Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Pamoja sana mkui
 
Mkuu nashukuru zaidi kujifunza mengi kwenye thread zako kwer wewe si mchoyo
Swali: naanza vipi nikihitaji kukodi shamba huko bonde la ruvu mkuu.
 
Hiyo Bei ya broiler ya Shilingi elfu saba. wewe upo wapi mkuu?
 
Hongera sana ONTARIO,

Swali langu la kwanza:
Ni wakati gani hasa ulipoamua kuachana na kununua chakula kwa ajili ya kuku wako wa broiler. Hapa naomba utueleze kwa ukubwa wa project ilipofikia. Ulifuata hatua gani mpaka kufanikiwa na changamoto zake ni zipi?

Swali la Pili:
Uliwezaje kwa mara ya kwanza kufanya biashara ya export maana nimeona uliexport vitunguu. Ulipataje Masoko, process za kuexport mpaka kufikisha mzigo. Tueleze na changamoto zake pia

Swali la tatu:
Nimeona umefanya packaging za kuku. Una process mwenyewe kuku wako wote?

Nisaidie kujibu, niendelee na maswali mpaka tuelewane mkuu
 
Mkuu ungekuwa na group la watsap ukatuunga humo then ukawa unatupa darasa ungetutoa sana.
 
daaah we dogo saafi saaana aisee nikija bongo nitakutfta mdogo wangu. Mimi nilikuwa na na nina experience saaana na vitunguu maji kwa miaka kama kumi hivi nimelima kitaaalam saana ila tatzo niligundua kuwa soko linazngua saaana saaana hapo bongo. ilifikia hatua nikaachaga kulima nikaenda kuwa dalali wa vitunguu huko mabibo hii yote ilikuwa ni mbinu ya kufanya research ya masoko ya vitunguu nilikaa miez minne nikaelewa saaana na baada ya hapo nilirudi shambani nikawa nalima kinyume na msimu. Hapo nilipata faida saaana. kuna kipind nilitembelea israel nikaona vitunguu swaum so nikapanga nikarud tz nikamwambia kakaangu tulime vitunguu swaum lakini jamaa akakataa akasema vinakubali maeneo ya baridi. wakat israel niliona vinalimwa open space jamani. sikukubaliana nae. nikajipanga nikalima ka shamba kangu ka nusu hekari nikatumia utaalamu waangu woote wa zao la kitunguu maji na nilisoma na nikaenda kuwatembelea baadhi ya wakulima huko mbeya nikajifunza nikaja kufanya kwa practical aisee amini usiamni kaka nilipiga gunia zangu kadhaa za vitunguu swaum tangu hapo nikawa mkulima mzuri saana wa vitunguu aisee. kwa hyo jamani msisikilize ya watu mimi home tz nalima had zabibu. kilimo kinalipa ila KILIMO AFRIKA BILA KUJUA SOKO NI SAWA NA KUPAKA RANGI UPEPO. Zaid ya Mbwa wa ulinzi wa kipolisi/kijeshi, mbuzi, bata mzinga na ng'ombe wa maziwa sijawah fuga. Mimi nimejifunza kuwa specific ktk jambo unalofanya. yaani amua nini unataka kufanya na ujikite huko. mimi nilijikita ktk vitunguu na hapo hunidanganyi lolote may be masoko ya nje ndio sijawah uzia huko na hapo ontario mdogo wangu utanisaidia nikija bongo. Nalima mbaazi, mpunga na ninasaga nyama na kutengeneza sausage pia na mikate. kwa hyo naenjoy, NIMESOMA FINANCIAL ENGINEERING lakin moyo wangu uko kwenye kilimo jamani. i miss home nikija nitakutfta mdogo wangu. nikusaidie forex (japo nimesimama kidogo).
 
Forex nayo unafanya ndugu??
 
ONTARIO Kwanini ulikuwa kimya miaka yote hiyo huko nyuma Chief? Anyways....in life it is never too late! Endelea kutujuza na kutufungua zaidi kuhusu fursa na namna ya kuziendea.
Bless u
 

Mkuu heshima yako, naona umeongelea seals la focus kwenye zao moja ili kujenga ubobezi lakini upande mwingine unaongelea kwamba unalima mazao mengine mengi ukiacha kitunguu.

Upo sahihi kuhusu focus lakini diversification nayo ni muhimu sababu Kama ilivyosema kuwa soko haliweleweki bongo ndio maana inabidi ulime mazao mengine ili kufidia yake ambayo hauto pata faida sababu ya soko kuwa baya

Nimependa maamuzi yako ya kwenda kuwa dalali, it was a very smart move. Ngoja tumsubiri ONTARIO pengine atatupa una na Wa kwenda kuuza kitunguu Kenya maana hata Mimi nimemuuliza lkn hajajibu

Mwisho
1. naomba unisaidie pale mabibo ni miezi gani kitunguu maji kinakuwa adimu?

2. Ukiacha mabibo wapi kwengine ulikuwa unauza mzigo?
 
Mkuu Ontario, nataka kulima vitunguu na mihogo shamba lipo mkoa wa Pwani. Je, ni mwezi/wakati gani hasa natakiwa kulima na kupanda mazao hayo ili kuwa na timing nzuri ya soko la Dar ?Natanguliza shukrani.
 
hyo ndo chanzo cha mtaji wangu kaka, japo nimenunua currency na kutunza, lakini hyo ndo imenitoa na kuweka hapa nilipo
 



ni kweli usemalo kaka ila licha ya diversification jiwekee wewee zao ambalo hata akija mtu ajue wewee ni nan hasa ktk anga hizo. mimi diversification ndo nilifanya kwenye mazao hayo niliyoyataja hapo pia kuongezea nilifanya ktk mazao ambayo hayana usumbufu kwa mkulima. mfano mazao kama dengu na mbaazi (zile za muda mrefu acha hizi za muda mfupi ambazo zinashambuliwa na madudu na hivyo kupoteza maana ya mazao ambayo hayana usumbufu). hayo ndo hayana usumbufu kabisaa. kwa upande wa swali lako la kwanza kaka.

1. kwanza kabisaa naomba uelewe kuwa kitunguu maji au kitunguu swaum hakipend mvua saana maana husababisha saaana bulb kuoza pia huambatana na magonjwa ya ukungu sugu pamoja na wadudu wakatao na wafyonzao. hvyo wakata wa masika huwa ni changamoto saaana saaana. na ndio maana kitunguu wakat wa kuanzia mwez wa 12 (kuanzia tarehe 20) huwa kinapanda saaana bei. ndo unakta wakat mwingine kama mwaka 2014 gunia lilifika Tsh 250,000/=. lakini kuna mwaka pia licha ya mwezi december zao hili hushuka hii ni kutokana na watu kuwahi kulima mapema kama mwaka huu nasikia mambo yalikuwa mabaya maana mvua zilichelewa na watu kibao walilima kwa kumwagilia. so all in all ni mwez wa 12 mpaka wa pili au 3 huwa ni miez mizuri kuuza ila kuanzia wa sita vitunguu huwa vinafurika saaana kutoka mang'ola huko na kwingineko halia huwa inabadilika na soko hushuka saaana.

2. Nje ya mabibo nilipataga chaka la wakenya maeneo ya kondoa huko wakipitia Arusha niliunganishwa na watu wa Balton. hao nao wako poa na bei zao ni nzuri.
so nakuhimiza tena na tena usilime kama hujui soko la bidhaa zako likoje. mimi nilikuwa nalijua saaana soko la ndani la vitunguu maji na ndio maaana kwa taarifa sahihi za soko nilikuwa napanga bei na sio kupangiwa na madalali.

kila la kheri kaka
 
Ontario unafanyaje hadi unapata faida

Maana na Mimi nafuga lakin nahisi kuacha maana chakula kimepanda sana bei na bei ya kuuzia ni ile ile

Nimejaribu kununua malighafi lakn bado naona gharama ziko juuu

Pia mimi nina tatizo kama lako nawaza tu kuachana na hii biashara ya kuku maana sioni faida yoyote
 
Sawa nimekupata

Ila sasa nilikuwa naomba unisaidie ratio ya chakula cha broiler
Stats,grower na finisher

Pia mfano Kuku 500 unalisha mifuko mingapi?
Ontario jamani hapo kwenye mifuko hapo ndio nachanganyikiwa kabisa embu niambie nawapa hadi mifuko 37 kwa kuku 500 ndio maana sioni faida kabisa
 
Reactions: 454
Hizo picha za Kuku wakiwa handani baadhi sio zako mkuu kama unabisha nikuletee ushahidi hapa
 
Reactions: 454
Kenya wanazalisha vitunguu kwa saaa mkuu hakuna tena soko kule. Wanalima sana tena mno. kwa sasa hawachukui sana vitunguu Mang'ora Karatu kama zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…