Naomba ufafanuzi: Kitu kisicho halali ni haramu, au kuna mazingira ya kufanya kisicho halali kisiwe haramu?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Kuna mtu kanichanganya hapa, naomba ufafanuzi: Kitu kisicho halali ni haramu? Kuna mazingira ya kufanya kisicho halali kisiwe haramu?
 
Kwa mfano, katika Uislamu, nyama inaweza isiwe halali lakini sio haramu kuila. Yaani, kuelekeza mnyama upande wa Kibla (Makka) wakati wa kuchinja ni Sunnah (jambo lililopendekezwa na linaleta thawabu), lakini sio sharti la lazima linalofanya nyama kuwa haramu isipofanyika. Kwa hiyo hapo kisicho halali sio haramu.
 
Uharamu au uhalali wa jambo unategemea mtu na mtu kulingana na utashi wake na jamii aliyokulia.....

Uhalali na uharamu haina mjumuisho wa moja kwa moja kwa muktadha huo wa mtu na mtu..........

Lakini kwa kawaida kinachoramisha kitu au kinachohalalisha kitu sio kitu chenyewe baada ya kupatikana au zao la kitu chenyewe bali mchakato mzima wa wewe kupata kitu hicho.....

Fedha ni halali kwa matumizi ikishaingia mkononi lakini uhalali na uharamu wa fedha Unatokana na jinsi ulivyoipata hiyo pesa!!

Aliyebeba zege na aliyeiba wote Wana shilingi elfu kumi lakini ya mmoja ni haramu na ya mwingine ni halali.......

Aliyeghushi cheti na aliyesoma na akapata cheti wote wana vyeti lakini mmoja chake ni haramu kutokana na njia aliyoitumia kukipata hicho Cheti
 
Hee, kichwa kinanizunguruka kwa maelezo!
 
Uharamu wa kitu upo kwa wasiokitumia Bongo milungi haramu na unaenda jela miaka mingi ila kenya sio mchongo wala nini
 
Kuna mtu kanichanganya hapa, naomba ufafanuzi: Kitu kisicho halali ni haramu? Kuna mazingira ya kufanya kisicho halali kisiwe haramu?
Mirungi ni haramu Tanzania, lakini ni halali Kenya.
Kwahiyo kuna mazingira ya kufanya kisicho halali kisiwe haramu.
 
Mirungi Tanzania ni haramu au siyo halali? Nadhani paleinapohusu suala la sheria neno sio halali ndio linatumika,sio haramu
 
Back
Top Bottom