Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole,naumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,
Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.
Mnisaidie
Hakuna ugonjwa wa kichwa. Kuumwa kichwa ni dalili ya tatizo fulani mwilini. Kumeza painkillers unatibu dalili tu. Nenda hospitali wakuchunguze sababu ya kichwa kuuma ili utibiwe kwa usahihi.naumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,
Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.
Mnisaidie
Nakupata vilivyoPole,
Kuna mambo mengi ya kuchakata ili kufikia mwafaka wa tatizo la msingi:
1: Umri
2: Jinsi
3: Kichwa huuma sehemu ipi
4: Jinsi kinavyouma
5: Una muda gani kikiwa kinauma
6: Uhusiano wa maumivu ya kichwa kwenye familia
7: Ukifanya nini kichwa huuma zaidi.
8: Nini hufanya maumivu kupungua
9: Jinsi/italeta mahusiano na upataji wa siku vs matumizi ya uzazi wa mpango.
10: Mahusiano ya maumivu vs ukikaa au kusimama au kulala.
11. Mahusiano ya maumivu ya kichwa na kelele, safari za mkoa mmoja mpaka mwingine, mwanga mkali, njaa, usingizi nk.
12: Vitals: BP na dalili nyingine zitakazohusishwa pia.
NB: Hapa kuna haja ya kuwaona wataalamu wa afya ili kudadavua haya na mengineyo ili kufikia mwafaka.
Unaweza kuanza na daktari wa kawaida/GP au daktari bingwa wa magonjwa ya ndani/physician kulingana na ulipo.Nakupata vilivyo
Je tatizo kama hili yatupasa kumuona mtaalamu wa nini? Macho,mishipa, mifupa au nn
Mimi nipo Arusha je daktari wa magonjwa ya ndani anspatikana hospitali gani ?Unaweza kuanza na daktari wa kawaida/GP au daktari bingwa wa magonjwa ya ndani/physician kulingana na ulipo.
Jaribu kupima pia kansa unaweza ukawa una uvimbe kichwaniNaumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,
Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.
Mnisaidie
1: Selian/AICC/Mount Meru/NSK/HospitalsMimi nipo Arusha je daktari wa magonjwa ya ndani anspatikana hospitali gani ?
Nilikuwa na wazo la kwenda kupiga CT scan ili nijue Nina tatizo wapi na kisababishi ili nishauriwe tiba au iekaaje hiyo
Asante sana ndugu nitaenda hospital na niwaelezee ninavyojisikia1: Selian/AICC/Mount Meru/NSK/Hospitals
2: Si jambo jema kwenda kwenye vipimo bila kuwa na nini kinaweza kuwa sababu au nini hasa kinaenda kuangaliwa kulingana na dalili.
Vipimo huja/huagizwa baada ya wazo la nini kinasumbua. Unaweza kufanya kipimo kikubwa na kuishia kwenye frustration. Kuna vitu vinaitwa incidental findings, lakini unakuta hakihusiani na tatizo lako la msingi au kila kitu kikakutwa kiko sawa nawe unaumwa lakini kwa uchaguzi wa kipimo ulitegemea ndo majibu yatapatikana kumbe hata kipimo hakihusiani kabisa na tatizo.
Hivyo, sikilizwa vyema kuwe na mwelekeo wa tatizo kwanza.
Au wewe una USHAURI mwingine kuhusu matatizo yetu Mimi na mleta mada?1: Selian/AICC/Mount Meru/NSK/Hospitals
2: Si jambo jema kwenda kwenye vipimo bila kuwa na nini kinaweza kuwa sababu au nini hasa kinaenda kuangaliwa kulingana na dalili.
Vipimo huja/huagizwa baada ya wazo la nini kinasumbua. Unaweza kufanya kipimo kikubwa na kuishia kwenye frustration. Kuna vitu vinaitwa incidental findings, lakini unakuta hakihusiani na tatizo lako la msingi au kila kitu kikakutwa kiko sawa nawe unaumwa lakini kwa uchaguzi wa kipimo ulitegemea ndo majibu yatapatikana kumbe hata kipimo hakihusiani kabisa na tatizo.
Hivyo, sikilizwa vyema kuwe na mwelekeo wa tatizo kwanza.
Ushauri wangu binafsi ni:Au wewe una USHAURI mwingine kuhusu matatizo yetu Mimi na mleta mada?
Kama una USHAURI
Tafadhali mtaalamu naomba utupe nitaupokea kwa mikono miwili!
Pia ushauri kuhusu maelezo ya mwanzo pindi tu nitakapofika hospili ni hatua gani muhimu nitaanza nazo
Natanguliza shukurani
Asante sana mkuuUshauri wangu binafsi ni:
1: Kufika hospitali na kumwona mtoa huduma ya afya/daktari.
2: Andaa maelezo mapema kufuatana na tatizo lako kwa historia, pia ukifuatilia msg #6 utakuwa na mwanga kidogo.
3: Mpe maelezo mtoa huduma ya afya kadri uwezavyo na anavyokuuliza.
4: Amini, maelezo yako ndo mwanzo wa tiba. Toa maelezo kwa kadri unavyojifahamu, usijibu kile ambacho haujakielewa au kumaliza tu consultation.
5: Uliza pale ambapo ulichoulizwa au kuelezwa hakijaeleweka.
6: Tiba yako haitokani na jina kubwa la taasisi husika bali mtoa huduma uliyekutana naye kwa matibabu atakayokupa au maelekezo ya nini ufanye kama liko juu ya uwezo wake.
NB: Kwa mtoa huduma rafiki sana huweza kukupa ni nini majumuisho/summary ya alichokipata kwako kutokana na maongezi yenu na examination na anaomba ufanye vipimo gani na kwa nini?