Naomba tiba ya chronic headache

Naomba tiba ya chronic headache

Mumlii

Senior Member
Joined
Mar 14, 2021
Posts
169
Reaction score
232
Naumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,

Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.

Mnisaidie
 
Pima macho yawezekana ndo yanasababisha kichwa kuuma
 
Kinaumaje? Kinauma chote kama umevaa rubber band ikakubana au ni sehemu moja ya kichwa ndo inauma sana?
 
naumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,

Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.

Mnisaidie
Pole,
Kuna mambo mengi ya kuchakata ili kufikia mwafaka wa tatizo la msingi:
1: Umri
2: Jinsi
3: Kichwa huuma sehemu ipi
4: Jinsi kinavyouma
5: Una muda gani kikiwa kinauma
6: Uhusiano wa maumivu ya kichwa kwenye familia
7: Ukifanya nini kichwa huuma zaidi.
8: Nini hufanya maumivu kupungua
9: Jinsi/italeta mahusiano na upataji wa siku vs matumizi ya uzazi wa mpango.
10: Mahusiano ya maumivu vs ukikaa au kusimama au kulala.
11. Mahusiano ya maumivu ya kichwa na kelele, safari za mkoa mmoja mpaka mwingine, mwanga mkali, njaa, usingizi nk.
12: Vitals: BP na dalili nyingine zitakazohusishwa pia.

NB: Hapa kuna haja ya kuwaona wataalamu wa afya ili kudadavua haya na mengineyo ili kufikia mwafaka.
 
Hakuna ugonjwa wa kichwa. Kuumwa kichwa ni dalili ya tatizo fulani mwilini. Kumeza painkillers unatibu dalili tu. Nenda hospitali wakuchunguze sababu ya kichwa kuuma ili utibiwe kwa usahihi.
 
inaweza kuwa kupungukiwa damu au damu imezidi lakini pia inaweza kuwa migraine ambayo kwa pain killer za kawaida inakuwa ngumu kutibika.. tafuta dawa inaitwa VASOGRAIN
 
Ukweli hata mimi naumwa kichwa sana
Nimekuwa ni mtu wa kumeza hedex kila kikiuma
Na Sasa kimebadili mtindo wa maumivu
Kuna muda nasikia mchakacho ndan ya kichwa
Nahisi sauti kama mgurumo fulan wa tumbo la njaa au mgusanisho wa waya ndan ya kichwa shida ni nini?
 
Pole,
Kuna mambo mengi ya kuchakata ili kufikia mwafaka wa tatizo la msingi:
1: Umri
2: Jinsi
3: Kichwa huuma sehemu ipi
4: Jinsi kinavyouma
5: Una muda gani kikiwa kinauma
6: Uhusiano wa maumivu ya kichwa kwenye familia
7: Ukifanya nini kichwa huuma zaidi.
8: Nini hufanya maumivu kupungua
9: Jinsi/italeta mahusiano na upataji wa siku vs matumizi ya uzazi wa mpango.
10: Mahusiano ya maumivu vs ukikaa au kusimama au kulala.
11. Mahusiano ya maumivu ya kichwa na kelele, safari za mkoa mmoja mpaka mwingine, mwanga mkali, njaa, usingizi nk.
12: Vitals: BP na dalili nyingine zitakazohusishwa pia.

NB: Hapa kuna haja ya kuwaona wataalamu wa afya ili kudadavua haya na mengineyo ili kufikia mwafaka.
Nakupata vilivyo
Je tatizo kama hili yatupasa kumuona mtaalamu wa nini? Macho,mishipa, mifupa au nn
 
Unaweza kuanza na daktari wa kawaida/GP au daktari bingwa wa magonjwa ya ndani/physician kulingana na ulipo.
 
