Naomba Ushauri: Gari gani linamfaa mstaafu.

Toyota Vitz ama Ist
 
Yupo mji mdogo, matumizi yake ni kwenda sokoni, kanisani n.k labda ikitokea na safari ndefu ya kwenda kwao na familia kilometers kama 700 hivi.
700kms.??? Mstaafu atakuwa anaendeshwa?
 
Mstaafu ukimnunulia Subaru Forester ya 2008 hio lazima apate presha...ila kuna watu wana maisha magumu gari anakuja nunua akistaafu daah hatari sana...
 
Mstaafu ukimnunulia Subaru Forester ya 2008 hio lazima apate presha...ila kuna watu wana maisha magumu gari anakuja nunua akistaafu daah hatari sana...

Ndio hivyo maisha ya walimu Tanzania, Hela yenywewe ya basic needs ni shida, ije iwe ya gari. Halafu unakuta mtu anasomesha, kwahiyo unaangalia priorities. Najua wapo wenye magari lakini ni kama nilivyosema hapo juu kila mtu na priorities zake na maisha yake jinsi yalivyokaa eg. Anawatoto na wategemezi au hana. Lakini cha msingi zaidi ni furaha, magari na vingine hivyo ni vya ziada.
 
Yupo mji mdogo, matumizi yake ni kwenda sokoni, kanisani n.k labda ikitokea na safari ndefu ya kwenda kwao na familia kilometers kama 700 hivi.

Kama unampenda mstaafu usimnunulie gari vinginevyo unamuwaisha na kifo. Umri huo anastahili kufanya sana mazoezi hasa ya kutembea ili kuuweka mwili wake fit. Umri huo ndo wa kuandamwa sana na non communicable diseases kwa hiyo mazoezi ya kutembea mara kwa mara kutamfanya azidi kua imara. Magari yana pressure zake kama hakuwahi kumiliki gari akiwa kazini kwa sasa litamtia pressure na kumuwaisha kwa sir God. Pressure za kupaki gari ikiwa nzima then unaamka asbh haiwaki ukienda kwa fundi anakwambia sensor imkufa na inauzwa laki 4 hizo zitamuua
 
Sawa mkuu nimeelewa...
 
😁😁😁😁 huwa na enjoy sana!
 
Hii ndiyo jamii forum.....
Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake....

Na mimi natoa mawazo yangu....
Mstaafu kama ni wa kufa mapema atakufa mapema tu bila kujalisha ana gari au hana....inategemea life style aliyokuwa nayo tangu ujanani....

Ni kweli kuna baadhi ya watu wakiwa na gari wanajizembea, hawatembei tena kwa miguu....na hawafanyi kazi zozote za kuwatoa jasho

Binafsi mstaafu ambaye ni Mwalimu, Mwanajeshi au Polisi....hawa watu sina wasiwasi nao....huwa hawajiweki kizembe hata wakiwa na magari 10....miili yao ilishazoea kutembea sana, kusimama sana na kufanya kazi nyingine za mikono...

Mstaafu akiwa na kazi zake za kawaida za mikono za kika siku zinazomtoa kajasho kidogo, ni zoezi tosha....
Sioni tatizo akiwa na usafiri wa kwenda sokoniz kanisani, harusini siku amealikwa au safari nyingine binafsi......

Binafsi bado naunga mkono wazo la mstaafu kuwa na usafiri...cha msingi aendelee kufanya kazi zake za mikono mfano kufua, kudeki, kuosha vyombo, kuhudumia bustani zake za mboga mboga na matunda....hizo movements ni zoezi tosha...
Pia apunguze matumizi ya nyama nyekundu, na azidishe mboga mboga na matunda, apende ibada...
Hapo mstaafu atafurahia maisha..
 
Tafuta vitz yenye engine ya 2sz na gear box ya Cvt... Ila old modal kwakua ipo juu, hato jutia.. Cheap , reliable, easy to maintain, fuel economy ipo juu kuliko sana. Angekua anaishi mahala barabara ni poa angenunua suzuk ke cc 650. Kumbuka huyu ni mstaafu... Anahitaji umakini sana kwenye matumizi ya pesa yake so she must be wise when it comes to financial decisions.
 
My take. Anunuwe Toyota Isis au Wish itamfaa sana kama yupo maeneo ya town yenye lami
 
Upo sahihi hata sisi zamani tuliishi kwa kutembea sana kwa sababu hakukua na vifaa vya kutosha baada ya maendeleo ya technolojia hasa ujio wa magari na boda boda tumejikuta taratiibu tunaanza kua wavivu na ni automatic vyombo hivi vimetulemaza.

Je vipi suala la pressure za kumiliki vyombo vya moto kwa mstaafu atakabiliana nazo?
 
Ila nikosa sana kununua gari uzeeni, kosa sana!!!
 
Kama ameshakamilisha yale mambo ya msingi mfano kusomesha, kujenga nyumba ya familia, kuweka vitega uchumi vya kula uzeen, nadhani ataweza kukabiliana na changamoto za kumiliki gari....
Pia anunue gari ambalo halijatumika kwenye mikono ya watanzania...hapo atakuwa na uhakika wa kuendesha miaka kama 5 bila kupata changamoto kubwa kubwa...yeye atakuwa anabadi oil ya engine na transmission, brake pads, bushes, plugs, matairi na mambo mengine ambayo ni ya kawaida sana kulingana na hali ya barabara zatu.....
Wastaafu wengi wanashikishwa magari mabovu, ndiyo yanaenda kusaidia kuchochea umasikini uzeeni.....kununua gari mkononi mwa mtanzania ni sawa na kucheza kamari...unaweza ukala au ukaliwa...
Nina mtumishi mwenzangu hapa kazini kauziwa IST namba C milioni 6, kwa kweli inamtesa...hiyo milioni 6angeongeza 2, angeweza kupata gari kule beforward ambaloangeendesha miaka 4 bila shida....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…