Naomba nitoe ushauri huu kwa serikali kuhusu wasanii wa Tanzania.

Naomba nitoe ushauri huu kwa serikali kuhusu wasanii wa Tanzania.

Manfried

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2024
Posts
1,288
Reaction score
4,074
Please Moderator msiunganishe huu uzi maana mtakuwa mmefeli big time.

First of all naipongeza serikali Kwa kufikiria wazo la kuwasaidia wasanii kuhusu kutibiwa magonjwa ya moyo


Hili wazo sio baya Ila napendekeza mjaribu kuliboresha kwa kuhakikisha wasanii wote ambao wanajihusisha na sanaa ikiwemo Musicians, dancers , watu wa boxing , wachezaji mpira , actors and actress n.k

Kabla MTU ajaingia katika moja ya kazi hapo juu . kinabidi kiwepo chombo, taasisi au mfumo wa kuwasimamia hao watu

Kwanini uwepo mfumo wa kuwasimamia , kwakuwa pamoja na kwamba wana vipaji na talanta kubwa bado asilimia kubwa hawajitambui na hawana akili ya kuwaza mbele kuhusu kesho yao.

Hivyo MTU yeyote akitaka kuanza hizi Kazi anabidi kusajiliwa maeneo matatu muhimu

Katika insurance (BIMA)
Katika Usimamizi wa Kazi zake na haki za msingi .
Katika bank maalumu .

Katika Bima msanii -atakuwa kila anapofanya show yoyote lazima ikatwe hela itakayoelekezwa katika bima mfano umefanya show au onesho fulani unakatwa 10% ya malipo yako yanaingizwa moja Kwa moja Kwa ajili ya BIMA -hii bima itakuwa Ina-cover pale msanii akiumwa au akipata majanga yoyote .

Kuhusu usimamizi wa Kazi zake - msaniii kila Kazi atakayohusika lazima aendelee kunufaika nayo milele haijalishi ameiuza au hajaiuza , mfano Kanumba Leo mama yake ni masikini aliyetukuka huku Kazi za mwanae zinaendelea kuuzwa na watu wanapiga hela, hivyo endapo ukiuza Kazi yako inabidi kuwepo asilimia Fulani unapokea kupitia mauzo ya kazi zako. MTU Kama Steve Nyerere hadi anageuka chawa ni kutokana na kutokuwepo na huo mfumo

Mfano unauza filamu million 100 inabidi katika hio contract ubaki na agreements inayosema nitalipwa million 100 Ila kila Kazi yangu ikioneshwa katika sehemu mbalimbali Kama YouTube , Netflix n.k nitaendelea kupokea asilimia labda 20 ya mauzo na nikiyemuuzia atapokea asilimia 80

Hii itafanya wanaojiita bongo movie wasiwe malaya wakutupwa na wanaume kuwa makuhadi wa soko huria.


Na kuhusu Bank- msanii kila anapofanya Kazi anabidi kukatwa hela na hiyo inaingia bank na ikifika bank inaingizwa katika mfuko wa mafao ya msanii moja kwa moja .


Naomba kuwasilisha haya maboresho

Mh Mwana FA utapitia hapa na Asante yangu utanitumia PM
 
Waziri wa sanaa na michezo ukifanya hivi utakuwa umefanya jambo ambalo litakufanya jina lako likumbukwe na kuandikwa katika mioyo ya wasanii daima.

Ebu fikiria Maisha wanayoishi wasanii waliopata majina makubwa

Mfano Ferooz , Daz Baba wamefika huku kote na kuwa depressed Kwa kukosa mifumo na muongozo sahii
 
Back
Top Bottom