dysdiadochokinesia
Ataxia
Oligodendrocytes
Astrocytes
Pericytes
Tuberosity 😂
Glossitis
Fontanelle
Mesoderm
Ectoderm
Endoderm
Extraembryonic coelom
Tubercle
Substantia nigra
Substantia feruginosa
Styloglossus
Thyrohyoid
 
Kwa muda mrefu sana nimekuwa napata wakati mgumu ninapoona baadhi ya maneno ya Kingereza haswa katika Technology au professional fulani kukosa tafsiri rasmi. Hapa neno "tafsiri" nina maana ya translation. Mfano maneno kama, excavator katika context ya machinery au equipment; hearse katika context ya vehicle; au digital katika context ya technology.

Kwa maneno yenye tafsiri rasmi, nimekuwa najiuliza zinapatikanaje na mchango wa jamii ni kiasi gani. Mfano mdogo tu, dunia ilipoanza kutumia email kama njia ya mawasiliano, ilinichukua muda mrefu kujua tafsiri yake ni barua pepe. Pia nafikiri tafsiri rasmi ya Artificial Intelligence au AI, ni "Akili Mnemba." Kwa mara nyingine tena swali langu ni je, hizo tafsiri rasmi zimepatikanaje? Wananchi walihusishwa kwa kiasi gani?

Mfano mwingine ambao umenipa maswali mengi hivi karibuni ni wakati nasikiliza taarifa ya Habari ya saa mbili usiku kutoka redio moja maarufu, (bila kuitaja jina) hapa nchini. Katika kuwasilisha Habari kuhusu taifa fulani kugomea mkutano wa UN kwasababu nchi hiyo imewekwa kwenye "Blacklist", mtangazaiji alisema, (sio nukuu ya moja kwa moja), "Nchi X ilitoka nje ya mkutano kwasababu imewekwa kwenye listi nyeusi." Baada ya kusikia hivyo nikajiuliza, Je katika muktadha huo, kusema "Listi nyeusi" ndio tafsiri rasmi ya "Blacklist?"

Baada ya kusikia hivyo, ikaamsha tena chachu yangu ya kujua tunapataje tafsiri rasmi ya maneno magumu ya Kingereza na, ni jinsi gani wananchi wanaweza kujumuika katika kutatua changamoto hiyo.

Baada ya kusema hayo machache, swali langu kwako ni, je, unafikiri lugha yetu ya Kiswahili ina changamoto hiyo? Au wewe binafsi umeshawahi kukumbana nayo katika masomo yako, au kazi zako za kila siku? Kama jibu ni ndiyo, naomba neno moja tu la Kingereza ambalo unafikiri halina tafsiri rasmi. Kwa kufurahisha mjadala huu, ukiweza, pendekeza tafsiri ambayo wewe unafikiri itafaa kwa neno ulilopendekeza.

Kwanini nimeleta ombi hili kwenu? Nia kubwa iliyonifanya nilete ombi hili kwenu ni kwasababu, kwanza binafsi nafikiri hii changamoto ipo. Pili, nafikiri ingekuwa vema kama wananchi nao wangejumuishwa katika utafutaji wa tafsiri rasmi ya menono magumu au mapya ya Kingereza. Tatu, kwa kushirikisha jamii, watajiona nao ni sehemu katika kukuza Kiswahili.

Kwa kumalizia, nimepata muarobaini wa changamoto hii. Muda si mrefu, nataka niweke platform ambayo itakuwa rafiki kwa jamii nzima. Itajumuisha jamii yote ndani na nje ya nchi kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto hii. Itasaidia kufanya watu wafikiri na kupanua mawazo.

Ndani ya siku 7, nitawajulisha jina la platform.

Nashukuru sana. Karibuni sote tujiunge kukuza Kiswahili.
Mimi natamani tujadili neno la mjasiriamali ambalo kwakimombo ni an entrepreneur kiuhalisia kunatofauti kati ya entrepreneurship na Entrepreneurs, entrepreneurship ni elimu inayo muwezesha mjasiriamali kubuni jinsi ya kuanzisha na kupanga jinsi atakavyo ifanya hiyo biashara kwa kutengeneza mpango wake wa biashara kwa kujumuisha jedwali la matumizi na mapato kwa muda wa mwaka mmoja ama zaidi wakati huohuo akiwa anajua biashara zina changamoto hivyo inatakiwa pia apange mikakati ya kukabiliana nazo lakini kumbe an entrepreneur ni ni mtu ambaye anazichangamkia fursa na kuzigeuza kuwa biashara kwa kuifanya hiyo biashara huyu eti akili yake imefungwa kwa maana hafikirii jinsi ya kubuni na kupanga atavyokabiliana na changamoto kwakifupi hana elimu ya ujasiriamali baada ya ufafanuzi huu naomba tujadili kwa kiswahili huyu mjasiriamali ambaye haja bahatika kupata elimu ya ujasiriamali anatakiwa aitweje
 
Shida kubwa ni kulazimisha kila kitu kipya kiwe na jina la kiswahili, matokeo yake ni kubuni vitu vya ajabu na vigumu au visivyo halisi. Mengine tuyatamke hivyo hivyo kama tulivyofanya kwenye Redio, baiskeli, tochi,kamisheni, n.k
Mfano kuna haja gani ya kuhangaika kubuni vitu kama
1. Flush disk eti_ disiki mweko
2. Computer.....
3. TV.....Runinga
Manene mengine yaingizwe kama yalivyo
Kuna mbwembe nyingine kama
1. Maji tiririka.. Hapa ni kama unayaamuru maji, kwa nini tusitumie --Maji yanayotiririka
2. Taasisi nunuzi (Procuring Entity) Kwa nini isiitwe Taasisi inayonunua?
 
Kiswahili ni lugha ya kuunga unga sana sijui kwanini tunaikumbatia
Yah! Ukiona neno moja la lugha nyingine linatafsiriwa kwa mtiririko wa maneno ili lieleweke hiyo lugha (inayotafsiri) bado sana.

In short Kiswahili is too verbose; you need a number of words to translate a single word from other languages.
 
Nashukuru kwa mchango wako. Je unaweza kusema "Orodha nyeusi" ndio tafsiri rasmi ya "Blacklist?" katika muktadha wa "Mwenye/wenye sifa mbaya iliyopitiliza?"
Labda kuwekewa vikwazo
 
Tafsiri zipo nyingi tu na hata maneno yaliyotoholewa yametafutiwa tafsiri...

Niliwahi kumsikia jamaa mmoja anaongea baadhi ya maneno.
Bora tuendelee na swanglish
 
Serendipity

Hili ni neno linalomaanisha ugunduzi wa kitu kizuri bila kukitafuta, au bahati nzuri isiyotarajiwa inayokuja kwa namna isiyo ya moja kwa moja.

Kiswahili hakina neno moja linalobeba maana hiyo kwa usahihi, hivyo mara nyingi linabaki kama lilivyo au linafafanuliwa kwa sentensi.

Ova
 
Lugha huzaliwa,hukua ,huishi,Kisha hufa.
Lugha ya Swahili hukua Kwa njia mblmbl 1.maendeleo ya tekinolojia.
2.kutohoa ktk lugha za kigeni ktk nyanja za kisiasa,kiuchumi,kielimu nk.
Hata wazungu nao wameamua kubaki na neno ,"UGALI" PASIPO KULITAFSILI KTK LUGHA YA KIINGEREZA.
 
Back
Top Bottom