Wadau wenye utaalamu na masuara ya Aviation naombeni mnisaidie hapa
Je pale inapotokea hitilafu na ndege ipo angani na same time kwamba may be Pilot anajua kwamba hii inaenda kutokea ajali.
Je hua wanawataarifu abiria au hua wanaongea maneno yapi kabla ya ajali? mwenye uelewa please.
Ndege inapopata hitilifu,ili pilot aweze walau kuinusuru lazima kuwe na mambo matatu, attitude,engine power na distance ya kutosha ili aweze kupata muda wakushughulika na pia kuwataarifu abiria. Kimsingi atawaeleza hali halisi ya kinachotokea na anachotarajia kufanya na nyie anataka mfanye nini labda,kama vile utulivu,kufunga mikanda, kuvaa oksijeni mask au kulaza kichwa mapajani..lakini mwishoni lazima atawaeleza kila mmoja kwa imani yake aombee hali ikawe sawa na sala zote utakazoona wewe.
Lakini ajali ndege za ndege huwa ni za ghafla kiasi pilot hana muda wa kuwaeleza chochote,huwa anajaribu kurekebisha hitilafu kwa mda huo mdogo alionao au anaweza asipate kbs muda wakuwaeleza abiria jambo lolote wala kufanya mawasiliano ya walio aridhini.
Ajali inapotokea,mara nyingi lazima utafiti wa kina ufanywe wakitegemea hasa 'black box'(FDR na CVR) ambazo hurekodi kila kitu kuhusiana na ndege,utafiti husaidia kujua chanzo cha ajali/hitilafu hivyo kuepusha tena ajali ya namna hiyo. All in all,ajali ya ndege inapotokea,ni miujiza watu kupona.
Imeisha tokea mara nyingi,black box imeharibika kabisa au kupotea hapo kazi ya utafiti huwa kubwa na ngumu zaidi wakitegemea kutafiti mabaki,mawasiliano ya ardhini na mashuhuda nk. Kwa ufupi ni hayo ila bado mambo ya kufanya ni mengi sana.