General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,064
Achukue corolla runx au allex ya cc 1500...
Ni ngumu hizo
Ni ngumu hizo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Toyota Vitz ama IstMama yangu ni mwalimu na anastaafu mwaka huu, na alikuwa anafikiria kununua gari. Kati ya haya lipi unaona linamfaa kwa budget isiyozidi 18M?. Mimi nilikuwa nafikiria haya, unaweza kuongeza unayodhani yanafaa zaidi.
Forester 2007 (najua 08 ndio bora zaidi lakini budget ndio tatizo)
Nissan xtrail.
700kms.??? Mstaafu atakuwa anaendeshwa?Yupo mji mdogo, matumizi yake ni kwenda sokoni, kanisani n.k labda ikitokea na safari ndefu ya kwenda kwao na familia kilometers kama 700 hivi.
Ili aanze ligi na Crown sio mkuu miezi mitatu tu pensheni yote imeisha hahahaAnunue Fuga tu mkuu [emoji16]
Mstaafu ukimnunulia Subaru Forester ya 2008 hio lazima apate presha...ila kuna watu wana maisha magumu gari anakuja nunua akistaafu daah hatari sana...
Mtafutie Nissan X-trail cheap (CIF), fuel economy na easy to maintain.Ya safari ndefu atakuwa anaendeshwa.
Yupo mji mdogo, matumizi yake ni kwenda sokoni, kanisani n.k labda ikitokea na safari ndefu ya kwenda kwao na familia kilometers kama 700 hivi.
Sawa mkuu nimeelewa...Ndio hivyo maisha ya walimu Tanzania, Hela yenywewe ya basic needs ni shida, ije iwe ya gari. Halafu unakuta mtu anasomesha, kwahiyo unaangalia priorities. Najua wapo wenye magari lakini ni kama nilivyosema hapo juu kila mtu na priorities zake na maisha yake jinsi yalivyokaa eg. Anawatoto na wategemezi au hana. Lakini cha msingi zaidi ni furaha, magari na vingine hivyo ni vya ziada.
😁😁😁😁 huwa na enjoy sana!Kama unampenda mstaafu usimnunulie gari vinginevyo unamuwaisha na kifo. Umri huo anastahili kufanya sana mazoezi hasa ya kutembea ili kuuweka mwili wake fit. Umri huo ndo wa kuandamwa sana na non communicable diseases kwa hiyo mazoezi ya kutembea mara kwa mara kutamfanya azidi kua imara. Magari yana pressure zake kama hakuwahi kumiliki gari akiwa kazini kwa sasa litamtia pressure na kumuwaisha kwa sir God. Pressure za kupaki gari ikiwa nzima then unaamka asbh haiwaki ukienda kwa fundi anakwambia sensor imkufa na inauzwa laki 4 hizo zitamuua
Hii ndiyo jamii forum.....Kama unampenda mstaafu usimnunulie gari vinginevyo unamuwaisha na kifo. Umri huo anastahili kufanya sana mazoezi hasa ya kutembea ili kuuweka mwili wake fit. Umri huo ndo wa kuandamwa sana na non communicable diseases kwa hiyo mazoezi ya kutembea mara kwa mara kutamfanya azidi kua imara. Magari yana pressure zake kama hakuwahi kumiliki gari akiwa kazini kwa sasa litamtia pressure na kumuwaisha kwa sir God. Pressure za kupaki gari ikiwa nzima then unaamka asbh haiwaki ukienda kwa fundi anakwambia sensor imkufa na inauzwa laki 4 hizo zitamuua
Upo sahihi hata sisi zamani tuliishi kwa kutembea sana kwa sababu hakukua na vifaa vya kutosha baada ya maendeleo ya technolojia hasa ujio wa magari na boda boda tumejikuta taratiibu tunaanza kua wavivu na ni automatic vyombo hivi vimetulemaza.Hii ndiyo jamii forum.....
Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake....
Na mimi natoa mawazo yangu....
Mstaafu kama ni wa kufa mapema atakufa mapema tu bila kujalisha ana gari au hana....inategemea life style aliyokuwa nayo tangu ujanani....
Ni kweli kuna baadhi ya watu wakiwa na gari wanajizembea, hawatembei tena kwa miguu....na hawafanyi kazi zozote za kuwatoa jasho
Binafsi mstaafu ambaye ni Mwalimu, Mwanajeshi au Polisi....hawa watu sina wasiwasi nao....huwa hawajiweki kizembe hata wakiwa na magari 10....miili yao ilishazoea kutembea sana, kusimama sana na kufanya kazi nyingine za mikono...
Mstaafu akiwa na kazi zake za kawaida za mikono za kika siku zinazomtoa kajasho kidogo, ni zoezi tosha....
Sioni tatizo akiwa na usafiri wa kwenda sokoniz kanisani, harusini siku amealikwa au safari nyingine binafsi......
Binafsi bado naunga mkono wazo la mstaafu kuwa na usafiri...cha msingi aendelee kufanya kazi zake za mikono mfano kufua, kudeki, kuosha vyombo, kuhudumia bustani zake za mboga mboga na matunda....hizo movements ni zoezi tosha...
Pia apunguze matumizi ya nyama nyekundu, na azidishe mboga mboga na matunda, apende ibada...
Hapo mstaafu atafurahia maisha..
Upo sahihi hata sisi zamani tuliishi kwa kutembea sana kwa sababu hakukua na vifaa vya kutosha baada ya maendeleo ya technolojia hasa ujio wa magari na boda boda tumejikuta taratiibu tunaanza kua wavivu na ni automatic vyombo hivi vimetulemaza.
Je vipi suala la pressure za kumiliki vyombo vya moto kwa mstaafu atakabiliana nazo?