Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Habari waungwana,

Kama mada inavyoonekana hapo juu naomba mwenye kujua suluhisho la kuondoa kitambi anisaidie, nilijifungua kwa operation mwaka jana 11 na sikufunga tumbo sasa badala ya kuendelea kupungua ndo kwanza tumbo linazidi kukua nakosa raha jamani hasa ukitaka kuvunja kabati nguo zinagoma!

Msaada please
Dada yangu walitumia Detox,
Kunywa asububi na jioni,,hii inaambatana na kupunguza quantity ya chakula.

Ndani ya mwezi hadi miezi miwili utaona matokeo mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna njia ya mkato.
Jitahidi kuuchosha mwili kwa zoez la kutembea chapchap hata 1km mida ya jion. Jitahidi kutenga hata siku mbili kwa juma moja.

Ukizoea utashangaa unafika 2km.
Ila matokeo yake yanakuja taratibu.

Ukiwa serious baada ya miez utaanza kuona mwili mwepesi.kupungua mwili mzima sio kitambi tu.

Kula we kula tu
Narudia tena kula

Ila mazoezi yawe sehem ya maisha yako yote

Kama ni mwajiriwa jitahidi jion pale au weekend.

Ukiwa na muendelezo mzuri
Hatimaye utabadili tabia na kuwa mazoea
Asante mkuu kwa maelekezo
 
Habari waungwana,

Kama mada inavyoonekana hapo juu naomba mwenye kujua suluhisho la kuondoa kitambi anisaidie, nilijifungua kwa operation mwaka jana 11 na sikufunga tumbo sasa badala ya kuendelea kupungua ndo kwanza tumbo linazidi kukua nakosa raha jamani hasa ukitaka kuvunja kabati nguo zinagoma!

Msaada please
Nenda Instagram mcheki Dr Boaz mkumbo MD
 
Thanks,but kibongo bongo Kula proteni ni ishu sababu ya uchumi unakuta vyakula tajwa visivyo ruhusiwa ndo vipo kwa urahisi
Unatafuta excuses sana hii itakuletea shida..

Google mboga za majani zenye protein kwa wingi kama nyama samaki na maharage ni ghali..

Maana vegetarian, source yao ya protein wanaipata kwenye mboga mboga pia...

Unapaswa kula healthy fat na protein kwa wingi..

Usile wanga / labda low carbs mara chache chache sana!!

Acha kabisa carbonated drinks kama Pepsi Big..nk

Fanya mazoezi hata kutembea pia ni mazoezi...

Kuna raia kila mahali ni kuzurula na boda boda tu hata kwenda sokoni umbali wa kawaida tu!!

Mwili wako utajengwa kutokana na lifestyle yako!!!

Anza leo taratibu na Matokeo utayaona!, hakuna shortcuts au solution ya muda mfupi /ambazo zinaweza kukuletea madhara!!
 
Nashukuru sana
 
Speaking from a 1 year experience ya kupunguza kitambi na kujenga misuli, Dawa kama dawa ya kupunguza kitambi hakuna, zipo njia kuu 2 rahisi
1. (a) kupunguza kula vyakula vyenye calories nyingi (carbohydrates & fats/oil) mfano soda, keki, ugali/wali, beer, chips, vyakula vya kukaanga n.k
(b)kula sana vyakula vyenye calories chache. Mfano mboga mboga, matunda, nyama choma, kuku, samaki n.k. Kwa kifupi kufanya diet.
2. Fanya mazoezi. Sio lazima uende gym unaweza tu ukawa unatembea, jogging, kwenye majengo badala ya kupanda lift ukawa unatumia ngazi, ila kama nafasi unayo sio vibaya ukaenda gym. Mazoezi yanasaidia kuchoma calories mwilini.

Muhimu:
1). Calories ni kipimo cha nguvu iliyopo kwenye chakula. Kuna vyakula vina nguvu nyingi mfano ugali au wali. So unapokula mwili unatumia calories unazoihitaji TU zile zinazobaki zinahifadhiwa kama Fats na kwa case yako ni kitambi.

2). Ili kupungua ni lazima uupe mwili calories chache kuliko unazohitaji ILI lile gap liweze kulipwa na zile calories ambazo mwili umezihifadhi. Kwa mfano mwili unahitaji calories 2500 wewe unakula chakula chenye calories 2000, kwahiyo calories 500 zitatoka kwenye hazina ya mwili. Ukifanya hivi kwa muda mrefu utapungua

3). Huwezi kulenga kupunguza kitambi pekee, utakapoanza kupungua utapungua mwili mzima. Namaanisha kwamba, kutoka point ya (2) hapo juu, hizo calories 500 hauwezi kuamua zitoke kwenye kitambi, mikono au sehemu nyingine yoyote. Zinazotoka kwenye mwili mzima sio tu sehemu moja.

4). Dawa zinazotangazwa kuwa zinapunguza kitambi na kwamba ukizinywa unaenda kuharisha mafuta sio za kweli. Kitu ambacho zinafanya ni kuuzuia mwili wako usimeng'enye vizuri chakula kwa maana hiyo nguvu/calories nyingi kwenye chakula unachokula zinaishia chooni. Kwa mtindo huo, ni kweli utapungua ila afya itakongoroka kwa sababu mwili utakua haupati virutubisho badala yake unavitoa karibia vyote.

5). Kupunguza kitambi inachukua muda kwahiyo Usijiwekee matarajio ya muda mfupi. Ukikaza kwenye diet na ukafanya mazoezi matokeo yatakuja TU.

Update:
Hii ilikua ni ushauri kwa mwanaume aliyekuwa anataka kupunguza kitambi kwa kutumia dawa. Ila hata Kwa case ya tumbo la uzazi, maelezo yana apply pia. Kwa kuongezea tu fanya pia abs workouts kwa lugha rahisi mazoezi ya kujenga na kukaza misuli ya tumbo, ni muhimu.

Lastly, it takes a lot of time Usikate tamaa.
 
Back
Top Bottom