Naomba tupate maelezo ya kina ya kisayansi, hivi inakuwaje mtu anashangilia na kupata furaha kali pale nchi yake au wenzake wanapopata matatizo?

Naomba tupate maelezo ya kina ya kisayansi, hivi inakuwaje mtu anashangilia na kupata furaha kali pale nchi yake au wenzake wanapopata matatizo?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Mfano hai kabisa ambao nimeshuhudia kwa macho yangu mitaani na pia katika mitandao, ni ile hamu na shauku waliyokuwa nayo baadhi ya waTz kuona ugonjwa wa Corona ukiingia Tz, na unamuona kabisa mtu huyo anaumia kila walipoambiwa kuwa ugonjwa bado haujafika.

Ile siku yule dada wa huko Kaskazini alipouleta huu ugonjwa kwa mara ya kwanza niliona nyuso za furaha, vifijo na nderemo huko mitaani as if kuna timu ya taifa imeshinda kombe la Afrika, kila mtu anafurahia kivyake, wengine wanashangilia mitandaoni, mara ooh “tutaongea lugha moja sasa” , mara ooh “ngoja tuone mtakavyondoka kama kumbi kumbi” , mara ooh “subirini wiki mbili tuone tukavyoisha”, halafu sasa unakuta zile wiki mbili zinaisha na hakuna lockdown wala hakuna watu wanaodondoka kama kumbi kumbi unaona kabisa jinsi watu wanavyoumia na kuteseka, sasa mimi niulize, hivi sisi tukifa nyiynyi mnafaidika nini? Au ni nini hasa kinachokuwa kinatembea akilini mwenu hadi mnafurahia misfortune za taifa, WHAT IS THIS?
 
Nadhani wanaoshangilia hawana Ndugu wala watoto wanaoishi hapa Tanzania, kwahiyo hayo magonjwa hayatawapata wao wala familia zao vinginevyo wasingeshangilia wala kuombea.
Pia chuki za kisiasa zimetawala sana Nchini kwetu, yaani mtu akifa kuna watu wanashangilia kisa tu kafa wa chama pinzani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ujinga tu wa watu, wazungu wanaumia kweli roho kwa nini Waafrica hawafi kama wao.. Alafu unashangaa Waafrica haohao tunaunga mkono mawazo ya wazungu tufe wengi hawajui hata wao wanaoshangilia wanaweza kufa au kupata madhara kwa janga hilo
 
Hawawezi kuja jibu hii hoja lakini mi nikuambie tu, hiyo ni tabia ya chuki na roho korosho.

Mtu mwenye roho mbaya hawezi kuona hatari inayoweza kumpata iwapo jirani yake au wa kwake akipata matatizo.

Chuki/roho mbaya huleta upofu na ukiziwi tena wa macho masikio na rohoni.

Ukiona mtu anatamani ardhi anayoikalia ikumbwe na mafuriko kisa anamchukia jirani yake huyo ni wa kumwogopa zaidi ya ukoma.

Bahati mbaya sana hii roho imewakumba watu wengi hapa nchini kisa tu wanamchukia Rais, na wanaomba usiku na mchana majanga yatokee utafikiri wao wana miadi na Mungu kwamba majanga yakitokea basi wao watakuwa salama kisha wakae pembeni na kuchekelea. Wakati mwingine ukiwaza sana unaweza hisi sio waTz hao lakini ni maraia halisi.

Ubinafsi chuki na roho mbaya vimetutawala sana sisi ngozi nyeusi. Pathetic!!
 
Kwanini mlishangilia Tundu Lissu alipomiminiwa risasi zaidi ya thelathini, tuanze na hili.
 
Kwa sababu wenye akili wanaamini kiongozi aliyepo hakushinda kihalali mfno dar hakufikisha hata kura 100000
 
Ni matatizo ya kisaikolojia ya kujitakia maana kuna watu wamejenga chuki yani wanamchukia Magufuli kupitiliza,sasa tatizo linakuja pale unapomchukia mtu halafu huna la kumfanya na yeye mambo yake yanaenda kama kawaida hapo ndipo watu wanapopata stress,kuna watu unaona kabisa hawako sawa.
 
Back
Top Bottom