Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

Sijawahi kufikiria kuishi na wakwe kabisa katika paa moja. mwenzi wa kwanza uishe wa pili 3,4,5 hadi mwaka hapana kabisa.......... Haiwezekani kabisa

Dada uzuri una kazi hakuna linaloshindikana tafuta nyumba ya bei rahisi zaidi ya hiyo jibane acha kwenda kwa wakwe kabisa hata kama nyumba mmemjengea ninyi. Fanya juu chini lakini sio kwenda kuishi kwa wakwe kabisa...

Na pia jamani hata kama uko kwenye ujenzi sio ujibane mpk tone la mwisho
Mie mwenyewe kwenda kuwasalimia tu basi inatosha hapa kwenyewe nishamaliza kazi zangu nimepumzika nipo nyuma ya keyboard sasa ukweli duu itakuwa ngumu kwenye shida sawa, mie mr alienda kusoma ng'ambu si wakaseme nikaishi kwao, mwenyewe eti haa atabaki hapa hapa haina shida, komaa tu mama

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
oh mama ako ni single mother! ebu nitolee laana mimi siyo single mother labda hao dada zako! jifunze kutokushobokea usiowajua!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
It's very stupid charty
Pole sana

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Sasa bi dada kama na wewe unafanya kazi shida nini? Kwanini msitafute nyumbani inayoendana na kipato chako mambo mengine kujitakiwa ni afadhali ukaishi kwako ukala dagaa kuliko kujipanga ukweni na watoti mmeo kanda ya ngosha nini!

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
KUMBE HUYU DADA AMEJENGA NYUMBA YAKE YA VYUMBA 3 HEBU TUMUULIZE ALIJENGA WAKATI YUKO NA MUME AU KABLA?
 
asante sana mm binafsi nimejenga nyumba ina 3 bedrooms but haina umeme mm nipo tayari kwenda tukaishi kwenye hii nyumba yangu lakini mume wangu hataki kwa kua anadai ni mbali sana usafiri tunao ila hayupo tayari kuishi ktk nyumba niliyoijenga
anataka tukaishi kwao kwa kua hiyo nyumba ya kwao aliijenga yeye ila ndio familia yote ipo humo mm nitakua na room yangu tu
yaani nachokaje sijawahi kugombana na mkwe au wifi wala shemeji naishi nao vizuri na wananipenda ila kwa kua tupo mbalimbali na nijelewa na uwezo wa kuyapuuza maudhi madogo kwa kua tulikua tupo mbali mbali sasa ninawaendea chini ya miguu yao

uuuwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Kataa hata mama mkwe akikwambia mgomee indirect bora ungeanzia kwawakwe then uje kwako kuliko utoke kwako uende kwa wakwe hyo ndoa ikimaliza mwaka mungu yu nawe

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Pole dada. Kama kuna uwezekano kataa ila kama hakuna jinsi nenda tu mama. Baada ya mwaka mmoja uje utupe mrejesho.
 
Tunaenda kushuhudia Marekani na N.Korea wakiingia kwenye mtanange ndani ya ardhi ya Tz...

Kuishi kwa wakwe unahitaji uwe na moyo wenye engine ya Boing 777...
 
Wewe ni muolewaji utabaki kuwa muolewaji sana sana utaenda kuishi kwa kuigiza no one is perfect ila mapungufu yako ndio itakuwa fimbo ya kuchapwa nayo, Kaa na mumeo mpange mipango yenu kama issue ni kipato ujue utamsadiaje ili kuepukana na issue ya kwenda kuhamia ukweni na huu ndio wakati wa wewe kuwa na msaada mkubwa kwa mumeo, huwenda mumeo anajambo zito linalomsumbua ila anashindwa kukuelezea ukweli kuhusu kipato chake huwenda anaogopa kuaibika mbele yako, pambana ujue anatatizo gani maana hayo sio maamuz ya kiume anayotaka kuyafanya.
Nyumba ya mama mkwe walijenga wao! Basically ni nyumba yao. It's not fair kupanga wakati ipo
 
Tangulia na watoto na housegirl wako atakuja tu, nina jirani mke alimfanyia hivyo hivyo, kwanza mume alinyuti na akaona freedom si ndio hii, mke akawa akija kusalimia kwa wakwe anachukua nguo moja baada ya moja, mume mwenyewe alienda, wewe wala usipige kelele wala nini, tumia akili zaidi, mara nguo, mara viatu, akikuuliza mwambie unamuandalia mazingira akija au waenda kuzifua na kuipiga pasi vizuri!
Hivi unaona huyu mama ni type ya kufua nguo za mume na kupiga pasi?
 
Ukweli mchungu, aadhani hili pia ni jibu maana huenda dada hakuwa anampa support mme wake. Kama wote mnafaanya kazi hamuwezi kushindwa kulipia hilo pango ila kwa vile dada hapo pengine anamwachia kaka issue nyingi. Kama wadau walivyosema, jaribuni kutafuta nyumba yenye kodi ya chini mhame hiyo ya sasa.
Kuna baadhi ya maneno yenye ukweli katika bandiko lako hasa kama bidada alishindwa kumpa support mme wake. Na nadhani ndo maana jamaa katapatapa na akaona ni bora akajibanze kwao wakati akijipanga. Ole wao hiyo nyumba ikamilike wakiwa ukweni au vyovyote vile yeye ajiandae tu
 
Nyie Madada Hela Zenu Huwaga Za Kwenu Tu Ila Ya Mwanaume Yenu Wote Sasa Mwanaume Kayumba Mnaponda Kwenda Ukweni

sio wanawake wote kama unavyofikiria mkuu laiti ungejua maisha ya wengine. na ukimsoma mleta mada amesema hata nyumba ambayo wanaishi wakwe naye alichangia tofauli kwa hiyo ni mtu anayeshiri kwenye pato la familia.

mkuu hakuna mtu ameponda kwenda kuishi ukweni isipokuwa mleta mada anapata kigugumizi kwenda kama ndivyo basi wajipange wote kama umenisoma vyema.......isitoshe mkuu familia zingine wakwe ni balaa unaweza kuona maisha magumu bora waendelee kupendana kama walivyo sasa.
 
