Naomba ufafanuzi toka wafuasi wa CCM na viongozi wao - Mabeberu ni kina nani, ni nchi wahisani au wafadhiri?

Naomba ufafanuzi toka wafuasi wa CCM na viongozi wao - Mabeberu ni kina nani, ni nchi wahisani au wafadhiri?

Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
ubeberu ni neon kongwe sana. hutumiwa na watu waliochoka kufikiri na kujenga hoja. kwenye dunia hii ya globalization/ utandawazi kila mtu anamuhitaji mwenzie. una Tanzanite sawa unaviwanda vya kuifanya iwe vitu? wakigoma kuinunua yanakuwa mawe ya kusugulia miguu tu yale. watueleze kilichotokea kwenye MKONGE. Zimbabwe iliitwa KAPU la chakula walivyoanza ujinga wao leo wanawaomba wazungu poo hata mkate sheeda
 
Kuna mahali nimesema hapo juu kuwa Magufuli na watu wake wanafikiri wanaweza kulitumia kama alivyofanya Nyerere, wakisahau kwamba enzi za Nyerere hili neno lilikuwa muafaka lakini sio siku hizi.

Nani siku hizi unasikia anaita watu makabaila?
 
Tanzania na wanasiasa wake hii ni utamaduni wao. Kila siku kuziita nchi za nje kama wakoloni, mababeru, masultani na adui wa nchi, lakini wakati huo huo wanawakimbilia na kuwapigia magoti kila leo kuomba misaada kwao na kuwaita marafiki wa nchi hii.
Unafiki wa hali ya juu!
 
10 September 2020

Tundu Lissu awahoji CCM Mpya Mabeberu ni nani

Back
Top Bottom