Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Speaking from a 1 year experience ya kupunguza kitambi na kujenga misuli, Dawa kama dawa ya kupunguza kitambi hakuna, zipo njia kuu 2 rahisi
1. (a) kupunguza kula vyakula vyenye calories nyingi (carbohydrates & fats/oil) mfano soda, keki, ugali/wali, beer, chips, vyakula vya kukaanga n.k
(b)kula sana vyakula vyenye calories chache. Mfano mboga mboga, matunda, nyama choma, kuku, samaki n.k. Kwa kifupi kufanya diet.
2. Fanya mazoezi. Sio lazima uende gym unaweza tu ukawa unatembea, jogging, kwenye majengo badala ya kupanda lift ukawa unatumia ngazi, ila kama nafasi unayo sio vibaya ukaenda gym. Mazoezi yanasaidia kuchoma calories mwilini.

Muhimu:
1). Calories ni kipimo cha nguvu iliyopo kwenye chakula. Kuna vyakula vina nguvu nyingi mfano ugali au wali. So unapokula mwili unatumia calories unazoihitaji TU zile zinazobaki zinahifadhiwa kama Fats na kwa case yako ni kitambi.

2). Ili kupungua ni lazima uupe mwili calories chache kuliko unazohitaji ILI lile gap liweze kulipwa na zile calories ambazo mwili umezihifadhi. Kwa mfano mwili unahitaji calories 2500 wewe unakula chakula chenye calories 2000, kwahiyo calories 500 zitatoka kwenye hazina ya mwili. Ukifanya hivi kwa muda mrefu utapungua

3). Huwezi kulenga kupunguza kitambi pekee, utakapoanza kupungua utapungua mwili mzima. Namaanisha kwamba, kutoka point ya (2) hapo juu, hizo calories 500 hauwezi kuamua zitoke kwenye kitambi, mikono au sehemu nyingine yoyote. Zinazotoka kwenye mwili mzima sio tu sehemu moja.

4). Dawa zinazotangazwa kuwa zinapunguza kitambi na kwamba ukizinywa unaenda kuharisha mafuta sio za kweli. Kitu ambacho zinafanya ni kuuzuia mwili wako usimeng'enye vizuri chakula kwa maana hiyo nguvu/calories nyingi kwenye chakula unachokula zinaishia chooni. Kwa mtindo huo, ni kweli utapungua ila afya itakongoroka kwa sababu mwili utakua haupati virutubisho badala yake unavitoa karibia vyote.

5). Kupunguza kitambi inachukua muda kwahiyo Usijiwekee matarajio ya muda mfupi. Ukikaza kwenye diet na ukafanya mazoezi matokeo yatakuja TU.

Update:
Hii ilikua ni ushauri kwa mwanaume aliyekuwa anataka kupunguza kitambi kwa kutumia dawa. Ila hata Kwa case ya tumbo la uzazi, maelezo yana apply pia. Kwa kuongezea tu fanya pia abs workouts kwa lugha rahisi mazoezi ya kujenga na kukaza misuli ya tumbo, ni muhimu.

Lastly, it takes a lot of time Usikate tamaa.
Point no.4 nimekuelewa sana. Kuna dawa inaitwa C9 inauzwa laki nne ndio kazi yake hiyo.
 
Asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom