Naomba ufafanuzi kuhusu Tractors zilizotumila Afrika Kusiniin South Africa

Naomba ufafanuzi kuhusu Tractors zilizotumila Afrika Kusiniin South Africa

Sio kweli tractor jembe na tela kutoka South Africa Massey Ferguson 375 ni million kumi na tisa unaletewa mpaka dar
Tunaomba link ya kampuni iliyokuletea mpaka Dar ili tufanye mambo ya uhakika tutoe ushuhuda. Maneno yamekuwa mengi kuliko vitendo
 
Suala la bei ji kweli zipo chini na usafirishaji sio shida sana.
Shida ipo kujua je ni kweli hizo tractor zina ubora na pia je hakuna utapeli kwenye hiyo biashara?
Pia ni Muhimu kujua hizo tractor unanunua kwa ajili ya matumizi ya kilimo au vinginevyo., Maana hizo tractor ni Kubwa sana Kama ni kwaajili ya kilimo tu..na uendeshaji wake ni wa gharama..
Labda uangalie ndogo zake Kama New Holland 75 , Mahindra nk..


Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Watafute hapo
Screenshot_20211031_164215_com.whatsapp.jpg
View attachment 1993493
 
Logistics za kulileta bongo Sasa ndio kimbembe.
Meli za kutoka South Africa to Dar ni chache Sana, na kusafirisha kwa truck ni gharama kubwa sana.
Sina uhakika, nasikia Zambia kuna treni inaenda South Africa, kwa hiyo unganishe na Tazara
Kweli kabisa mdau na meli yenye uhakika zaidi from south to dar port ni ya kampuni ya messina hii inabeba kontena au hoegh zile za wanorway zinazobeba magari...
 
Hiyo kampuni ya Agricom ipo TZ lakini inauza matrekta mapya tu na choice ni kati ya Swaraj (India) na Kubota (Japan). Mimi nimenuanua Swaraj 855 (55 hp), kwa millioni 36,000 za Kitanzania. Kumbuka materkta hayana kodi TZ kwa hiyo bei za TZ ni chini kuliko nchi nyingi.. Ukiagiza zee toka SA utauziwa na kodi yao.

Kwa vile nilikuwa sina pesa ya kutosha, nililipa millioni 22, na millioni 14 ukawa mkopo wa riba ya 15 kwa mwaka mmoja. Majembe nitanunua baada ya kumaliza kulipia trekta. Jembe 3 ni millioni 5, na trailer millioni 7.5. Ukiagiza SA, ukalipia usafiri mpaka kufika TZ hiyo pesa inaweza kutosha kununua Swaraj 855 (55 hp) mpya. Ukinunua trekta kwa r200,000 ni sawa na tsh millioni 32. Ukiongeza millioni kwa cash au mkpo unapata Swaraj mpya.

Swaraj inatengenezwa na kampuni ya matrekta ya Mahindra. Mahindra ni ya tatu kwa mauzo USA. Waliyonunua Swaraj wanaisifu kwa matumizi mazuri ya mafuta na bei nafuu za vipuri. Google Agricom uwatafute. Wana offisi za kanda Dar, Morogorio, Kahama, na Mbeya. Try them, you will not regret. I need to declare that I am not affiliated with Agricom TZ but I am their customer.
Kwa huu uzi nimevutika na hii swaraj japo cjawah itumia I wish one day nikiwa njema nijaribu hii Trekta naonaga mashambani kana fujo sana kama boda boda za kkoo
 
Wale wadau wa trekta kuna wasap group tukutane tusaidiane ushauri na utatuzi wa haya mambo nicheki 0653 639214
 
 
Logistics za kulileta bongo Sasa ndio kimbembe.
Meli za kutoka South Africa to Dar ni chache Sana, na kusafirisha kwa truck ni gharama kubwa sana.
Sina uhakika, nasikia Zambia kuna treni inaenda South Africa, kwa hiyo unganishe na Tazara
kwan kuliendesha mdog mdgo mpaka bongo haiwezekan???
 
Kwa huu uzi nimevutika na hii swaraj japo cjawah itumia I wish one day nikiwa njema nijaribu hii Trekta naonaga mashambani kana fujo sana kama boda boda za kkoo
Swaraj trekta ya kimasikini ipo poa
 
Nilikuwa songea juz Kati nikamkuta bwana mmoja anamassey 90hp amechukulia msumbiji chuma inanguvu ad inaboa anasema katumia 31m liko vzur Ni 4wd linaweza bomoa hata barabara ya lami tatizo jamaa akawa hatak kuwa muwazi namna ya kupata msumbiji anahsi nitaharibu biashara yake ya kulima mashamba ya watu! Naomba mwenye maelezo ya kupata kwa msumbiji aje maana pale karbu sio km SA
 
Back
Top Bottom