Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

Ishi kwa kipato chako.Sikatai maisha magumu ila tafuteni nyumba ya bei nafuu kulingana na kipato chenu muishi maisha yenu

Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mtazamo uliopo... Siyo tu baba na mama mke hapana.. Bali kuishi na mbali na mtu yoyote yule ambae ni ndugu, mwanafamilia au hivyo ulivyosema huepusha mambo mengi sana...

Ukiwa mbali nao, ukisemwa au kulalamikiwa au kushutumiwa as far husikii it wont hurt you...



Cc: mahondaw

Cc: mahondaw
 
Kuna vitu hivyo lazima muongee na mkubaliane sio kubebwa kama zigo....
Pia huo ni udhaifu kushindwa kulipa kodi ya pango na kukimbilia home.

Sent from my SM-G903F using JamiiForums mobile app
 
Dada yangu amini usiamini nakupa miezi sita tuu huna ndoa Mwambie Mumeo atafute sehemu ya bei ya chini muendelee kupanga ndoa itavunjika na bado mnapendana.
 
Mmh! Yataka moyo sana kuishi na ndugu wa Mume lazima tu watakufanyia vitimbi na hvi unafanya kazi ndo kabisa.na huwez kuwa comfortable chochote utakachofanya wao kitawauma bola mpange
 
Hiyo miaka minne ungempa saporti mume wako mngekuwa kwenu
ngoja ukaonje joto ya mawe;
You're very right madame! Kudos!

She stayed with her hubby for four years without any contribution of her salary in support to her hubby; she is selfish and she use her salary on her own private matters!

Today she complain about going to live with her in laws as alternative proposed by hubby to reduce living expenses; is she a mad??

Go and swallow it dude! Why women are selfish even in supporting your children and hubby in your family??
 
habari zenu wadau mm na baba watoto tulikua tunaishi ktk nyumba ya kupanga kwa muda wa miaka minne sasa ila anataka tukaishi kwao kwa kua kidogo kodi imepanda ili tusave tuweze kuanza kujenga makazi yetu sasa jamani naomba mnipe uzoefu wa kukaa na mama mkwe baba mkwe mashemeji na mawifi ndani ya nyumba mm nikiwa nina watoto wawili wadogo 3 years na 1 year mm ni mfanyakazi naenda kazini asubuhi jumatatu hadi ijumamosi siku yangu ni moja tu jumapili kiukweli mm sipo comfortable kuenda kulundikana kwenye nyumba moja yaani nipo nafuraha nikiwa naishi kwangu. si kama siwapendi ndugu wa mume lakini sipo comfortable. hebu nipeni mawazo yenu juu ya hii ishu.

naomba mwenye lugha ya kejeli afunge mdomo wake

Kwa usemi 'afunge mdomo wake' na 'kulundikana' inaonesha kwenye nyumba hiyo patakuwa na pata shika nguo kuchanika. Bora mtafute nyumba au vyumba vya bei nafuu halafu mjenge nyumba ambayo mtaamia mkiweka tu paa, milango ya kuingia ndani na madirisha ya grill na wavu wa mbu wa bei rahisi, halafu mengine yataendelea baadae.

Usijaribu kabisa kwenda kukaa huko kwani sababu za msingi unazo. Halafu hiyo 'saving' inapatikanaje? Hiyo sio saving bali kuongeza gharama huko ukweni. Kwa kifupi, utaratibu wa maisha utakuwa mgumu sana, yaani ni sawa na Uganda na Tanzania ziwe nchi moja bila kuunganisha katiba serikali na kuendelea kuwa na maraisi wenye madaraka sawa.
 
Tafuteni chumba na sebule kilicho self contained. .
Kukaa na wakwe ni shida ndugu yangu, bora niishi kama nipo stoo nimebanana huku nakomaa

Kama vitu n vingi Sana, ndio mkaombe mama awawekee mpk mtakapohamia kwenu
 
You're very right madame! Kudos!

She stayed with her hubby for four years without any contribution of her salary in support to her hubby; she is selfish and she use her salary on her own private matters!

Today she complain about going to live with her in laws as alternative proposed by hubby to reduce living expenses; is she a mad??

Go and swallow it dude! Why women are selfish even in supporting your children and hubby in your family??
Acting like you know her
 
Hutakiwi kuongea ongea kuwa kimya

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kwa usawa huu huo ujenzi mtaanzia wapi acheni utoto komaeni hata kwa chumba kimoja ila mko kweni kuliko kwenda kuishi huko

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza, ningependa kujua mazingira ya ukweni kwako.
Mnakwenda kuishi NYUMBA ya namna gani? MF chumba chako na mumeo kisha watoto wachanganyike na watoto wenzao au upande mmoja mtakuwa mnajitegemea kivyenu.au kuna vyumba vya kutosha lkn mnachangia baadhi ya mambo kama vile jiko.
Nikifahamu hayo ntakuwa na cha kuchangia


hapo nina chumba tuu jiko pata sote sebule pata sote
 
Mhh! Inategemea aina ya wakwe. Ila kwa uzoefu hapo mnaenda kukaa nyumbani na mkubali kuwa kama watoto. Kwa mujibu wa vitabu vya dini fulani, inapasa mtu aachane na wazazi na aambatane na mkewe! Hapo mnaenda kuambatana na wazazi! Yatakayowapata simooo!

Sent from my BGO-DL09 using JamiiForums mobile app

mm ndio ninavowaza nipo na mume wangu bega kwa bega kuna kaka yake ambae alikataa kushiriki kumjengea mama yao watu walimuona ni katili lakini kwa kweli ameshajenga kwake yupo na familia yake wapo nafuraha na hakukuwa na ugomvi wowte baada ya kuwaambia ukweli kuwa mm naanza kujijenga mm na familia yangu kwanza
 
asanteni sana wakuu kwa michango yenu wengi wenu kwa kweli munawaza kile ninachokiwaza mm na wale wanaoona kuwa mm pesa yangu ni yangu si kweli kwa kua wakati anahangaika kumuhifadhi mama mm nilijitoa sana ktk kuhakikisha mahitaji yetu hapo nyumabni yanakamilika na support kubwa ninatoa ktk mambo mbali mbali
 
hapo nina chumba tuu jiko pata sote sebule pata sote
Pole saana sasa hapo inabidi ujikaze kike, mshauri mumeo kama walivyotangulia kukushauri wengine nendeni mkapange NYUMBA ya kawaida ambayo mtaimudu, lkn kwa kwenda kukaa ukweni kwa malengo ya kujibana ili mjenge NYUMBA yenu. Itabidi mvumilie mengi,mchangie mengi, mwisho lawama na dhihaka huku malengo yenu hayatotimia kamwe.
 
Hakuna mbinu hapo zaidi ya kuacha roho mbaya,kujifunza kupotezea mambo na kutokuongea sana

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom