Naomba ufafanuzi toka wafuasi wa CCM na viongozi wao - Mabeberu ni kina nani, ni nchi wahisani au wafadhiri?

ubeberu ni neon kongwe sana. hutumiwa na watu waliochoka kufikiri na kujenga hoja. kwenye dunia hii ya globalization/ utandawazi kila mtu anamuhitaji mwenzie. una Tanzanite sawa unaviwanda vya kuifanya iwe vitu? wakigoma kuinunua yanakuwa mawe ya kusugulia miguu tu yale. watueleze kilichotokea kwenye MKONGE. Zimbabwe iliitwa KAPU la chakula walivyoanza ujinga wao leo wanawaomba wazungu poo hata mkate sheeda
 
Kuna mahali nimesema hapo juu kuwa Magufuli na watu wake wanafikiri wanaweza kulitumia kama alivyofanya Nyerere, wakisahau kwamba enzi za Nyerere hili neno lilikuwa muafaka lakini sio siku hizi.

Nani siku hizi unasikia anaita watu makabaila?
 
Tanzania na wanasiasa wake hii ni utamaduni wao. Kila siku kuziita nchi za nje kama wakoloni, mababeru, masultani na adui wa nchi, lakini wakati huo huo wanawakimbilia na kuwapigia magoti kila leo kuomba misaada kwao na kuwaita marafiki wa nchi hii.
Unafiki wa hali ya juu!
 
10 September 2020

Tundu Lissu awahoji CCM Mpya Mabeberu ni nani

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…