Naomba ufafanuzi kuhusu kibali cha kujenga

Kiti Chema

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2017
Posts
1,793
Reaction score
1,961
Habari wana jamvi,

Naombeni kuuliza au kupata ufafanuzi kwa wanaofahamu haya mambo au waliopitia hizi heka heka za serikali na mifumo ya sheria zetu za Tanzania.

Hivi inakuwa mtu unakiwanja na ulisha kilipia, kimepimwa vizuri na kina hati ya umiliki, ila unapotaka kujenga serikali inakuja kuweka zuio mpaka uwe na kibari cha ujenzi na gharama ya kibari cha ujenzi sio ya kitoto. Shida ipo wapi jamani kwa nchi yetu ya Tanzania.

Naombeni ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa haya mambo au kwa yeyote aliyewahi kukutana nalo hili.

Asanteni.
 
  • Kibali cha ujenzi ni ubunifu wa kupata mapato kwa wizara husika.
  • Unachotakiwa kufanya peleka nakala ya michoro ya jengo lako pamoja na nakala ya umiliki wa eneo
  • kama ni jengo la kawaida haitazidi laki
 
Huo ni utaratibu lazima ufuatwe. Kiwanja chako kimepimwa,kina hati mbona zoezi la kawaida hilo. Nenda manispaa kaombe kibali,tena walioweka zuio ndio watakusaidie. Usikaidi hilo zuio utajitafutia matatizo.
 
Gharama za kibari nikubwa why so,
 
Mkuu, mtu akijenga bila kibali atakumbwa na nini? Naomba ufafanuzi
Najuwa atakujibu kwa ufafanuzi, huwa wanakuja kubomoa jengo lako, i hope huu ni wizi wa kimnya kimnya coz sioni haja ya kulipia kibari wakati eneo ni lakwangu
 
Porojo? Ajenge bila kibali tuje tumshike makalio kama ulivyoshikwa wewe wakati ule. Sawa bwana mdogo?
Mkuu ukubari ukatae huu ni wizi wa kalamu kawa ulivyo wizi mwingine, maana sioni haja ya kibari kwa nyumba za kawaida tofauti na kujenga ghorofa.
 
  • Kibali cha ujenzi ni ubunifu wa kupata mapato kwa wizara husika.
  • Unachotakiwa kufanya peleka nakala ya michoro ya jengo lako pamoja na nakala ya umiliki wa eneo
  • kama ni jengo la kawaida haitazidi laki
Weee nyumba yangu ya kawaida ya chini wamenilima tsh.370,000 kibali pamoja na faini 200,000 kujenga bila kubali
 
Mkuu, mtu akijenga bila kibali atakumbwa na nini? Naomba ufafanuzi
Huwa wanapotezea tu ila wana uwezo wa kubomoa nyumba yako ila utapigwa faini . Sasa kama nyumba ina thamani 100m. Matatizo yote ya nini kama unaweza kuomba kibali?
 
Je wasipokushtukia mpaka umemaliza kujenga...umehamia...

Watakuja tena kusema "ulijengaga bila kibari au?
Wasipo kusitukia basi umepona lakini kwa vyovyote vile utasitukiwa tu maana mwenyekiti wako wa mtaa ndiye atakaye wasitua coz kunamgao wake mle
 
Back
Top Bottom