KERO Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uondoe CCTV Camera zilizowekwa chooni

KERO Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uondoe CCTV Camera zilizowekwa chooni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

sitagliptin

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2023
Posts
1,208
Reaction score
2,525
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ya Upanga, tafadhali fanyeni busara kuziondoa kamera ambazo zimefungwa chooni.

Sio busara, sio ustaarabu, ni kuingilia faragha za watu. Chooni ni eneo nyeti sana usiri mkubwa sana.

Nimeshangazwa kukuta kamera zimewekwa ndani chooni, eneo ambalo mkoaji anafungua zipu akojoe juu kamera hiyooo Janab na timu yake wanakuchungulia.

Sababu yao baada ya kujaribu kudadisi ni kutokana na wizi wa koki za mabomba chooni.

Ushauri: waweke mabomba marefu ambayo mtu hata akiiba mfukoni halingii na pia wazuie mtu kuingia na beg chooni.

Hata aliweka ile kesho akienda lodge halafu akute kuna kamera lazima akimbie hapo aende kwingine halafu meneja alete majibu eti kwa sababu ya wateja wanaondoka na mashuka au mataulo ikabidi tufunge kamera.

Lamba makofi kabisa bili kwa mangi.

Kamera chooni ni kashfa na ni unyanyasaji mkubwa sana kwa wateja wenu.

Wahusika tunaomba hili mlifanyie kazi sheria za kitaifa na hata kimataifa hapa zinagoma.

Kwa sababu ya sheria za hospitali picha imekuwa ngumu kuiweka hapa.

photo_2024-06-20_14-23-13.jpg

Pia soma ~ Hospitali yaTaifa ya Muhimbili kweli mmeamua kutuvua nguo kwa kufunga camera kwenye vyoo, hamjui mnaingilia faragha zetu?
 
Back
Top Bottom