Naomba nieleweshwe kwenye ukristo! Kwahiyo akikaribia kufa na akaomba sala ya toba haendi motoni?

Naomba nieleweshwe kwenye ukristo! Kwahiyo akikaribia kufa na akaomba sala ya toba haendi motoni?

Mungu aliona Dhambi zote zitakazofanywa na Binadamu wote aliowaumba Duniani! Damu ya Yesu imefuta Dhambi zote kwa atakaeamini na kutubu Dhambi zake , ajalishi ni muda gani!! Sali kabla ujaswaliwa
Damu ya Yesu haiwezi kufuta dhambi ya binadamu unajidanganya Yesu mwenyewe alimuomba Mungu amuepushe na kifo cha Msalaba. Iweje Damu yake iweze kukusaidai wewe mwenye dhambi? Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe utavuna kile ulicho kipanda usijidanganye ukaona Damu ya Yesu itakuokoa na adhabu ya moto wa Jahanamu sio rahisi. Ninakataa kabisa. Tenda mema duniani kabla ya hujafa ili utakapo kufa upate kulipwa mema yako acha kufanya madhambi na mabaya saidia masikini wagonjwa, mayatima,Wasiojiweza , watendee wema wazazi wako sali sana kama ni mfanya biashara toa kila mwaka fungu lako la 10 Utakacho kipanda ndicho utakacho kivuna.
 
Hiyo sala ni Moja ya mbinu ya ugaidi inayotumia na wanamaombi Kwa kumsalia sala ya Toba kama vile wao ni madaktari na wamesha mpima kuwa Sasa ndiyo mwisho wa uhai wako na ni lazima ufe. Kitendo hichi kinamtia hofu mgonjwa na kumuongezea pressure ambayo lazima immalize tu.
 
Damu ya Yesu haiwezi kufuta dhambi ya binadamu unajidanganya Yesu mwenyewe alimuomba Mungu amuepushe na kifo cha Msalaba. Iweje Damu yake iweze kukusaidai wewe mwenye dhambi? Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe utavuna kile ulicho kipanda usijidanganye ukaona Damu ya Yesu itakuokoa na adhabu ya moto wa Jahanamu sio rahisi. Ninakataa kabisa. Tenda mema duniani kabla ya hujafa ili utakapo kufa upate kulipwa mema yako acha kufanya madhambi na mabaya saidia masikini wagonjwa, mayatima,Wasiojiweza , watendee wema wazazi wako sali sana kama ni mfanya biashara toa kila mwaka fungu lako la 10 Utakacho kipanda ndicho utakacho kivuna.
 
Nukuu!
********
36. Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki

37. wakisema: “Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”

38. Vilevile maandishi haya yalikuwa yamewekwa juu yake: “Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.”

39. Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: “Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia.”

40. Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: “Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.

41. Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”

42. Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.”

43. Yesu akamjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.”

***********
End of quote
Maneno haya umeyatoa injili ipo? Matayo, Luka, Marko au Yohana?!
 
Mbingu haijawahi kuwepo haipo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Motoni hakupo na hakujawahi kuwepo.

Mungu na Shetani hawajawahi kuwepo, hawapo na hata uwezekano wa kuwepo kwao haupo.

Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu.
 
Dini ni utapeli .. Kuna wengi walikuwa wanauza Coupon za kusamehewa dhambi.
 
Back
Top Bottom