Naomba nieleweshwe kwenye ukristo! Kwahiyo akikaribia kufa na akaomba sala ya toba haendi motoni?

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
 
Nukuu!
********
36. Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki

37. wakisema: “Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”

38. Vilevile maandishi haya yalikuwa yamewekwa juu yake: “Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.”

39. Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: “Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia.”

40. Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: “Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.

41. Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”

42. Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.”

43. Yesu akamjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.”

***********
End of quote
 
mkuu Nesi mkunga mbona kama heading na content zimepishana kidogo heading inauliza kama akaomba sala ya toba alafu content inauliza kama ataombewa sala ya toba
 
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
Vitendo vyako vyema ndivyo vitakavyo kuingiza wewe peponi sio sala ya toba na haswa ukiwa mkristo usitegemee kama utaingia peponi kwa sala ya toba sio rahisi kabisa. Ukitaka kuingia peponi Kuwa Muislam na fanya vitendo vizuri utaingia peponi.
 
Kufanya matendo mazuri ili tu kuokoka ni sawa na kujiokoa mwenyewe.

Mwanadamu hawezi kujiokoa mwenyewe.

Unadai kwamba matendo mema ndiyo yatamwingiza mtu peponi na wala si sala ya toba.

Kumbe sala ya toba si hidaya njema?

Tuna safari ndefu sana kama taifa la kiroho.
 
Sisi tunapiga propaganda hatujawahi kufa ila kifo ni usingizi wa milele yaan hauta hamka tena thats kifo
 
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
Kinachompeleka mtu mbinguni ni utakatifu, kwa mtu mwenye dhambi kinachomwokoa akiwa hapa duniani ni toba ya kweli bila kujali ametubu wakati gani. Hawezi mtu kujitengenezea utakatifu hata kama ni mtenda mema sana, matendo mema yanakuja kama matokeo ya toba ya kweli ambayo ni kumwamini Yesu na kuamua kuokoka.

Lakini pia hata mtu awe na mzigo wa dhambi kiasi gani bado anaweza kusamehewa, kwa sababu deni lake la dhambi lilishalipiwa na Yesu aliyempokea.
 
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
TUMIA AKILI DAUDI NA MUSA WALIUA SANA WALA AWAKUOMBA TOBA. KUUA SIYO DHAMBI BALI DHAMBI NI KUUA DAMU ISIYO NA HATIA .
MFALME SAULI ALIACHA KUUA MUOVU MUNGU AKAMKATAA ...

HIVYO KUNA ...

1)KUUA KUTAKATIFU NA KUNA KUUA KWA DHAMBI.
2)UPO UPOLE MTAKATIFU NA UPO UPOLE WA DHAMBI..
3)UPO WEMA MTAKATIFU NA UPO WEMA WA DHAMBI.
4)IPO TOBA TAKATIFU NA IPO TOBA ILETAYO DHAMBI
5)IPO SADAKA TAKATIFU NA IPO SADAKA ISIYO TAKATIFU
6)UPO UPOLE MTAKATIFU NA UPO UPOLE WA DHAMBI.
7)KIPO KIBURI KITAKATIFU NA KIPO KIBURI CHA DHAMBI
8)IPO IBADA TAKATIFU NA IPO IBADA ILETAYO DHAMBI
9)WAPO MITUME NA MANABII WATAKATIFU NA WAPO WA DHAMBI(FEKI)
10)IPO INJILI TAKATIFU NA IPO INJILI YA DHAMBI.
.
NK
 
Kufanya matendo mazuri ili tu kuokoka ni sawa na kujiokoa mwenyewe.

Mwanadamu hawezi kujiokoa mwenyewe.

Unadai kwamba matendo mema ndiyo yatamwingiza mtu peponi na wala si sala ya toba.

Kumbe sala ya toba si hidaya njema?

Tuna safari ndefu sana kama taifa la kiroho.
Sala ya Toba haito kusaidai kitu Vitendo vyako vyema ulivyokuw aupo hai ndivyo vitakavyoweza kukuingiza peponi.Sio eti uwe mzinifu,muuwaji, ,mbadhirifu, jambazi, Mlevi mtu unaye dhulumu haki za watu na mchawi eti ukifa uombee na mchungaji au Baba Askofu sala ya toba Mungu akuingize peponi usio rahisi kabisa umemfanya huyo Mungu mjomba wako nini? Akuingize katika pepo yake kwa sala ya Toba ya kuombea na Baba Askofu au Wachungaji? mMunaongopewa sana na Viongozi wenu Makanisani.Hebu wajaribuni kuwauliza mswali na wakupeni uhakika sio kuwaongopea waumini eti ukiombewa Sala ya toba utaingia peponi sio rahisi kabisa.
 
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
Yesu Kristu alishalipa Dhambi zote kwa Wanadamu wote mpaka yule wa mwisho kuzaliwa katika Dunia hii! Kabla ya Siku ya Mwisho .Siku ile atakayerudi Simba wa Yuda kutoa hukumu ya haki.... Siku ambayo ( Dan 12:2-3 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao we | Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV) | Pakua Programu ya Biblia Sasa) Ajalishi Umetubu na kumwamini Muda gani.... Ata kama una dhambi kama Adolf Hitler mlango wa Mungu upo wazi Bado Karibu Mbinguni .https://www.bible.com/sw/bible/164/ISA.1.18.SUV:
 
Sala ya Toba haito kusaidai kitu Vitendo vyako vyema ulivyokuw aupo hai ndivyo vitakavyoweza kukuingiza peponi.Sio eti uwe mzinifu,muuwaji, ,mbadhirifu, jambazi, Mlevi mtu unaye dhulumu haki za watu na mchawi eti ukifa uombee na mchungaji au Baba Askofu sala ya toba Mungu akuingize peponi usio rahisi kabisa umemfanya huyo Mungu mjomba wako nini? Akuingize katika pepo yake kwa sala ya Toba ya kuombea na Baba Askofu au Wachungaji? mMunaongopewa sana na Viongozi wenu Makanisani.Hebu wajaribuni kuwauliza mswali na wakupeni uhakika sio kuwaongopea waumini eti ukiombewa Sala ya toba utaingia peponi sio rahisi kabisa.
Mungu aliona Dhambi zote zitakazofanywa na Binadamu wote aliowaumba Duniani! Damu ya Yesu imefuta Dhambi zote kwa atakaeamini na kutubu Dhambi zake , ajalishi ni muda gani!! Sali kabla ujaswaliwa
 
Vitendo vyako vyema ndivyo vitakavyo kuingiza wewe peponi sio sala ya toba na haswa ukiwa mkristo usitegemee kama utaingia peponi kwa sala ya toba sio rahisi kabisa. Ukitaka kuingia peponi Kuwa Muislam na fanya vitendo vizuri utaingia peponi.
NAKAZIA HAPA..
Nakumbuka nilisoma mahala kwenye kitabu cha ayubu nimesahau sura, but last minute decisions wont matter...
 
Naomba nieleweshwe kabisa maana leo wakati nipo na washikaji tunapiga story nikaambiwa na hawa watu wakristo ya kwamba hata kama mtu amefanya mabaya sana kama vile amefanya mauaji kama yale ya akina ben saa nane,azory gwanda na akwalina au yale mauaji ya zanzibar akiombewa kwa sala ya toba eti haendi motoni eti kisa ameaaidiwa sala ya toba nikashituka how and why?

Naomba mnieleweshe wakuu how and why?!!!!!!!!!!!!! Naombeni majibu
Mungu anajua mioyo yetu na anafahamu fikra zetu na mipango yetu kabla ya sisi kuiweka wazi

Anaijua mwisho kabla hata ya mwanzo, hivyo suala la toba inaendana na kukiri ya kuwa yeye ndie muweza wa yote hivyo shukrani, sifa na utukufu ni kwake pekee

Lakini je wewe ambae unaomba toba sasa ukiwa katika nyakati za mwisho katika maisha yako hukuisikia kweli?? Au uliisikia na ukaipuuzia???

Na unaotubu sababu umejua ya kuwa kuna Mungu anaepaswa kuabudiwa au kwa sababu umeambiwa ya kuwa hatua uliyofikia huwezi kupona kamwe?

Hayo yote anaejua ni yeye na ndio maana kuna hukumu kwa wema na waovu na kila mmoja atavuna alichopanda
 
Back
Top Bottom