Kuna baadhi ya maneno yenye ukweli katika bandiko lako hasa kama bidada alishindwa kumpa support mme wake. Na nadhani ndo maana jamaa katapatapa na akaona ni bora akajibanze kwao wakati akijipanga. Ole wao hiyo nyumba ikamilike wakiwa ukweni au vyovyote vile yeye ajiandae tu
Sana tu mkuu, si unajua hawa viumbe kwa maneno. Kaka kakosa pakushika, kaona arudi home kwanza wakati akijipanga pia stress zipungue. Kuna mdau hapo juu kasema pengine mshahara wa kaka ni wa wote, ila wa dada ni wake. So inakuwa shida kidogo but kama wanashirikiana vizuri, hawawezi kushindwa kupata solution nzuri zaidi. Kurudi home naona kama last option kwangu maana kusudio lao ni kuwa na familia yao na kuvumiliana huku wakiwa tayari kukumbana na changamoto za dunia kwa hekima na mipango halali. Naona bidada ajaribu kumpa nafasi yake mmewe kama kumuweka wazi katika kile anachokipata nakinavyotumika huenda kaka anaona unamtumika na maneno juu. Jaribu pia kubadili huu utaratibu wa kulala lala wanaume wengi hatuipendi wengi huwa hatusemi, ingawa nikikukuta umellala mchana naona sawa tu.
 
MBONA WAARABU,WAZUNGU,WACHINA NA WAPEMBA WANAISHI NA WAKWE ZAO AU WEWE MVIVU MVIVU UNANAVYO ONEKANA NDIO MAANA UNAJICONFESS KWA KUHOFIA KUWA UTASHINDWA KUISHI UKWENI
Utamaduni wa wale na sisi ni tofauti sana
 
Muulize kama wazazi wasingekuwepo mngeenda kuishi wapi?...jibu atakalo kupa ndo litakuwa sahihi,ila si kweda kwa wakwe

naomba mwenye lugha ya kejeli afunge mdomo wake[/QUOTE]
 
KUMBE HUYU DADA AMEJENGA NYUMBA YAKE YA VYUMBA 3 HEBU TUMUULIZE ALIJENGA WAKATI YUKO NA MUME AU KABLA?
Haaaa haaa wengine waume hawana nongwa hela unayo anaweza kwambia fanyia mambo yako sasa hapo ruhusa ninayo si unajenga tu, ila hajasema alijenga wakati gani!

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Ulikosea kumkubalia mumeo tena mkiwa na lengo zuri la kuokoa pesa ili mjenge...kumbe hutaki(tabia isiyo njema) Jichunguze tabia hiyo na kisha usiioneshe kwa ndugu wa mumeo. Ukiweza hilo umefanikiwa.

Waoneshe upendo na imani ili wafanye hivyo pia kwako."Children react to kind treatment by becoming confident" kwa tafsiri isiyo rasmi...mtoto hubadilika na kuwa mwema kwa kumtendea ukarimu.

Jifunze kusema hapana kwenye HAPANA na unaposema ndiyo imaanishe NDIYO.
______ni hayo tu_________

Wakati mwingine mume huenda kaamua muishi kwao ili ujifunze maisha yao na desturi za kwao,yawezekana anataka kuongeza mahusiano yako na familia yake maana siku hizi baadhibya akina dada hawapendi ukweni kwao. Inawezekana ni kutokana na ugumu mulio nao au anakupa SOMO bila wewe kujua.

Kila la heri katika ndoa yako na maisha ya ukweni

Sent from KICHWA CHANGU mwenyewe
 
Kama hutakuwa comfortable mfanye utaratibu muhamie kwenu haraka, endeleeni kupanga hivyohivyo

Sent from my Lenovo TAB 2 A7-30H using JamiiForums mobile app
 
KUNA METHALI INASEMA HIVI:
"An idle person may have just three tasks;sleeping,eating and quarrelling"

Hivyo basi kama wakwe zako hawana shuhuli..tegemea ugomvi na lawama.

Suluhisho kataa kwenda kukaa..ni aibu kwa morani kurudisha mpira kwa kipa..mwambie mumeo akaze kamba.kuna vyumba vya bei poa tu.Huko kujenga sio suala la miezi miwili tu mmehamia.
 
Tena ni bora muendelee kulipa kodi mnaweza mkajopanga mkajenga na mkahamia kabla haijaisha vizuri,, huko mnakoenda mtaenda kuyavaa majukumu mtashindwa hata kujinunulia vocha, maana kama miaka yote mawifi wapo na mashemeji wapo ila mumeo ndo aliweza mkomboa mama !!!! Mhhh bora mkapange hata chumba na sebule mbagala

Sent from my HUAWEI Y336-U02 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo miaka minne ungempa saporti mume wako mngekuwa kwenu
ngoja ukaonje joto ya mawe;
Inashangaza sana, kama anafanya kazi siku sita kwa juma, mume wake naye ni mtafuta kipato, nini kimewashinda kuweka kibanda? Chako changu, changu changu system at work!

Ila ni jambo jema kuishi pamoja kwa umoja, acha jamaa ampime level ya busara na ustahimilivu alionao mke wake. Kila la kheri
 
Back
Top Bottom