Mimi nipo Arusha je daktari wa magonjwa ya ndani anspatikana hospitali gani ?
Nilikuwa na wazo la kwenda kupiga CT scan ili nijue Nina tatizo wapi na kisababishi ili nishauriwe tiba au iekaaje hiyo
 
Naumwa kichwa nameza pain killer hakiishi,

Nikisema ninywe maji mengi muda naenda kujisaidia inabdi nishike mishipa ya kichwa kianzdi sana.

Mnisaidie
Jaribu kupima pia kansa unaweza ukawa una uvimbe kichwani
 
Mimi nipo Arusha je daktari wa magonjwa ya ndani anspatikana hospitali gani ?
Nilikuwa na wazo la kwenda kupiga CT scan ili nijue Nina tatizo wapi na kisababishi ili nishauriwe tiba au iekaaje hiyo
1: Selian/AICC/Mount Meru/NSK/Hospitals

2: Si jambo jema kwenda kwenye vipimo bila kuwa na nini kinaweza kuwa sababu au nini hasa kinaenda kuangaliwa kulingana na dalili.

Vipimo huja/huagizwa baada ya wazo la nini kinasumbua. Unaweza kufanya kipimo kikubwa na kuishia kwenye frustration. Kuna vitu vinaitwa incidental findings, lakini unakuta hakihusiani na tatizo lako la msingi au kila kitu kikakutwa kiko sawa nawe unaumwa lakini kwa uchaguzi wa kipimo ulitegemea ndo majibu yatapatikana kumbe hata kipimo hakihusiani kabisa na tatizo.

Hivyo, sikilizwa vyema kuwe na mwelekeo wa tatizo kwanza.
 
Asante sana ndugu nitaenda hospital na niwaelezee ninavyojisikia
 
1: Selian/AICC/Mount Meru/NSK/Hospitals

2: Si jambo jema kwenda kwenye vipimo bila kuwa na nini kinaweza kuwa sababu au nini hasa kinaenda kuangaliwa kulingana na dalili.

Vipimo huja/huagizwa baada ya wazo la nini kinasumbua. Unaweza kufanya kipimo kikubwa na kuishia kwenye frustration. Kuna vitu vinaitwa incidental findings, lakini unakuta hakihusiani na tatizo lako la msingi au kila kitu kikakutwa kiko sawa nawe unaumwa lakini kwa uchaguzi wa kipimo ulitegemea ndo majibu yatapatikana kumbe hata kipimo hakihusiani kabisa na tatizo.

Hivyo, sikilizwa vyema kuwe na mwelekeo wa tatizo kwanza.
Au wewe una USHAURI mwingine kuhusu matatizo yetu Mimi na mleta mada?
Kama una USHAURI
Tafadhali mtaalamu naomba utupe nitaupokea kwa mikono miwili!

Pia ushauri kuhusu maelezo ya mwanzo pindi tu nitakapofika hospili ni hatua gani muhimu nitaanza nazo

Natanguliza shukurani
 
Ushauri wangu binafsi ni:

1: Kufika hospitali na kumwona mtoa huduma ya afya/daktari.

2: Andaa maelezo mapema kufuatana na tatizo lako kwa historia, pia ukifuatilia msg #6 utakuwa na mwanga kidogo.

3: Mpe maelezo mtoa huduma ya afya kadri uwezavyo na anavyokuuliza.

4: Amini, maelezo yako ndo mwanzo wa tiba. Toa maelezo kwa kadri unavyojifahamu, usijibu kile ambacho haujakielewa au kumaliza tu consultation.

5: Uliza pale ambapo ulichoulizwa au kuelezwa hakijaeleweka.

6: Tiba yako haitokani na jina kubwa la taasisi husika bali mtoa huduma uliyekutana naye kwa matibabu atakayokupa au maelekezo ya nini ufanye kama liko juu ya uwezo wake.

NB: Kwa mtoa huduma rafiki sana huweza kukupa ni nini majumuisho/summary ya alichokipata kwako kutokana na maongezi yenu na examination na anaomba ufanye vipimo gani na kwa nini?
 
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom