Naomba nondo kuhusu gari aina ya Subaru Forester XT


Mimi ninayo ya cc 2456 +turbo charged speed 240 ph
 
Acha nitoe ushuhuda kidogo kwani ninamiliki Subaru xt ya 2010 yenye cc 2456 + turbo charged Ej 25, speed 240 ph, ni bonge la Gari, nainjoy sana, ina nguvu ni hatari,ila inahitaji care sana pia spare ni ghali ukilinganisha na Gari nyingi, barabarani inatulia sana haiyumbi hata kidogo, si bravis, crown, alfard au kluger anaeweza kufata Gari hii, ila inahitaji umakini mkubwa sana kwani ni nyepesi sana kuchangana.
 
off road perfomance ikoje maana hiyo ni class ya SUV.
kulinganisha na subaru 2006.
 
Mjeruman uyo msikariri gari ni mileage bossy ndomana mnapigwa. Gari yenye above 100k hzi nyingi zimepigwa service ya maana kiwandan
Ninachosema ni kwamba,

Kununua gari yenye mileage above 100k ni sawa na ununue scraper. Majority ya parts zinakuwa zimechoka na ni ngumu kubadilisha zote huo ni uongo. Unachooneshwa ni rangi mpya ila huko chini kumeanza kuoza. Baada ya km 30k utaanza kulia kubadilisha parts.

Kuna gari zina mileage ndogo na service zinapata kwa wakati. Hata baadhi ya areas zinakuwa hazijachoka. Na kuna watu wengi wanauza magari yenye mileage ndogo bila utapeli. Wakati unaweza enda zaidi ya 100k bila major overhaul.
 
Naunga mkono hoja... natumia vw polo ni gari bora kabisa... asijiulize mara mbili...achukue hio gari halaf atakuja kushukuru later

Mkuu mutu murefu , share nasi experience yako kuhusu VW Polo. Ni gari nayoiwaza sana kuimiliki in near future.

Watu wengi wanasema kuwa gari za mjerumani ni pasua kichwa, hasa kwenye maintenance. Hili lipoje?
 
Wengi wanasema hvo wanasema bora marcedes
Champagnee, kila mtu na gari lake ndio maana nikakwambie Subaru bado ipo mbali na mm na kwa maintanance kuna gari inamaliza miaka 50 bila block au cyilinder head kubadilishwa
Mbaula ya mwaka 1968 mpaka leo ipo barabarani,
Your browser is not able to display this video.

F I A T naona wengi hawakuwa wamezaliwa, sikiliza gia zinavyobadilishwa sio hizi za kwetu kila mwanamke anaendesha
hapo lazima ubebe galoni la maji na diesel pia
 
Sio kweli. Nina GX100 imeacha kusoma (speedometer imekufa) at 200k+ huko Hadi leo mashine jino moja tu inaitika naipaki bila kuigusa hata mwezi mzima,nilikuwa na Volvo nimeikata spares at 160k+ miles ambazo ni kama 260km sasa hivi nina Toyota nimeinunua from Japan ina 145,000km Hadi leo ina 151,000km tangu niinunue ni miezi 6 nasafiri nayo na huko njiani hakuna rangi wanaacha ona!
Nawaambia hivi usiogope km hizo ni namba tu gari body sio engine kama huamini jiulize kwanini engine ilala zinauzwa 1-2m kama gari ingekuwa engine? Sasa nenda katafute gari iliokufa engine kama utauziwa 1-2m.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…