Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Naomba nijibiwe maswali yangu kuhusu huu mtaala mpya wa elimu.
Jedwali na.4: Somo, umahiri mkuu na umahiri mahususi kwa darasa la iii hadi la vi.
Kipengele na:
8. Elimu ya Dini Itatolewa na viongozi wa dini inayohusika kwa kuzingatia mwongozo utakaotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
. Hili somo la dini litahusisha mafunzo ya dini gani kwa wanafunzi ?
. Utaratibu gani utatumika kwa wanafunzi wasio na dini kuto kushiriki mafunzo hayo kwa kuzingatia uhuru wao kama ulivyo elezwa na katiba ya jamhuri ya muungano ?
. Uandikishaji wa kipengele hiki ulizangatia matakwa ya katiba ya jamhuri ya muungano ?
Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1992 Na.4 ib… 19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.